Wednesday, May 2, 2018

SHIRIKA LA BIMA LA TAIFA(NIC) LASHIRIKI MAADHIMISHO YA MEI MOSI KWA KUPIGA JEKI ELIMU IRINGA MJINI


IMG-20180502-WA0053
Meneja wa tawi la NIC Iringa Bw. Francis Mlelwa, akimwakilisha Mkurugenzi Mtendaji wa SHIRIKA LA BIMA LA TAIFA(NIC) Bw. Sam Kamanga kukabidhi hundi ya TZS 2, 500, 000/= kwa  Bw. Augustino Mathias Nyenza, ambaye ni Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa, ikiwa ni mchango wa kuendeleza juhudi zilizoanzishwa na Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mh. Richard A. Kasesera kwa ushirikiano na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa katika kutatua changamoto hii ya upungufu wa vyumba vya madarasa katika halmashauri hiyo.
Kulia kwa Bw. Francis Mlewa ni Bi. Mwanaidi Shemweta, ambaye ni Mkuu wa Kitengo cha Mahusiano NIC na kushoto kwa Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya manispaa ya Iringa ni Bw. Majaliwa Hamis Kassim, ambaye ni Afisa Biashara wa Halmashauri ya manispaa ya Iringa, wakishuhudia makabidhiano hayo.
Kabla ya Shirika hilo kukabidhi hundi hiyo lilishiriki kikamilifu katika maadhimisho ya siku ya wafanyakazi duniani Mei Mosi ambayo kitaifa yalifanyika kwenye uwanja wa Samora mkoani Iringa yakiongozwa na Rais Dk. John Pombe Magufuli ka picha zinavyoonyesha matukio mbalimbali.
1
Rais wa Jahuri ya Muungano ya Tanzania Dk. John Pombe Magufuli akiwapungia mkono wafanyakazi wakati alipokuwa akipokea maandamano kwenye maadhimisho ya Mei Mosi katika uwanja wa Samora mjini Iringa kutoka kulia ni Waziri Mkuu Kassim Majaliwa  Rais wa TUCTA Bw. Tumaini Nyamuhokya na kutoka kushoto ni Mh. Job Ndugai Spika wa Bunge na Waziri Jenista Mhagama Waziri wa nchi  Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu.
2
Baadhi ya wafanyakazi wa Shirika la Bima la Taifa NIC wakishiriki katika maandamano ya wafanyakazi siku ya Maadhimisho ya Mei Mosi mjini Iringa.
3
Baadhi ya wafanyakazi na wananchi waliohudhuria kwenye maadhimisho hayo wakiwa kwenye uwanja wa Samora mjini Iringa.
4
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Bima la Taifa NIC Bw. Sam Kamanga akiwa pamoja na baadhi ya waalikwa katika maadhimisho hayo.
5
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Bima la Taifa NIC Bw. Sam Kamanga akishiriki pamoja na baadhi ya waalikwa kuwakumbuka baadhi ya waliokuwa wafanyakazi waliotangulia mbele ya haki katika maadhimisho hayo.

No comments :

Post a Comment