Pages

Saturday, March 3, 2018

FINCA MICROFINANCE BANK YASHEREHEKEA MIAKA 20 TANGU KUANZISHWA KWAKE


1
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Amina Khamis Shaaban akitoa hotuba yake katika hafla ya FINCA Microfinance Bank kutimiza miaka 20 tangu kuanzishwa kwake nchini Tanzania ambapo ameipongeza benki hiyo kwa jinsi ambavyo imekuwa ikisaidia wajasiriamali wadogowadogo vijijini na mijini, Benki hiyo imeweza kusaidia wajasiriamali wapatao Milioni moja tangu ilipoanza kutoa huduma  za kifedha.
02
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya FINCA Microfinance, Tanzania Issa Ngwegwe akizungumzia mafanikio ya sherehe zake FINCA Microfinance kutimiza miaka 20 ya utendaji wake wa shughuli za kifedha nchini Tanzania tangu kuanzishwa kwake.
2
Dk. Bernald Yohana Kibese akizungumza wakati alipokuwa akimkaribisha Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Amina Khamis Shaaban ili kutoa hotuba yake katika hafla hiyo.
3
Rais na Mkurugenzi Mtendaji wa FINCA Microfinance Holding Company, Andree Simon akiipongeza FINCA Microfinance kwa kufanya kazi kwa ufanisi wa hali ya juu.
4
Mwenyekiti wa Bodi ya FINCA ambaye pia ni Makam wa Rais na Mkurugenzi wa Kanda ya Afrika Mike Gama-Lobo akizungumza katika mkutano huo.
5
Baadhi ya wakurugenzi na mameneja wa FINCA Microfinance Bank kutoka Mataifa mbalimbali walioalikwa katika hafla hiyo ya miaka 20 ya benki hiyo.
6 7 8 9 10 11
Baadhi ya wajumbe wa bodi ya FINCA Microfinance wakiwa katika hafla hiyo.
12
Jimmy Ngoye meneja wa FINCA mkoani Arusha akionyesha tuzo yake aliyokabidhiwa kwa kuwa mfanyakazi bora katika taasisi hiyo kwa upande wa mameneja.
13
Rais na Mkurugenzi Mtendaji wa FINCA Microfinance Holding Company, Andree Simon akimpongeza  Jimmy Ngoye meneja wa FINCA Microfinance mkoani Arusha baada ya kushinda tuzo ya ufanyakazi bora kwa kufanya kazi kwa ufanisi wa hali ya juu.
14
15
Kikundi cha burudani kikiongozwa na Msanii maarufu Bob Rich kikitumbuiza katika hafla hiyo.
16
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Amina Khamis Shaaban akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa FINCA Duniani pamoja na wa Tanzania.

No comments:

Post a Comment