Ofisa wa Idara ya Biashara wa Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) Lily Fungamtama
akizunguza na wageni mbalimbali waliotembelea katika banda la ATCL
katika maonyesho ya biashara ya TANTRADE viwanja vya Sabasaba leo.
Mmoja wa akina mama ambaye jina
lake halikupatikana akiwa katika picha huku akionyesha mfano wa ndege
mpya ya 787 Dreamliner inayotarajiwa kuwasili hivi karibuni. Hapa ni
kama anasema “Kitu cha Dreamliner 787 hichooo”
…………………………………………………………………..
WATANZANIA nchini wametakiwa
kukaa mkao wa kukalia kiti cha ndege mpya ya Dreamliner 787 itakayokuwa
na uwezo wa kubeba abiria 262 ambayo inatarajiwa kuwasili nchini hivi
karibuni.
Hayo yamesemwa leo na Ofisa wa
Idara ya Biashara wa Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) Lily Fungamtama
wakati anazungumza na wananchi waliofika kwenye banda la ATCL lililopo
kwenye Maonesho ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea Sabasaba jijini
Dar es Salaam.
“Watanzania wakae mkao wa
kukakilia kiti cha ndege mpya yenye uwezo wa kubeba abiria 262 .Ndege
ambayo inauwezo wa kukaa angani muda mrefu,”amesema Fungamtama.
Ameongeza kuwa watanzania wana
kila sababu ya kumuunga mkono Rais Dk.John Magufuli kwa kuhakikisha
wanapanda ndege hiyo yenye uwezo wa kusafiri masafa marefu.
Amewahakikishia wananchi wote
kuwa ATCL imejipanga kutoa huduma bora na za kisasa na kufafanua kuwa
wafanyakazi wa ndege zao wamepikwa katika kutoa hduma bora na
kuzingatia heshima na maadili ya mtanzania.
Ameongeza kuwa wafanyakazi wa
ndege wameandaliwa vema kupitia chuo cha ATCL Training Institute ambacho
jukumu lake ni kuandaa wafanyakazi wenye viwango bora vya kutoa huduma
katika ndege za shirika hilo.
“ATCL tunatoa huduma katika
kiwango cha juu kwa kuzingatia misingi ya maadili ya
mtanzania.Tumejipanga vema kuwahudumia Watanzania wote na kwa sasa
tunasubiri ujuo wa ndege mpya ya Dreamliner,”amesema.
Mmoja ya wananchi waliofika
kwenye banda la ATCL ambaye jina halikupatikana alisikika akisema
hajapanda ndege ya Bombardier lakini atahakikisha Dreamliner 787
anaipanda.
“Hii Dreamliner lazima nitaipanda
tu maana kutoka Tanzania hadi Mumbai nchini India tunasafiri angani
bila kuchimba dawa.Lazima niipande tu na ni vema nikamuunga mkono Rais
wangu kwa vitendo,’amesema.
No comments :
Post a Comment