Jana tarehe 26 Machi, 2018, katika
Taarifa ya Habari ya saa 2 usiku, miongoni mwa habari zilizotolewa
kupitia Televisheni ya STAR TV ilieleza kuwa, zaidi ya magari 100
yanayosafirisha makaa ya mawe kutoka mgodi wa TANCOAL NGAKA Wilayani
Mbinga kwenda Nchi za Kenya, Rwanda na Uganda yamekwama Mkoani Dodoma
kwa zaidi ya wiki mbili yakingoja vibali vya kusafirisha madini hayo nje
ya nchi kutoka kwa Kamishna wa Madini. Taarifa hiyo ilitolewa na Kaimu
Meneja wa mgodi wa Tan Coal Bw. Edward Mwanga wakati akizungumza
na
waandishi wa habari mjini Songea.
Wizara inapenda kufafanua kuwa,
katika kipindi cha wiki mbili zilizopita Wizara imepokea jumla ya maombi
ya vibali 69 hadi tarehe 26 Machi, 2018 ya Kampuni hiyo kwenda nchi za
Nje kwa mchanganuo ufuatao;
| No | TAREHE/KUPOKEA VIBALI | JUMLA YA MAOMBI | TAREHE/KUSAINIWA VIBALI |
| 1. | 12 Machi, 2018 | 07 | 13 Machi, 2018 |
| 2 | 14 Machi, 2018 | 12 | 16 Machi, 2018 |
| 3 | 16 Machi, 2018 | 06 | 19 Machi, 2018 |
| 4 | 19 Machi, 2018 | 13 | 20 Machi, 2018 |
| 5 | 20 Machi, 2018 | 01 | 20 Machi, 2018 |
| 6 | 21 Machi, 2018 | 03 | 22 Machi, 2018 |
| 7 | 23 Machi, 2018 | 10 | 23 Machi, 2018 |
| 8 | 26 Machi, 2018 | 17 | 27 Machi, 2018 |
| JUMLA | 69 | ||
Aidha, baada ya mapitio ya vibali
vilivyotolewa kwa Kampuni ya TanCoal katika kipindi cha wiki mbili
zilizopita Wizara imejiridhisha kuwa hakuna kibali kilichochukua zaidi
ya siku 2 kutolewa.
Kwa mujibu wa Marekebisho ya
Sheria ya Madini ya Mwaka 2010, vibali vya kusafirisha madini kwenda
nchi za nje vinatolewa na Tume ya Madini kupitia kwa Mtendaji Mkuu wa
Tume ya Madini. Aidha, hivi sasa kuna Kaimu Mtendaji Mkuu wa Tume ya
Madini ambaye anahusika kutoa vibali hivyo.
Hata Hivyo, Wizara inaendelea kuchukua hatua za kuboresha utaratibu wa utoaji wa vibali ili vitolewe ndani ya muda mfupi zaidi.
No comments:
Post a Comment