Na Mwandishi Wetu
WATETEZI
wa Rasilimali Wasio na Mipaka(Warami)limesema limesikitishwa na kitendo
cha Kamati kuu ya Chadema kuingilia uhuru wa Mahakama baada ya jana
kuitisha mkutano kuzungumzia mambo yalipo mahakamani.
Warami
wameongeza kuwa si tu kuingilia uhuru wa mahakama pia chama hicho
kimekwenda mbali zaidi kwa kutoa masharti yanayoashiria uvunjifu wa
amani iwapo Mwenyekiti wa Freeman Mbowe na viongozi wengine watanyimwa
dhamana leo.
Akizungumza
leo jijini Dar es Salaam Mkurugunzi wa Utafiti wa Warami Philipo
Mwakibinga amesema jana baadhi ya viongozi wa Chadema kupitia mkutano
wao wameonesha dhahiri kuingilia uhuru wa Mahakama kwa kuanza
kushinikisha maamuzi ya Mahakama.
“Mbunge
wa Arusha Mjini Godbles Lema, Profesa Abdallah Safari na wenzao wakiwa
wanajua kuwa Mahakama ni chombo cha haki walitengeneza mazingira ya
kuonesha kuwa viongozi hawatetendewi haki kama hawatapa dhamana leo.
“Wanafanya
hivyo wakijua wazi jambo hili limelenga kuishawishi , kushinikiza na
kuilazimisha mahakama ifanye watakavyo wao kwa kuacha misingi ya haki
wajibu na maadili ya kimahakama,”amesema Mwakibinga.
Amefafanua
Watanzania ni mashahidi Mbowe na wenzake ambao wapo Mahakamani
wamekamatwa kama matokeo ya matendo yao ya kushawishi na kuchochea chuki
miongoni watanzania jambo ambalo si la kiutamaduni kwa Taifa.
“Warami
tunapenda kuwakumbusha Watanzania kuwa sheria ni kama kaa la moto na
unapovunja sharia lazima ujue umeamua kushika kaa la moto kwa hivyo
lazima ujiandae kuungua.
“Tunawakumbusha
Chadema ,hasa wakina Lema na wenzao watii sheria , waache maneno ya
kichochezi yasiyo ya kiuongozi na wasiendelee kuropoka ropoka, zama za
kuwachekea waropokaji zimepitwa na wakati,”amesema.
Mwakibinga amesema Lema kukamatwa kwa viongozi wa chama chake ni mkakati uliopangwa na Serikali kwa ajili ya kuwakomoa.
Amesema
Warami wanawapa changamoto Chadema , wamuulize Waziri Mkuu mstaafu
Frederick Sumaye ajitokeze hadharani wakati Augustino Mrema akiwa
NCCR-Mageuzi na baadae TLP alivyokuwa anakamatwa na vyombo vya dola je
alikuwa analazimisha vyombo vya dola vimkamate wakati Mrema hakuwa na
makosa kwa wakati ule.
“Chadema
waache kuharibu sifa ya vyombo vyetu vya kiusalama hasa idara nyeti ya
Usalama wa Taifa kwa kuwasingizia mambo ya ajabu ajabu kwa ajili ya
kuficha udhaifu wao wa kuimarisha chama,”amesema Mwakibinga.
Ameongeza Warami inawataka Chadema kuacha kukimbia kivuli chao na waswahili wanasema ‘ukilikoroga lazima ulinywe’ .
“Hivyo
Chadema walinywe kwa kadiri ya walivyorikoroga.Pia iache Mahakama
itafisiri sheria na kwa kuwa wameweka wanasheria wanaowaamini,
wawahimize wanasheria wao kuhakikisha wanashinda kesi
zinazowakabili,”amesisitiza.
KUHUSU MAASKOFU KUTUMIKA
Mwakibinga amesema mara ya mwisho walihoji iwapo maaskofu wanatumika na vyama vya siasa hasa Chadema.
“Nafikiri
wote sasa tumejiridhisha kuwa maaskofu wetu wameamua kutumika kulipa
fadhila za waliokuwa wanawapa fedha katika zama za kufanya harambee ya
fedha kuelekea uchaguzi mkuu mwaka 2015.
“Matukio
ya Chadema kuunga mkono hadharani waraka wa maaskofu ,ACT Wazalendo
kunifukuza uanachama kwa mimi kuwakosoa maaskofu na Maalim Seif
kutangaza hadharani anaunga mkono madudu yale ya maaskofu,”amesema.
Ameongeza
hivyo ni vishiaria na kuthibitisha wazi maaskofu wameamua kutumika na
kuyaacha maelekezo na mafunzo ya dini yanayotaka kilicho cha kaisari
apewe kaisari na kilicho cha Mungu apewe Mungu.
Ametumia
nafasi hiyo kuwaasa wanasiasa, wanaharakati , wanahabari , viongozi wa
dini , taasisi binafsi waanzishe utaratibu wa kuheshimu uhuru wa
Mahakama na kutoa kauli za mashinikizo.
Mkurugenzi wa Utafiti kutoka
Watetezi wa Rasilimali wasio na Mipaka (WARAMI),Philipo Mwakibinga ,
akizungumza na Waandishi wa habari kuhusu mkutano wa Kamati Kuu ya
Chadema uliofanyika jana ukiwa na lengo la kuingia uhuru wa Mahakama.
Mkurugenzi wa Utafiti kutoka
Watetezi wa Rasilimali wasio na Mipaka (WARAMI),Philipo Mwakibinga,
akiwaeleza jambo waandishi wa habari yaliyojiri katika mkutano mkuu wa
Chadema.
No comments :
Post a Comment