KWAMBA TAREHE 1.02.2017 MAJIRA YA
SAA 15:45HRS KATIKA ENEO LA IGOMBE – SOKONI KATA YA BUGOGWA WILAYA YA
ILEMELA JIJI NA MKOA WA MWANZA, ASKARI WAKIWA DORIA NA MISAKO
WALIFANIKIWA KUMKAMATA MTU MMOJA ALIYEJULIKANA KWA JINA LA SAMWEL HOSEA
MIAKA 24, MKAZI WA KIJIJI CHA KABANGAJA, AKIWA NA NOTI BANDIA 25 ZA
SHILINGI ELFU KUMI KILA MOJA ZENYE JUMLA YA THAMANI YA TSH 250,000/=.
AIDHA ASKARI WALIENDELEA NA DORIA
NA MISAKO NA ILIPOFIKA MAJIRA YA SAA 20:30HRS USIKU YA TAREHE TAJWA
HAPO JUU KATIKA ENEO LA NYAMANORO ILIYOPO WILAYA YA ILEMELA MKOA WA
MWNZA, ASKARI WALIFANIKIWA KUMKAMATA KIJANA MWINGINE WA KIUME
ALIYEJULIKANA KWA JINA LA PAUL FAIDA MIAKA 21, MKAZI WA GEITA AKIWA NA
NOTI BANDIA 12, ZA SHILINGI ELFU KUMI ZIKIWA NA JUMLA YA THAMANI YA TSH
120,000/=, KITENDO AMBACHO NI KOSA LA JINAI.
AWALI ASKARI WAKIWA KWENYE DORIA
NA MISAKO WALIPOKEA TAARIFA KUTOKA RAIA WEMA KWAMBA KATIKA MAENEO YA
IGOMBE – SOKONI NA NYAMARO WAPO WATU AMBAO INASEMEKANA WANAMILIKI NOTI
BANDIA, POLISI WALIFANYA UFUATILIAJI WA HARAKA KATIKA MAENEO HAYO,
AMBAPO MISAKO NA UPELELEZI ILIFANYIKA KATIKA MAENEO YOTE KWA PAMOJA NA
KUFANIKIWA KUWATIA NGUVUNI WAHALIFU HAO.
WATUHUMIWA WAPO KATIKA MAHOJIANO
NA JESHI LA POLISI, PINDI UCHUNGUZI UKIKAMILIKA WATAFIKISHWA MAHAKAMANI,
ASKARI BADO WANAENDELEA NA UPELELEZI ILI KUWEZA KUBAINI MAHALI AMBAPO
NOTI HIZO ZA BANDIA ZINATENGENEZWA NA WATU WENGINE AMBAO
WANAOSHIRIKIANA NA WATUHUMIWA TAJWA HAPO JUU KATIKA KUFANIKISHA UHALIFU.
KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA
MWANZA KAMISHINA MSAIDIZI WA POLISI AUGUSTINO SENGA ANATOA WITO KWA
WANANCHI AKIWATAKA KUENDELEA KUTOA USHIRIKIANO KWA JESHI LA POLISI ILI
KUWEZA KUENDELEA KUDHIBITI UHALIFU KATIKA MKOA WA MWANZA, LAKINI PIA
ANAWATAKA VIJANA KUACHA TABIA YA KUJIHUSISHA NA UHALIFU ILI WASIJE
WAKAINGIA KWENYE MATATIZO.
KATIKA TUKIO LA PILI,
KWAMBA TAREHE 01.02.2017 MAJIRA
YA SAA 16:00HRS JIONI KATIKA ENEO LA MSITU WA HIFADHI YA SERIKALI WA
BUHINDI ULIPO KIJIJI CHA ILYAMCHELE TARAFA YA BUCHOSA WILAYA YA
SENGEREMA MKOA WA MWANZA, ASKARI WAKIWA PAMOJA NA MAAFISA WA HIFADHI YA
MSITU WA SERIKALI YA BUHINDI WALIFANIKIWA KUTEKETEZA SHAMBA LA BHANGI
LENYE UKUBWA EKARI MBILI NA NUSU AMBALO LILIKUWA NDANI YA HIFADHI HIYO.
