Mwanzilishi Mwenza wa Young Scientists Tanzania (YST) Dk. Gosbert Kamugisha (kulia), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari kuhusu maonyesho ya Young Scientists Tanzania (YST) 2018 yatakayofanyika mwezi Agosti mwaka huu Ukumbi wa Julius Nyerere International Convention Centre (JNICC) jijini Dar se Salaam. Wengine kutoka kushoto ni Patricia Mhondo kutoka Kampuni ya Shell Explorstion snd Production Tanzania Ltd (shell) na Joseph Clawry kutoka nchi ya Iland.
Meza Kuu pamoja na wadhamini wa maonyesho hayo.
Mkurugenzi wa Karimjee Jinanjee Foundation (KJF), Yusuf Karimjee akizungumzia udhamini wao
Patricia Mhondo kutoka Kampuni ya Shell Explorstion snd Production Tanzania Ltd (shell) akizungumza kwenye mkutano huo.Joseph Clawry kutoka nchi ya Iland akizungumzia kazi za ubunifu na jinsi nchi yao inavyowawezesha wanafunzi waliofanya vizuri katika miradi yao.
Muonekano wa chumba cha mkutano huo.
Na Dotto Mwaibale
Na Dotto Mwaibale
MAONYESHO
ya Young Scientists Tanzania (YST) 2018 yatafanyika mwezi Agosti mwaka
huu Ukumbi wa Julius Nyerere International Convention Centre (JNICC)
jijini Dar se Salaam.
Akizungumza
na waandishi wa habari Dar es Salaam jana Mwanzilishi Mwenza wa YST,
Dk. Gosbert Kamugisha alisema maonesho hayo yatafanyika kuanzia tarehe
moja hadi mbili mwezi huo.
“Wanafunzi
wote wanaopenda kushiriki wanashauriwa kutuma kazi za miradi yao kwenda
YST kabla ya tarehe 21 Aprili 2018” alisema Kamugisha.
Kamugisha
alisema wanafunzi 200 watakaochaguliwa wataonyesha kazi za teknolojia
na ugunduzi wa kisayansi kwenye onesho hilo la mwaka huu na kuwa na
wanafunzi watakaochaguliwa watapewa mafunzo kutoka kwa washauri wa
sayansi wa YST kuhusu namna ya kutengeneza kazi zao za kisayansi.
Alisema
onesho hilo pamoja na mpango wa kuzitembelea shule na wanafunzi
kuwapatia ushauri wa kisayansi vinawezeshwa na wadhamini wakuu wa YST
ambao ni Shell Explorstion snd Production Tanzania Ltd (shell) na
Karimjee Jinanjee Foundation (KJF)
“Tunapenda
kuwashukuru wadhamini wetu tangu mwaka 2012. Mwaka huu wa 2018 KJF
wameongeza kiwango cha udhamini na kuwa mmoja wapo wa wadhamini wakuu wa
YST kwa kipindi cha miaka mitano ijayo.
Alisema
udhamini huo utaiwezesha programu ya YST kuwa endelevu na kuwawezesha
vijana kufanya ubunifu na kufanya tafiti za kisayansi ili kuleta
maendeleo ya kijamii na kiuchumi.
Kamugusha
aliongeza kuwa wanasayansi chipukizi wakaoshiriki onesho la YST mwaka
huu kwa sasa wanaendelea kutengeneza kazi za miradi yao katika nyanja
mbalimbali za kisayansi kama kemia, fizikia na hesabu, biolojia na
ekolojia, saynsi ya jamii na teknolojia na kuwa kazi miradi nyingi
zimejikita katika sekta ya afya,kilimo na usalama wa chakula,
mawasiliano na usafirishaji, nishati,elimu, mazingira na mabadiliko ya
tabia nchi.
Alisema
wanafunzi watakajituma na kufanya ugunduzi mzuri watazawadiwa pesa
taslimu, medali, vikombe na uimarishaji wa maktaba ya shule yao kama
ambavyo wamefanya kwa miaka sita iliyopita KJF watawazadia wanafunzi
wenye ugunduzi mzuri zaidi zawadi za udhamini wa masomo ya chuo kikuu
ili kuwawezesha kusoma masomo ya sayansi na teknolojia katika ngazi ya
chuo kikuu.
No comments :
Post a Comment