Waziri
wa Fedha na Mipango Mhe. Philip Mpango (Mb) akizungumza na Wakurugenzi
Watendaji 12 wanaoziwakilisha nchi zao katika Benki ya Maendeleo ya
Afrika (AfDB), kuhusu hali ya uchumi wa Tanzania, katika ukumbi wa
Wizara ya Fedha na Mipango jijini Dar es Salaam.(Picha zote na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, WFM)
Naibu
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) (kulia)na
Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bw. Doto James (kushoto) wakimsikiliza Waziri
wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb), (hayupo pichani)
alipokuwa akielezea umuhimu wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB)
wakati akizungumza na Wakurugenzi 12 wanaoziwakilisha nchi zao katika
Benki hiyo Mkutano uliofanyika jijini Dar es salaam.
Maafisa waandamizi kutoka Wizara ya Fedha na Mipango wakisikiliza kwa Makini Maelezo ya Mkurugenzi
Mtendaji kutoka Afrika ya Kusini anayeiwakilisha nchi hiyo (AfDB) Bi.
Elizabeth Mmakgoshilekethe (hayupo) pichani wakati wa mkutano kati yake
na Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb) katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango jijini Dar es salaam.
Mkurugenzi Mtendaji kutoka Afrika
ya Kusini anayeiwakilisha nchi hiyo (AfDB) Bi. Elizabeth
Mmakgoshilekethe (kulia) akiipongeza Serikali kwa kuweka vipaumbele vya
maendeleo vinavyoendana na vile vya Benki ya Maendeleo ya Afrika katika
Mkutano na Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Philip Mpango (Mb) (kushoto) katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango jijini Dar es Salaam.
Mmoja
wa Wakurugenzi anayeiwakilisha nchi yake katika Benki ya Maendeleo ya
Afrika (AfDB) akipongeza juhudi za Serikali katika kuwataulia wananchi
wake matatizo ya kiuchumi wakati wa Mkutano kati ya Wakurugenzi hao na
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb) jijini Dar es
salaam.
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb) (kushoto) akifafanua jambo wakati wa Mkutano wake na Mkurugenzi Mtendaji kutoka Afrika ya Kusini anayeiwakilisha nchi hiyo (AfDB) Bi. Elizabeth Mmakgoshilekethe (kulia) katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango, jijini Dar es salaam.
Waziri
wa Fedha na Mipango Mhe. Philip Mpango (Mb), akiongoza mkutano ulio
wakutanisha Wakurugenzi Watendaji wanaoziwakilisha nchi zao katika Benki
ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) kuhusu hali ya uchumi wa Tanzania huku
ahadi zilizotolewa na Benki hiyo zikijadiliwa katika ukumbi wa Wizara ya
Fedha na Mipango jijini Dar es salaam.
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Philip Mpango (Mb), (katikati) na Kiongozi wa Ujumbe wa AfDB,
Bi. Elizabeth Mmakgoshilekethe, kutoka Afrika Kusini (wa pili kushoto),
wakiwa katika picha ya pamoja na Wakurugenzi wengine wanaowakilisha
nchi zao katika Benki ya AfDB baada ya kumalizika kwa Mkutano katika
ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango, jijini Dar es salaam.
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Philip Mpango (Mb) (kulia) na Naibu wake Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) (kushoto) pamoja na Mkurugenzi
Mtendaji kutoka Afrika ya Kusini anayeiwakilisha nchi hiyo (AfDB) Bi.
Elizabeth Mmakgoshilekethe (katikati) wakibadilishana mawazo baada ya
kumalizika kwa Mkutano kuhusu Hali ya uchumi nchini Tanzania katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango, jijini Dar es salaam.
…………………………………………………………………………………
Na Benny Mwaipaja, WFM, Dar es Salaam
Waziri wa Fedha na Mipango
ameishukuru Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) kwa kukubali kuendelea
kufadhili miradi ya maendeleo ya kipaumbele hususani ya ujenzi wa
barabara na usafirishaji wa umeme ili kufungua fursa za kiuchumi katika
kanda ya Magharibi.
Dkt. Mpango ametoa shukrani hizo
alipokutana na Wakurugenzi Watendaji 12 wanaowakilisha nchi zao katika
Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), jijini Dar es salaam.
