Shamrashamra za ushindi mnono na
vikombe kwenye michezo minane kati ya kumi ambayo timu za michezo TPDC
ilishiriki katika mashiondano ya Mei Mosi.
Timu za michezo za TPDC zikiwa na mafuriko ya vikombe vya ushindi zilizoupata kwenye mashindano mbalimbali ya Mei Mosi.
………………………………………………………………………..
Shirika la Maendeleo ya Petroli
Tanzania (TPDC) lafanikiwa kubeba vikombe vinanena na medali nne katika
michuano ya mashindano ya Maadhimisho ya Sikukuu ya Wafanyakazi
Duniani-Mei Mosi yaliyofanyika katika viwanja vya Chuo cha Ushirika
Mkoani Kilimanjaro.
Katika mashindano hayo yaliyoanza
tarehe 19 hadi 29 Aprili, 2017 yaliyoandaliwa na COTWU(T) yalihusisha
mashindano katika michezo ya kuvuta kamba, mbio za marathon, mbio za
baiskeli, bao, kalata, draft, mpira wa pete na mpira wa miguu kama
sehemu ya maandalizi ya siku ya Mei Mosi.
Akizungumza na vyombo vya habari
Mwenyekiti wa Michezo wa TPDC ndugu Nelson Rwechunguraalieleza kuwa timu
yake imezidi kuwa bora zaidi kwakuwa mashindano yaliyopita ilifanikiwa
kuchukua jumla ya vikombe vitano na medali tatu lakini katika mashindano
ya safari TPDC imefanikiwa kuchukua vikombe vinane na medali nne.
“Tumeweza kuchukua kikombe cha
mshindi wa wa tatu katika mashindano ya kuvuta kamba kwa wananume,
kikombe cha mshindi wa pili katika mashindano ya kuvuta kamba kwa
wanawake, kikombe cha mshindi wa tatu katika mbio za baiskeli kwa
wanawake na kikombe cha mshindi wa pili kwa upande wa wanaume, kikombe
cha mshindi wa pili katika mashindano ya marathon kwa wanaume na kikombe
cha mshindi wa kwanza kwa upande wa wanaume na kikombe kwa mshindi wa
tatu katika mchezo wa draft’’ alieleza mwenyekiti wa TPDC.
Kwa mujibu wa ndugu Rwechungura
wafanyakazi wa TPDC walioipatia timu vikombe ni Diana Byonge na Peter
Ngalu kwa upande wa baiskeli, Neema Mdegela na Darush Shija kwa upande
wa mbio ndefu na Diana Byonge katikamchezo draft.
Aidha akizungumzia kushindwa
kuchukua ubingwa wa mpira wa miguu, Mwenyekiti alieleza kuwa pamoja na
kufungwa na timu Geita Gold Mining, kwake yeye timu yake ndiyo bingwa wa
mashindano kutokana na mpira mzuri walioonyesha katika mtanange huo
pamoja na kuwa pungufu kwa muda mrefu.
“Pamoja na kushindwa kuchukua
ubingwa wa mpira wa miguu, bado kwangu mimi naichukulia timu yangu kama
ndiye bingwa wa mashindano hayo kwakuwa tumecheza kwa kiwango bora zaidi
na hata watazamaji wameshuhudia hilo na hivyo tumepata faraja na pia
tunawapongeza Geita kwa ushindi walioupata ingawa changamoto zilikuwepo
kwa upande wa maamuzi lakini ndio mchezo na tunatumaini zitafanyiwa kazi
katika mashindano yajayo’’ alieleza mwenyekiti.
Kwa upande wake Kapteni wa timu
ya mpira wa miguu TPDC ameeleza kuwa hatua waliyofikia ya kuwa washindi
wa pili ni ya kumshukuru Mungu kwakuwa timu bora zilikuwa nyingi lakini
‘wao walifanikiwa kufika hatua ya fainali.
“Kiukweli najivunia kuwa na timu
bora zaidi kwenye mashindano haya na hiiimedhihirishwa na ushindi
tuliokuwa tukiupata hadi kufikia hatua na tumecheza vizuri saana pamoja
ya kuwa pungufu kwa zaidi ya dakika 76 lakini bado tumeweza kuwadhibiti
wa pinzania wetu kwa muda mrefu hadi walipoweza kutufunga gori la pili
ambapo hadi mwisho wa mchezo tulitoka gori mbili kwa moja’’ alichambua
kapteni wa TPDC.
Aidha alisisitiza kuwa waajiri
wanapaswa kuzingatia na kusisitiza michezo kwa wafanyakazi ili kuboresha
afya za wafanyakazi, kuleta umoja na kutangaza shughuli za Mashirika
kwa wananchi.
No comments :
Post a Comment