Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu
(Watu wenye Ulemavu) Mhe.Stella Ikupa akizungumza jambo wakati wa
ufunguzi wa warsha ya mashauriano juu ya uwajibikaji wa masuala ya Watu
wenye Ulemavu iliyoshirikisha Wizara,Taasisi na Waratibu wa madawatu
yanayoshughulikia masuala ya wenye ulemavu iliyofanyika Juni 27 na 28,
2018 Morena Hotel Jijini Dodoma
Mkuregenzi wa Shirika la ADD
Tanzania Bi. Rose Tesha akizungumza jambo na washiriki wa mkutano huo
(kulia kwake) ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Watu wenye Ulemavu)
Mhe.Stella Ikupa (kushoto kwake) ni Mwenyekiti wa Shirika la Vyama vya
Watu wenye Ulemavu Tanzania (SHIVYAWATA) Bi. Ummy Nderiananga.
Kaimu Mkuu Kitengo cha Wenye
Ulemavu Bw. Jacob Mwinula akizungumza na washiriki kutoka kwenye Wizara
na Taasisi mbalimbali juu ya ujumuishwaji wa masuala ya Watu wenye
Ulemavu walipokutana Jijini Dodoma 28 Juni, 2018.
Mmoja wa wajumbe wa warsha hiyo
Bw. Kaganzi Rutachwagyo akielezea jambo kwa washiriki (hawapo pichani)
waliohudhuria warsha hiyo Jijini Dodoma.
Baadhi ya washiriki wakifuatilia
igizo fupi lililokuwa likielezea jinsi gani jamii imekuwa ikiwatenga
Watu wenye Ulemavu kupata huduma mbalimbali ambazo katika jamii.
Baadhi ya washiriki wakifuatilia
uwasilishwajji wa mada mbalimbali katika warsha hiyo, (Katikati) ni
mkalimani wa lugha za alama Bi. Hawa Manyilika akimfafanulia Bw.
Frolence Libogoma (mwenye uziwi).
Sehemu ya washiriki wakifuatilia mada zilizowasilishwa.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu
(Watu wenye Ulemavu) Mhe.Stella Ikupa akiwa kwenye picha ya pamoja na
washiriki wa warsha hiyo mara baada ya ufunguzi rasmi uliofanyika Jijini
Dodoma Juni, 2018.
(PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU
…………………….
NA.MWANDISHI WETU
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu
(Watu wenye Ulemavu) Mhe.Stella Ikupa ameiasa jamii kutokuwa kikwazo kwa
watu wenye ulemavu kupata haki ya kuoa na kuolewa kutokana na
mitazamo
hasi inayowagandamiza.
Rai hiyo ameitoa wakati wa
kufungua Warsha ya siku mbili Juni 28 hadi 29, 2018 iliyofanyika katika
Hoteli ya Morena Jijini Dodoma.
Lengo kuu la warsha hiyo lilikuwa
kujadili na kupeana mikakati ya namna bora ya ujumuishwaji, usimamizi na
utekelezaji wa masuala ya Watu wenye Ulemavu ambapo ilihusisha Wizara
na Taasisi zinazohusika na masuala ya Watu wenye Ulemavu nchini pamoja
na Waratibu wa madawati ya Watu wenye Ulemavu kutoka katika Wizara na
Taasisi mbalimbali.
Waziri Ikupa alieleza kuwa jamii
inapaswa kubadili mitazamo hasi inayokiuka haki za watu wenye ulemavu
kwani kumekuwa na mila na desturi potofu za kuwaona watu wenye ulemavu
kama wasiojiweza na wasiostahiri kuwa na mahusiano ya kimapenzi na mtu
asiye na ulemavu.
“Jamii inapaswa kuwathamini na
kuwapa fursa sawa watu wenye ulemavu hususan kwa kuheshimu maamuzi yao
na kuwapa uhuru katika kuchagua watu sahihi wa kuishi nao pasipo vikwazo
vyovyote,”alisema Ikupa
Naye Mkurugenzi wa Shirika la Action on Disability and Development (ADD)
Bi. Rose Tesha alifafanua umuhimu wa kuangalia makundi ya watu wenye
ulemavu katika kupewa haki na usawa katika maamuzi ya kimsingi ikiwemo
maamuzi ya kuchagua wenza wao katika maisha ya ndoa.
“Kimsingi ni kuangalia namna gani
watu wenye ulemavu wataweza kupata fursa sawa kama aliyo mwanadamu
mwingine kwa kutambua ni nini wanahitaji kufanya katika jamii yao
sambamba na malengo waliyonayo, kwa kufanya hiyo itasaidia kutatua
changamoto zinazowakabili,” alisema Tesha.
Aidha, Kaimu Mkuu wa Kitengo cha
Wenye Ulemavu Ofisi ya Waziri Mkuu Bw. Jacob Mwinula aliungamkono rai
iliyotolewa na Naibu Waziri kwa kuitaka jamii kubadili mitazamo
inayogandamiza haki na usawa kwa wenye ulemavu ili kuwa na jamii
jumuishi.
“Watu wenye ulemavu wamekuwa
wakikumbana na changamoto kwenye masuala ya mahusiano ambapo jamii
imekuwa kikwazo kwa kutowapa ushirikiano, hivyo jamii yetu ikiwa yenye
mazingira jumuishi itasaidia kupunguza au kukomesha kabisa changamoto
hizi,” Alisema Mwinula.
No comments :
Post a Comment