Meneja wa tawi la NIC Iringa Bw. Francis Mlelwa,
akimwakilisha Mkurugenzi Mtendaji wa SHIRIKA LA BIMA LA TAIFA(NIC) Bw.
Sam Kamanga kukabidhi hundi ya TZS 2, 500, 000/= kwa Bw. Augustino
Mathias Nyenza, ambaye ni Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya
Iringa, ikiwa ni mchango wa kuendeleza juhudi zilizoanzishwa na Mkuu wa
Wilaya ya Iringa Mh. Richard A. Kasesera kwa ushirikiano na Mkurugenzi
wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa katika kutatua changamoto hii ya
upungufu wa vyumba vya madarasa katika halmashauri hiyo.
Kulia kwa Bw. Francis Mlewa ni Bi. Mwanaidi
Shemweta, ambaye ni Mkuu wa Kitengo cha Mahusiano NIC na kushoto kwa
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya manispaa ya Iringa ni Bw. Majaliwa
Hamis Kassim, ambaye ni Afisa Biashara wa Halmashauri ya manispaa ya
Iringa, wakishuhudia makabidhiano hayo.
Kabla ya Shirika
hilo kukabidhi hundi hiyo lilishiriki kikamilifu katika maadhimisho ya
siku ya wafanyakazi duniani Mei Mosi ambayo kitaifa yalifanyika kwenye
uwanja wa Samora mkoani Iringa yakiongozwa na Rais Dk. John Pombe
Magufuli ka picha zinavyoonyesha matukio mbalimbali.
Rais wa Jahuri ya Muungano ya
Tanzania Dk. John Pombe Magufuli akiwapungia mkono wafanyakazi wakati
alipokuwa akipokea maandamano kwenye maadhimisho ya Mei Mosi katika
uwanja wa Samora mjini Iringa kutoka kulia ni Waziri Mkuu Kassim
Majaliwa Rais wa TUCTA Bw. Tumaini Nyamuhokya na kutoka kushoto ni Mh.
Job Ndugai Spika wa Bunge na Waziri Jenista Mhagama Waziri wa nchi Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu.
Baadhi ya wafanyakazi wa Shirika
la Bima la Taifa NIC wakishiriki katika maandamano ya wafanyakazi siku
ya Maadhimisho ya Mei Mosi mjini Iringa.
Baadhi ya wafanyakazi na wananchi waliohudhuria kwenye maadhimisho hayo wakiwa kwenye uwanja wa Samora mjini Iringa.
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Bima la Taifa NIC Bw. Sam Kamanga akiwa pamoja na baadhi ya waalikwa katika maadhimisho hayo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la
Bima la Taifa NIC Bw. Sam Kamanga akishiriki pamoja na baadhi ya
waalikwa kuwakumbuka baadhi ya waliokuwa wafanyakazi waliotangulia mbele
ya haki katika maadhimisho hayo.
No comments:
Post a Comment