Tuesday, March 27, 2018

UFAFANUZI KUHUSU MAGARI ZAIDI YA 100 YANAYOSAFIRISHA MAKAA YA MAWE YA NJE CHI KUKWAMA DODOMA


lorry-drivers-787197
Jana tarehe 26 Machi, 2018, katika Taarifa ya Habari ya saa 2 usiku, miongoni mwa habari zilizotolewa kupitia Televisheni ya STAR TV ilieleza kuwa, zaidi ya magari 100 yanayosafirisha makaa ya mawe kutoka mgodi wa TANCOAL NGAKA Wilayani Mbinga kwenda Nchi za Kenya, Rwanda na Uganda yamekwama Mkoani Dodoma kwa zaidi ya wiki mbili yakingoja vibali vya kusafirisha madini hayo nje ya nchi kutoka kwa Kamishna wa Madini. Taarifa hiyo ilitolewa na Kaimu Meneja wa mgodi wa Tan Coal Bw. Edward Mwanga wakati akizungumza
na waandishi wa habari mjini Songea.
Wizara inapenda kufafanua kuwa, katika kipindi cha wiki mbili zilizopita Wizara imepokea jumla ya maombi ya vibali 69 hadi tarehe 26 Machi, 2018 ya Kampuni hiyo kwenda nchi za Nje kwa mchanganuo ufuatao;
No TAREHE/KUPOKEA VIBALI JUMLA YA MAOMBI TAREHE/KUSAINIWA VIBALI
1. 12 Machi, 2018 07 13 Machi, 2018
2 14 Machi, 2018 12 16 Machi, 2018
3 16 Machi, 2018 06 19 Machi, 2018
4 19 Machi, 2018 13 20 Machi, 2018
5 20 Machi, 2018 01 20 Machi, 2018
6 21 Machi, 2018 03 22 Machi, 2018
7 23 Machi, 2018 10 23 Machi, 2018
8 26 Machi, 2018 17 27 Machi, 2018
JUMLA 69
Aidha, baada ya mapitio ya vibali vilivyotolewa kwa Kampuni ya TanCoal katika kipindi cha wiki mbili zilizopita Wizara imejiridhisha kuwa hakuna kibali kilichochukua zaidi ya siku 2 kutolewa.
Kwa mujibu wa Marekebisho ya Sheria ya Madini ya Mwaka 2010, vibali vya kusafirisha madini kwenda nchi za nje vinatolewa na Tume ya Madini kupitia kwa Mtendaji Mkuu wa Tume ya Madini. Aidha, hivi sasa kuna Kaimu Mtendaji Mkuu wa Tume ya Madini ambaye anahusika kutoa vibali hivyo.
Hata Hivyo, Wizara inaendelea kuchukua hatua za kuboresha utaratibu wa utoaji wa vibali ili vitolewe ndani ya muda mfupi zaidi.

No comments :

Post a Comment