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe.
Dkt. Philip Mpango (Mb) ameiomba Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB)
kuharakisha kazi za upembuzi yakinifu na hatimaye kutoa fedha ili
utekelezaji wa miradi ya Maendeleo kuanza mapema iwezekanavyo.
Amesema kuwa Benki hiyo iliahidi
kutoa fedha ili kujenga barabara ya Nyakanazi, kupitia Kibondo, Kasulu
hadi Manyovu, kwa kiwango cha lami na kwamba mradi huo ukipatiwa fedha
na kukamilika kwa wakati kutasaidia kuchochea biashara ya wakazi wa
maeneo hayo na Nchi jirani ya Burundi.
Pia mradi wa North – West grid wa
kusafirisha Nishati ya Umeme kutoka Shinyanga hadi Mbeya kupitia Kigoma
Katavi na Rukwa. Mradi huu utawezesha Mikoa ya ukanda wa Magharibi
kupata Nishati ya uhakika ya umeme na kufungua fursa za Maendeleo
mbalimbali yakiwemo ya ujenzi wa Viwanda vidogo na vya kati.
“Katika kikao hicho tumewaeleza
Wakurugenzi hao wa AfDB hatua mbalimbali ambazo Serikali inazichukua
katika kutatua changamoto ya Miundombinu ya Umeme na Barabara, kupanua
fursa za Ajira, na kuharakisha maendeleo ya ukuaji wa Sekta ya Kilimo
ambayo inategemewa na wananchi wengi” Alifafanua Waziri Mpango.
Aidha amewaeleza wageni juu ya
jitihada za Serikali ya Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli za
kukusanya mapato ya kodi na yasiyo ya kodi, kupambana na rushwa na
biashara haramu ya madawa ya kulevya.
Waziri Mpango ametumia fursa hiyo
kuomba AfDB kusaidia kujenga uwezo wa Tanzania kukabiliana na majanga
yakiwemo ya matetemeko ya ardhi, ajali kubwa za majini na kwenye migodi.
Maeneo mengine ambayo AfDB imeombwa kuisaidia Tanzania ni uvunaji wa
rasilimali za bahari (blue economy), kuelekeza mitaji katika Sekta ya
kilimo na kukabiliana na athari za mabadiliko ya Tabia nchi.
Naye Naibu Waziri wa Fedha na
Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) ameipongeza Benki ya AfDB kwa kuwa
mdau mkubwa wa Maendeleo ya nchi za Afrika na hasa Tanzania kwa kuwa
imekuwa mnufaika mkubwa wa program/ miradi inayofadhiliwa na Benki
hiyo.
Amewataka wananchi kutoa
ushirikiano kwa wageni hao watakapokuwa wakitembelea miradi mbalimbali
inayogharamiwa na AfDBi katika siku takribani tano ambazo watakuwepo
nchini
Kwa upande wa Wakurugenzi
Watendaji wa AfDB wanaoziwakilisha nchi zao, wakiongozwa na Mkurugenzi
Mtendaji kutoka Afrika ya Kusini Bi. Elizabeth Mmakgoshilekethe,
wameipongeza Serikali ya Awamu ya Tano kwa mafanikio ya kiuchumi kwa
kuwa Tanzania imekuwa na viashiria vingi ambavyo vinaonesha uchumi wa
Taifa ni imara ukilinganisha na nchi nyingine katika bara la Afrika
kusini mwa jangwa la Sahara.
Aidha wameitaka Tanzania
kuendeleza jitihada za kupambana na Umaskini hasa katika maeneo ya
vijijini na kuongeza fursa za ajira ili kuharakisha maendeleo. Pia
wameipongeza Serikali kwa mikakati waliyonayo kupitia Mpango wa Pili wa
Maendeleo wa miaka mitano kwa kuwa unaendana na vipaumbele vya Benki
hiyo.
Benki hiyo imeitaka pia Tanzania
kushiriki na kuchangamkia fursa za miradi ya kikanda hasa katika Nishati
ya Umeme, Barabara na Reli na pia kuhakikisha utawala bora.
No comments :
Post a Comment