Waziri wa Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu akifafanua jambo kwa wadau
wa mkutano wa wawekezaji wenye nia ya kuanzisha viwanda vya dawa na
vifaa tiba nchini (hawapo pichani) wakati wa mkutano wa wadau hao mapema
hii leo jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu akifafanua jambo kwa wadau
wa mkutano wa wawekezaji wenye nia ya kuanzisha viwanda vya dawa na
vifaa tiba nchini wakati wa mkutano wa wadau hao mapema hii leo jijini
Dar es Salaam.
Waziri wa Viwanda, Biashara na
Uwekezaji, Charles Mwijage akisisitiza jambo kwa kwa wadau wa mkutano wa
wawekezaji wenye nia ya kuanzisha viwanda vya dawa na vifaa tiba nchini
(hawapo pichani) wakati wa mkutano wa wadau hao mapema hii leo jijini
Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa Bohari Kuu ya
Dawa (MSD), Laurean Bwanakunu akitoa taarifa ya hali ya soko la dawa
nchini kwa wadau wa mkutano wa wawekezaji wenye nia ya kuanzisha viwanda
vya dawa na vifaa tiba nchini (hawapo pichani) wakati wa mkutano wa
wadau hao mapema hii leo jijini Dar es Salaam.
Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo cha
Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS), Prof Appolinary Kamuhabwa
akisisitiza jambo kwa wadau wa mkutano wa wawekezaji wenye nia ya
kuanzisha viwanda vya dawa na vifaa tiba nchini (hawapo pichani) wakati
wa mkutano wa wadau hao mapema hii leo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa Kituo cha
Uwekezaji nchini (TIC), Geofrey Mwambe akielezea vivutio vya uwekezaji
katika viwanda vya dawa nchini kwa wadau wa mkutano wa wawekezaji wenye
nia ya kuanzisha viwanda vya dawa na vifaa tiba nchini, mapema hii leo
jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wadau wa mkutano wa
wawekezaji wenye nia ya kuanzisha viwanda vya dawa na vifaa tiba nchini
wakimsikiliza Mgeni rasmi Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,
Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu (hayupo pichani) wakati wa mkutano wa
wadau hao mapema hii leo jijini Dar es Salaam.
Picha Na Idara Ya Habari – MAELEZO
…………………………………………………………………………
Na Fatma Salum-MAELEZO
Serikali imekutana na wadau
mbalimbali kutoka sekta ya umma na binafsi wenye nia ya
kuanzisha
viwanda vya dawa na vifaa tiba hapa nchini kwa lengo la kujadili namna
ya kufanikisha mchakato huo.
Mkutano huo uliofanyika leo
jijini Dar es Salaam uliandaliwa na Serikali kupitia Wizara ya Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto pamoja na Wizara ya Viwanda,
Biashara na Uwekezaji kufuatia agizo la Rais John Pombe Magufuli la
kutaka hatua za haraka zichukuliwe ili kupata wawekezaji watakaojenga
viwanda hivyo.
Akizungumza na wafanyabiashara
pamoja na wadau waliohudhuria mkutano huo, Waziri wa Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mheshimiwa Ummy Mwalimu alisema kuwa
Serikali imeharakisha mchakato wa kuanzisha viwanda vya dawa kutokana na
changamoto zilizopo kwenye ununuzi wa dawa nje ya nchi.
“Serikali kupitia Bohari Kuu ya
Dawa (MSD) inakumbana na changamoto kadhaa katika uagizaji wa dawa nje
ya nchi ikiwemo kuletewa dawa baada ya muda mrefu tangu kuagiza,
kupungua kwa thamani ya fedha zetu kwa kubadilisha na dola za kimarekani
pamoja na kuagiza dawa nyingi kwa mkupuo ambazo hatimaye huharibika
kutokana na kukaa muda mrefu,” alisema Ummy.
Pia Waziri Ummy alibainisha kuwa
ni muhimu kuanzisha viwanda vya dawa hapa nchini kwani bado watanzania
wanasumbuliwa na magonjwa mbalimbali yakiwemo ya kuambukiza na yasiyo ya
kuambukiza.
“Mahitaji ya dawa nchini ni
makubwa na mwaka huu wa fedha Serikali imetenga shilingi bilioni 269 kwa
ajili ya kununua dawa na vifaa tiba hivyo ni muhimu kujenga viwanda ili
fedha za Tanzania ziendelee kuzunguka hapa hapa nchini,” alisema Ummy.
Katika mkutano huo wawekezaji 38
wenye nia ya kujenga viwanda hivyo walijitokeza na Waziri Ummy
aliwahakikishia kuwa Serikali itanunua dawa za ndani lakini lazima ziwe
na ubora na pia viwanda vishirikiane na Chuo cha Sayansi ya Tiba
Muhimbili (MUHAS) ili kuhakikisha ubora wa dawa hizo.
Kwa upande wake Waziri wa Viwanda
,Biashara na Uwekezaji Charles Mwijage aliipongeza sekta binafsi nchini
kwa kushirikiana vizuri na Serikali na kukubali kuhudhuria mkutano huo
ili kufanikisha azma ya ujenzi wa viwanda vya dawa na vifaa tiba.
“Hili tunalolifanya leo lipo
kwenye Mpango wa Pili wa Taifa wa Maendeleo wa Miaka Mitano ila
tunaharakisha mchakato huu ili ifikapo mwaka 2025 zaidi ya asilimia 50
ya dawa tunazotumia ziwe zinazalishwa hapa nchini,” alisisitiza Mwijage.
Aidha alisema kuwa lengo la
Serikali ni kutengeneza sekta binafsi imara na kuwataka wadau katika
sekta hiyo wajiandae kujenga viwanda vya dawa na Serikali na Taasisi
zake zipo tayari kuwasaidia kufanikisha zoezi hilo.
Mkutano huo wa Serikali na
wawekezaji wenye nia ya kujenga viwanda vya dawa ulihudhuriwa na wadau
mbalimbali wakiwemo wafanyabiashara wakubwa hapa nchini na Taasisi za
Serikali zinazohusika na sekta ya afya zikiwemo Bohari Kuu ya Dawa
(MSD), Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA), Chuo Kikuu cha Sayansi ya Tiba
(MUHAS), Kituo cha Uwekezaji (TIC) na Shirika la Taifa la Maendeleo
(NDC).
No comments :
Post a Comment