Saturday, March 3, 2018

Wasanii wa Filamu Nchini Waaswa Kuzingatia Maadili


P0
Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania (KBF), Joyce Fissoo akionyesha Leseni inayotolewa na bodi hiyo kwa ajili ya waendeshaji wa vibanda vya kuonyeshea filamu wakati wa kikao kazi cha wadau wa tasnia ya Filamu na Maafisa Utamaduni wa Mkoa wa Arusha kilichofanyika jana Jijini Arusha. Kutoka kushoto ni Afisa Utamaduni wa Mkoa wa Arusha Bi. Irene Ngao na Afisa Utamaduni wa Halmashauri ya Wilaya ya Arusha Gasper Tesha.
P1
Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania (KBF), Joyce Fissoo akiwasilisha mada  wakati wa kikao kazi cha wadau wa tasnia ya Filamu na Maafisa Utamaduni wa Mkoa wa Arusha kilichofanyika jana Jijini Arusha.
P2
Afisa Utamaduni wa Mkoa wa Arusha akisisitiza jambo wakati wa kikao kazi cha wadau wa tasnia ya Filamu na Maafisa Utamaduni wa Mkoa wa Arusha kilichofanyika jana Jijini Arusha. Katikati ni Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania (KBF), Joyce Fissoo na kulia ni Afisa Utamduni wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru.
P3
Katibu wa Umoja wa Wasanii wa Filamu na Michezo ya Kuigiza Mkoa wa Arusha (TDFA), Said Mohamed Gogola akichangia mada wakati wa kikao kazi cha wadau wa tasnia ya Filamu na Maafisa Utamaduni wa Mkoa wa Arusha kilichofanyika jana Jijini Arusha.
P4
Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania (KBF), Joyce Fissoo (kulia) akiagana na Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha, Hargeney Chitukuro mara baada ya kumaliza kikao kazi cha wadau wa tasnia ya Filamu na Maafisa Utamaduni wa Mkoa wa Arusha kilichofanyika jana Jijini Arusha.
P5
Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania (KBF), Joyce Fissoo (waliokaa kwenye viti katikati) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya washiriki wa kikao kazi cha wadau wa tasnia ya Filamu na Maafisa Utamaduni wa Mkoa wa Arusha kilichofanyika jana Jijini Arusha.
Na: Mpiga Picha Wetu
……………..
Rai hiyo imetolea na Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania (KBF) Joyce Fissoo alipokuwa akiwasilisha mada katika kikao kazi cha maafisa Utamaduni na wadau wa tasnia ya filamu wa mkoa wa Arusha iliyofanyika jana Jijini Arusha.
Mama Fissoo alisema kuwa nidhamu imekuwa kikwazo kikubwa kwa wasanii jambo
linalowafanya wasiaminike miongoni mwa jamii ikiwa ni pamoja na taasisi za kifedha ambazo zingeweza kuwawezesha.
” Mnapaswa kuwa na nidhamu ya hali ya juu, wasanii wengi hasa wa tasnia ya filamu mmeshindwa kuaminiwa kutokana na nidhamu inayotiliwa mashaka” alisisitiza Mama Fissoo.
Kwa upande wake Katibu  Umoja wa Wasanii wa Filamu Mkoa wa Arusha Said Mohamed Gogola ameishukuru Serikali kupitia Bodi ya Filamu kwa kuona umuhimu wa kukutana na wadau wa tasnia hiyo ili kuwajengea uelewa juu ya mambo mbalimbali yanayohusiana na maendeleo ya  tasnia hiyo.
Amesema kuwa kikao kazi hicho kimewapa chachu ya kupiga hatua mbele zaidi katika kuhakikisha tasnia ya filamu mkoani Arusha inasonga mbele kwa kasi zaidi.
Naye Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha Hargeney Chitukuro ameishukuru Bodi ya Filamu kwa kuupa mkoa wao fursa ya kukutanisha wadau wa tasnia hiyo na kuongeza kuwa wao kama Serikali ya Mkoa wako tayari kutoa ushirikiano ili kuhakikisha vijana wa mkoa wa Arusha wanapata ajira ya uhakika kupitia filamu.

No comments :

Post a Comment