Mkurugenzi Msaidizi kutoka Wizara
ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto anayesimamia Vyuo
vya Maendeleo ya Jamii Bi. Neema Ndoboka akieleza mpango wa Wizara
katika kusimamia Sekta ya Maendeleo ya Jamii kupitia Vyuo vya Maendeleo
ya Jamii wakati akifungua Kikao cha wadau wa Sekta ya Maendeleo ya Jamii
kujadili Rasimu ya Mitaala ya fani ya Maendeleo ya Jamii kilichofanyika
Mjini Morogoro Kushoto ni Mkuu wa Taasisi ya Maendeleo ya Jamii Tengeru
Dkt. Bakari George.
Kaimu Mkuu wa Taasisi ya Maendeleo
ya Jamii Tengeru Dkt. Bakari George akieleza dhumuni la kikao cha
kupitia Rasimu ya Mitaala ya Fani ya Maendeleo ya Jamii kupitia Vyuo
vya Maendeleo ya Jamii wakati wa Kikao hicho cha wadau wa Sekta ya
Maendeleo ya Jamii kujadili Rasimu ya Mitaala ya fani ya Maendeleo ya
Jamii kilichofanyika Mjini Morogoro.
Afisa Maendeleo ya Jamii Bw. Abel
Palala akiwasilisha mada kuhusu Mtaala wa mafunzo ya Maendeleo ya Jamii
ngazi ya Stashahada katika kikao cha kupitia Rasimu ya Mitaala ya Fani
ya Maendeleo ya Jamii katika Vyuo vya Maendeleo ya Jamii wakati wa
Kikao hicho cha wadau wa Sekta ya Maendeleo ya Jamii waliokutana
kujadili Mitaala pendekezi ya fani ya Maendeleo ya Jamii katika ukumbi
wa TAFOLI Mjini Morogoro.
Mhadhiri wa Taasisi ya Maendeleo
ya Jamii Tengeru Bw. Simon Kilasala akitoa taarifa ya utafiti wa Soko
la ajira kwa wataalam wa Maendeleo ya Jamiki wakati wa kikao cha
kupitia Rasimu ya Mitaala ya Fani ya Maendeleo ya Jamii kupitia Vyuo
vya Maendeleo ya Jamii wakati wa Kikao hicho cha wadau wa Sekta ya
Maendeleo ya Jamii wanaokutana kujadili Rasimu ya Mitaala ya fani ya
Maendeleo ya Jamii katika ukumbi wa TAFOLI Mjini Morogoro.
Mkufunzi Chuo cha Maendeleo ya
Jamii Rungemba Bw. Kidubya Kulamiwa akiwasilisha mada kuhusu Mtaala wa
mafunzo ya Maendeleo ya Jamii ngazi ya Astashahada katika kikao cha
kupitia Rasimu ya Mitaala ya Fani ya Maendeleo ya Jamii katika Vyuo vya
Maendeleo ya Jamii wakati wa Kikao hicho cha siku moja cha wadau wa
Sekta ya Maendeleo ya Jamii waliokutana kujadili Rasimu ya Mitaala ya
fani ya Maendeleo ya Jamii kilichofanyika Mjini Morogoro.
Mkufunzi Chuo cha Maendeleo ya
Jamii Buhare mkoani Mara Bw. Anicet Rwezaula akiwasilisha mada kuhusu
Mtaala wa mafunzo ya Maendeleo ya Jamii ngazi ya Cheti cha Msingi
katika kikao cha kupitia Rasimu ya Mitaala ya Fani ya Maendeleo ya
Jamii katika Vyuo vya Maendeleo ya Jamii wakati wa Kikao hicho cha
wadau wa Sekta ya Maendeleo ya Jamii waliokutana kujadili Rasimu ya
Mitaala ya fani ya Maendeleo ya Jamii kilichofanyika Mjini Morogoro.
Baadhi ya wadau na wataalamu wa
Maendeleo ya Jamii wakijadiliana katika makundi ili kutoa maoni na
kuboresha Rasimu ya Mitaala ya Vyuo vya Maendeleo ya Jamii wakati wa
Kikao kilicho wakutanisha Mjini Morogoro hivi karibuni.
Picha na Kitengo cha Mawasiliano WAMJW
……………..
Na Mwandishi Wetu Morogoro
Serikali kupitia Wizara ya Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (Idara Kuu ya Maendeleo ya
Jamii) imeahidi kuimarisha taaluma ya Maendeleo ya Jamii ili iweze
kuongeza tija katika jamii.
Hayo yamesemwa mjini Morogoro na
Mkurugenzi Msaidizi anayesimamia Vyuo vya Maendeleo ya Jamii Bi. Neema
Ndoboka wakati wa kikao cha wadau waliokutana kujadili rasimu ya mitaala
na kupata maoni yatakayowezesha kuboresha mitaala ya vyuo hivyo.
Bi. Neema amesema kuwa Wizara
itafuatilia kwa karibu utoaji mafunzo ya fani ya Maendeleo ya Jamii kwa
vyuo vyake inavyovisimamia na pia kushirikiana na Mamlaka nyingine
katika kufuatilia utoaji wa mafunzo hayo kwa Vyuo visivyosimamiwa na
Wizara.
“Kikao cha wadau cha kupitia
mitaala ya vyuo vya maendeleo ya jamii kinajenga uwezo wa Wizara katika
kuhakikisha usimamizi wa vyuo hivi unazingatia Kanuni na taratibu za
Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) jukumu ambalo Wizara imekuwa
ikilitekeleza kila inapohitajika” alisisitiza Bi Neema.
Akizungumza katika mkutano huo
Kaimu Mkuu wa Tasisi ya Maendeleo ya Jamii Tengeru Dkt. Bakari George
suala la kuwa na mkutano wa wadau kupitia rasimu ya mitaala ya vyuo vya
Maendeleo ya Jamii ni hitaji la muhimu ili kupta maoni ya takayosaidia
kkuboresha mada, mahudhui, mbinu, stadi za kufundishia na kujifunzia na
maarifa.
Dkt. Bakari aliongeza kuwa awali
Wizara iliandaa utafiti wa mahitaji, kubaini majukumu na wajibu wa
wataalam wa maendeleo ya jamii, na hatimaye kuweza kuandaa rasimu ya
awali ya mitaala ya Vyuo vya Maendeleo ya Jamii kwa lengo la kuimarisha
umahiri wa Vyuo vya Maendeleo ya jamii, weledi wa wataalam wa maaendeleo
ya jamii na kutoa mchango katika kufikia maendeleo jumuishi.
“Wizara inaandaa mitaala ya vyuo
vya maendeleo ya jamii ili kujenga umahiri wa vyuo na kuchangia ujenzi
wa Tanzania ya viwanda na uchumi wa kati” alisema Dkt. Bakari.
Naye Mhadhiri wa Taasisi ya
Maendeleo ya Jamii Tengeru Bw. Simon Kilasala amesema kuwa utafiti
uliofanyika kuhusu mitaala ya vyuo vya maendeleo ya jamii umebainisha
kuwa wahitimu wengi kutoka katika vyuo hivyo bado wanahitaji stadi zaidi
katika kuongeza mbinu na umahiri ziada wa kuweza kujiajiri na
kutengeneza ajira mpya.
“ Utafiti huu utasaidiakuboresha
Mitaala ya Vyuo vya Maendeleo ya Jamii kutokana na mahitaji ya soko la
ajira kwa wataalm wa Maendeleo ya Jamii nchini na nje ya nchi”
alisisitiza Bw. Kilasala
No comments :
Post a Comment