Kaimu Mtendaji Mkuu Baraza la
Taifa la Ujenzi,Elias Kissamo akizungumza katika ufunguzi wa mkutano wa
mchakato wa utoaji wa taarifa za miradi ya ujenzi wa miundombinu ya
umma katika ukumbi wa Holiday Inn jijini Dar es Salaam jana. (PICHA NA
ELISA SHUNDA)
Katibu Mkuu kutoka Ofisi ya Rais
Ikulu,Peter Ilomo,akifungua mkutano wa mchakato wa utoaji wa taarifa za
miradi ya ujenzi wa miundombinu ya umma katika ukumbi wa Holiday Inn
jijini Dar es Salaam jana. Kulia ni Mwenyekiti wa Sekta ya Uwazi na
Uwajibikaji katika Ujenzi (Cost Tanzania),Mhandisi Kazungu Magili na
Kaimu Mtendaji Mkuu Baraza la Taifa la Ujenzi,Elias Kissamo.
Wadau wa masuala ya ujenzi wakifuatilia kwa umakini wakati mkutano huo ukiendelea.
Mwenyekiti wa Baraza la Ujenzi la Taifa (Cost Tanzania),Mhandisi Kazungu Magili,akizungumza katika mkutano huo.
Katibu Mkuu kutoka Ofisi ya Rais
Ikulu,Peter Ilomo akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi wa Baraza la
Taifa la Ujenzi Tanzania na wadau wa masuala ya ujenzi nchini.(www.elisashunda.blogspot.com)
……………………………………………………………………………….
NA MWANDISHI WETU
SERIKALI itaokoa angalau Sh.bilioni 900 kwa mwaka endapo itafanikiwa katika utekelezaji wa Mkakati Uwazi katika Ujenzi (CoST).NA MWANDISHI WETU
Aidha kupitia mkakati huo, miradi mbalimbali ya mashirika ya umma 10 inatarajiwa kufanyiwa tathmini itakayokamilika ifikapo Julai mwaka huu.
Akizungumza katika mkutano wa mashauriano ya utoaji wa taarifa za miradi ya ujenzi wa miundombinu ya umma wa baraza la wajenzi, Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Ikulu, Peter Ilomo alisema kuwa mkakati huo utapunguza rushwa na upotevu wa fedha za Serikali.
Ilomo alisema CoST itaisaidia Serikali na umma kujua fedha zinavyotumika katika ujenzi wa miundombinu, kuokoa fedha za umma kwa kupunguza rushwa na kuboresha usimamiaji wa utekelezaji wa miundombinu.
Mwenyekiti wa CoST, Kazungu Magili alitaja mashirika yatakayofanyiwa tathmini na kuweka wazi miradi yake kuwa ni, Wakala wa Majengo (TBA), Wakala wa Barabara (Tanroads) na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC)/.
Mashirika mengine ni mifuko wa Taifa wa hifadhi ya jamii ya NSSF, GEPF, LAPF, Wizara ya Elimu na Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii jinsia Wazee na Watoto na kutoa taarifa kwa umma ambapo utaweza kuitumia kufuatilia utekelezaji wa miradi husika.
Alisema kupitia tathmini hiyo, CoST itapata fursa ya kutambua majengo yaliyojengwa kwa mujibu wa vigezo ama chini ya kiwango halisi cha fedha zilizotolewa na thamani ya jengo husika.
Magili alisema ikitokea kuna baadhi ya miradi imejengwa chini ya kiwango itafikishwa katika mamlaka mbalimbali ikiwemo Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Mamlaka ya Manunuzi ya Umma (PPRA) na Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali (CAG) ili hatua mbalimbali zichukuliwe.
Aidha alisema kuwa awali kabla ya kuanzishwa mkakati huo mambo mengi yalikuwa hayawekwi wazi hali ambayo imekuwa ikisababisha upotevu wa fedha.
No comments :
Post a Comment