POLISI WALIPOKEA TAARIFA ZA UWEPO
WA SHAMBA HILO LA BHANGI KUTOKA KWA MAAFISA WA HIFADHI YA MSITU HUO, NA
KWAMBA WANANCHI AMBAO WANAOISHI KARIBU NA MSITU NDIO WALIOPANDA BHANGI
HIYO KATIKA ENEO HILO NA PINDI WANAPOKATAZWA WAACHE TABIA HIYO WAMEKUWA
WAKIKAIDI NA KUWATISHIA KUWAPIGA KWA MAWE MAAFISA WA HIFADHI HIYO.
ASKARI WALIKWENDA PAMOJA NA MAAFISA HAO HADI ENEO LA HIFADHI YA MSITU NA
KUKUTA ENEO LA EKARI MBILI NA NUSU LIKIWA LIMEOTESHWA BHANGI, ASKARI
KWA KUSHIRIKIANA NA MAAFISA WA HIFADHI YA MSITU WALIFANIKIWA KUTEKETEZA
SHAMBA HILO LA BHANGI LILILOKUWA NA JUMLA YA IDADI YA MICHE 7300 YA
BHANGI. POLISI BADO WANAENDELEA NA UPELELEZI ILI KUWEZA KUWABAINI WATU
AMBAO WALIHUSIKA NA KUOTESHA BHANGI KATIKA ENEO LA MSITU WA HIFADHI YA
SERIKALI WA BUHINDI.
AIDHA KATIKA TUKIO LINGINE LA
TAREHE 02.02.2017 MAJIRA YA SAA 06:00HRS ASUBUHI KATIKA KIJIJI CHA
KAFUNZO KILICHOPO WILAYA YA SENGEREMA MKOA WA MWANZA, ASKARI WAKIWA
KWENYE MISAKO WALIFANIKIWA KUMKAMATA MTU MMOJA ALIYEJULIKANA KWA JINA LA
MKORO MSAMI MIAKA 74, MKAZI WA KIJIJI CHA MAFUNZO, KWA KOSA LA KUOTESHA
MICHE 84 YA BHANGI KWENYE SHAMBA LENYE UKUBWA WA EKARI MOJA NA NUSU,
KITENDO AMBACHO NI KOSA KISHERIA.
AWALI POLISI WALIPOKEA TAARIFA
KUTOKA KWA RAIA WEMA JUU YA UWEPO WA MTU KATIKA KIJIJI TAJWA HAPO JUU
ANAYEJIHUSISHA NA KILIMO CHA BHANGI, ASKARI WALIFANYA UFUATILIAJI JUU YA
TAARIFA HIZO NA KUFANIKIWA KUMKAMATA MTUHUMIWA PAMOJA NA SHAMBA LAKE NA
KUANZA ZOEZI LA KUNG’OA MICHE YOTE YA BHANGI KATIKA SHAMBA HILO KISHA
KUITEKETEZA KWA MOTO.
MTUHUMIWA YUPO KATIKA MAHOJIANO
NA ASKARI, PINDI UCHUNGUZI UKIKAMILIAKA ATAFIKISHWA MAHAKAMANI, POLISI
WANAENDELEA NA UPELELEZI PAMOJA NA MISAKO KATIKA MAENEO YOTE ILI KUWEZA
KUWAKAMATA NA KUWADHIBITI WATU WOTE WANAOJIHUSISHA NA KILIMO HARAMU CHA
BHANGI.
KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA
MWANZA KAMISHINA MSAIDIZI WA POLISI AUGUSTINO SENGA ANATOA WITO KWA
WAKAZI WA JIJI NA MKOA WA MWANZA AKIWATAKA KUENDELEA KUTOA USHIRIKIANO
KWA JESHI LA POLISI, ILI LIWEZE KUWAKAMATA NA KUDHIBITI WATU WOTE AMBAO
WANAJIHUSISHA NA KILIMO HARAMU CHA BHANGI NA KUWAFIKISHA KATIKA VYOMBO
VYA SHERIA.
IMETOLEWA NA,
ACP: AUGUSTINO SENGA
KAIMU KAMANDA WA POLISI (M) MWANZA
No comments :
Post a Comment