Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Amina Khamis Shaaban
akitoa hotuba yake katika hafla ya FINCA Microfinance Bank kutimiza
miaka 20 tangu kuanzishwa kwake nchini Tanzania ambapo ameipongeza benki
hiyo kwa jinsi ambavyo imekuwa ikisaidia wajasiriamali wadogowadogo
vijijini na mijini, Benki hiyo imeweza kusaidia wajasiriamali wapatao
Milioni moja tangu ilipoanza kutoa huduma za kifedha.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya
FINCA Microfinance, Tanzania Issa Ngwegwe akizungumzia mafanikio ya
sherehe zake FINCA Microfinance kutimiza miaka 20 ya utendaji wake wa
shughuli za kifedha nchini Tanzania tangu kuanzishwa kwake.
Dk. Bernald Yohana Kibese akizungumza wakati alipokuwa akimkaribisha Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Amina Khamis Shaaban ili kutoa hotuba yake katika hafla hiyo.
Rais na Mkurugenzi Mtendaji wa
FINCA Microfinance Holding Company, Andree Simon akiipongeza FINCA
Microfinance kwa kufanya kazi kwa ufanisi wa hali ya juu.
Mwenyekiti wa Bodi ya FINCA
ambaye pia ni Makam wa Rais na Mkurugenzi wa Kanda ya Afrika Mike
Gama-Lobo akizungumza katika mkutano huo.
Baadhi ya wakurugenzi na mameneja
wa FINCA Microfinance Bank kutoka Mataifa mbalimbali walioalikwa katika
hafla hiyo ya miaka 20 ya benki hiyo.
Baadhi ya wajumbe wa bodi ya FINCA Microfinance wakiwa katika hafla hiyo.
Jimmy Ngoye meneja wa FINCA
mkoani Arusha akionyesha tuzo yake aliyokabidhiwa kwa kuwa mfanyakazi
bora katika taasisi hiyo kwa upande wa mameneja.
Rais na Mkurugenzi Mtendaji wa
FINCA Microfinance Holding Company, Andree Simon akimpongeza Jimmy
Ngoye meneja wa FINCA Microfinance mkoani Arusha baada ya kushinda tuzo
ya ufanyakazi bora kwa kufanya kazi kwa ufanisi wa hali ya juu.
Kikundi cha burudani kikiongozwa na Msanii maarufu Bob Rich kikitumbuiza katika hafla hiyo.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Amina Khamis Shaaban akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa FINCA Duniani pamoja na wa Tanzania.
No comments :
Post a Comment