Na Magreth Subi,Moshi
Shirika
la umeme Nchini Tanzania (TANESO) limeibuka kidedea katika maonesho ya wakala
wa Afya na Usalama Mahali pa Kazi (OSHA) ambayo yamefikia kilele chake Aprili
28, 2017 Mjini Moshi.
Mgeni Rasmi katika maonesho hayo, Waziri wa Nchi
Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na wenye Ulemavu Mhe. Jenista
Mhagama,(pichani katikayi), alitoa pongeza kwa TANESCO kwa Huduma nzuri inayotolewa katika kuhudumia
jamii na kuwataka Wafanyakazi kuwa na ari siku zote pamoja na changamoto
wanazokutana nazo kwani changamoto ndio chachu ya maendeleo kuelekea Nchi ya
Viwanda kama kauli mbiu ya Mhe. Rais inavyo sema.
Akizungumza
katika hafla hiyo, Mhe. Mhagama alitoa shukurani kwa washiriki na kutangaza
washindi katika Nyanja mbali mbali na TANESCO kuibuka mshindi wa kwanza wa masuala
ya Afya na Usalama kazini mahala pa Kazi katika Sekta ya Huduma kwa Wateja.
Kwa
upande wake, Afisa Mkuu kitengo cha Afya na Usalama Kazini Bw. Fred Kayega alitoa
maelezo ya vifaa mbalimbali vya vinavyotumiwa na Wafanyakazi kujikinga na ajali
pahala pa kazi kwa Mhe. Mhagama alipotembelea banda la TANESCO kabla maonesho
hayo hayajafikia hitimisho.
Baadhi
ya Wafanyakazi wa TANESCO Makao Makuu, pamoja na Wafanyakazi wa Mkoani
Kilimanjaro, walifurahia ushindi huo kwani utazidi kuongeza hari kwa
Wafanyakazi na kufanya vizuri Zaidi katika utendaji wa Kazi.
Mfanyakazi wa TANESCO akitoa maelezo kwa Mhe. Waziri
No comments :
Post a Comment