Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiweka na mradi wa uboreshaji wa
Bandari ya Dar es Salaam leo. Kushoto ni Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya
Dunia Bella Bird.
(Picha na: Frank Shija – MAELEZO)
…………………………………………………………….
Na: Lilian Lundo – MAELEZO
Jumla ya shilingi bilioni 922
zitatumika kwa ajili ya kuboresha bandari ya Dar es Salaam ili
kuifanya
kuwa ya kisasa itakayoweza kupokea meli na shehena kubwa za mizigo kwa
wakati mmoja.
Rais Dkt. John Pombe Magufuli
ameyasema hayo leo katika eneo la bandari ya Dar es Salaam alipokuwa
akiweka jiwe la msingi la mradi wa uboreshaji wa bandari hiyo.
“Mradi huu utakapokamilika
utainufaisha Taifa letu na nchi jirani kama vile Malawi, Zambia, Kongo,
Rwanda, Uganda na Burundi ambazo zinategemea bandari yetu kusafirisha
mizigo,” amesema Dkt. Magufuli.
Amesema kuwa, bandari hiyo ni
lango kuu la biashara na ni kitovu cha uchumi wa nchi. Hivyo kama
itaboreshwa ufanisi na uwezo wake itasaidia kukuza uchumi wa nchi
kuelekea uchumi wa kati.
Aidha amesema, uboreshaji wa
bandari hiyo utaondoa ucheleweshaji wa upakuaji na upakiaji wa mizigo
uliokuwa ukisababishwa na ufinyu wa gati lakini baada ya kukamilika kwa
upanuzi huo meli kubwa zaidi zitaweza kutia nanga.
“Mradi huu ukikamnilika utaifanya
badari ya Dar es Saalam kuwa ya mfano na kutakuwa hakuna ucheleweshaji
wa mizigo na itachangia maendeleo kiuchumi sio tu kwa Tanzania bali hata
kwa zile nchi zitakazokuwa zinatumia bandari hii kupitisha mizigo yao”
alieleza Rais Magufuli.
Aidha Rais aliuataka wa TPA
kuimarisha ulinzi katika badari hiyo ili mkuifanya kuwa mahali salama pa
kupitishia mizigo na kuhakikisha mizigo yote inayopita bandarini
taarifa zake zinajulikana.
Kwa upande wake, Waziri wa
Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa amesema kuwa mradi
huo utanufaisha Taifa la Tanzania pamoja na nchi jirani zinazotumia
bandari hiyo.
“Mradi utabadilisha ufanisi wa bandari ya Dar es Salaam na kuifanya kuwa ya kisasa,” amesema Prof. Mbarawa.
Nae Mkurugunzi Mkuu wa Mamlaka ya
Bandari Tanzania Mhandisi Deusdedit Kakoko amesema kuwa uboreshaji wa
bandari hiyo utaweza kuhudumia shehena ya mizigo kutoka tani milioni 14
zinazohudumiwa kwa sasa hadi kufikia tani milioni 28 na pia itaweza
kuhudumia meli kubwa zenye urefu wa hadi mita 320.
Mkurugenzi wa Benki ya Dunia
Nchini Tanzania, Bella Bird amesema Benki hiyo kwa kushirikiana na
Serikali ya Uingereza kupitia Idara yake ya Maendeleo ya Kimataifa
(DFID) itaendelea kusaidia kukua kwa Tanzania na kusaidia kuboresha
maisha Tanzania.
Katika Uboreshaji wa bandari
hiyo, Serikali ya Tanzania inachangia dola milioni 63.4, Benki ya Dunia
Dola milioni l. 345.2 na Serikali ya Uingereza Dola milioni 12.4. Mradi
unategemewa kutekelezwa katika kipindi cha miezi 36 chini ya kampuni ya
China Harbour Engineering.
No comments :
Post a Comment