Waziri wa Afya Zanzibar Mahmoud
Thabit Kombo akipata maelezo ya mashine mpya ya kusagia taka za
hospitali kwa Mtaalamu wa mashine hizo kutoka Kenya Benard Abere.
Picha na Makame Mshenga.
……………..
Na Ramadhani Ali/Maelezo Zanzibar
Waziri wa Afya Mahmoud Thabit
Kombo amesema tatizo la kuharibika kwa mashine ya kusagia taka katika
Hospitali Kuu ya Mnazimmoja siku za karibuni kulipelekea kurundikana
kwa
taka na kusababisha usumbufu kwa wananchi.
Amesema baadhi ya wafanyakazi
wakorofi wa Hospitali hiyo walitumia kasoro hiyo kuzitupa taka kwenye
ufukwe wa bahari, nyuma ya Hospitali, ambapo ni kosa kwa mujibu wa
sheria na kanuni za afya na uhifadhi wa mazingira.
Waziri Mahmoud ametoa kauli hiyo
alipofanya ziara ya kutembelea mashine ya kusagia taka zinazozalishwa
katika Hospitali hiyo ambayo hivi sasa imefanyiwa matengenezo na ipo
tayari kufanyakazi na kuondosha kero hilo.
Amesema wafanyakazi saba
waliobainika kufanya kosa la kutupa taka sehemu ya ufukwe wamechukuliwa
hatua za nidhamu na kuuagiza uongozi wa Hospitali ya Mnazimmoja
kutomvumilia mfanyakazi atakaekiuka kanuni za afya.
Hata hivyo Waziri wa Afya amekiri
kuwa uzalishaji wa taka katika Hospitali ya Mnazimmoja umekuwa mkubwa
kutokana na ongezeko kubwa la wagonjwa baada ya kutanuliwa na kufikia
daraja la kuwa Hospitali ya rufaa.
Ameyashauri Makampuni yanayohitaji
taka kwa ajili ya kuzisarifu na kuzigeuza kwa ajili ya matumizi mengine
waonane na uongozi wa Hospitali kwani sehemu kubwa ya taka hizo
zinaweza kutumika kwa shughuli nyengine.
Amesema hivi sasa uongozi wa
Hospitali ya Mnazimmoja umeandaa utaratibu mzuri wa kukusanya taka
ambapo za aina moja zinatiwa katika pipa moja na mapipa hayo yamewekwa
katika wodi ili kuondosha usumbufu kwa wafanyakazi, wagonjwa na watu
wanaofika kwa shughuli mbali mbali.
“Nataka wananchi wawe waangalifu
wakati wa kuhifadhi taka kwani kila pipa linatiwa taka maalumu na
hakuna kuchanganya taka zote katika pipa moja,” alisisitiza Waziri
Mahmoud.
Amewataka wafanyakazi wa Hospitali
kusimamia na kuwaelimisha wananchi matumizi ya mapipa hayo ili kila
pipa liingizwe taka zinazostahiki ili kuondosha usumbufu wakati wa zoezi
la kuzisaga.
Mtaalamu wa mashine ya kusagia
taka kutoka Kenya Benard Abere amemueleza Waziri wa Afya kwamba kazi ya
kuifanyia matengenezo mashine hiyo imekamilika na katika kipindi cha
wiki moja mkusanyiko wa taka utaondoka
No comments :
Post a Comment