Baaadhi ya ndugu wa marehemu wakiwa wameketi kwa masikitiko wakisubilia muafaka wa kuzikwa kwa ndugu yao.
Kamanda wa Polisi Mkoani Geita Mponjoli Mwabulambo akikiri kutokea kwa tukio hilo mbele ya waandishi wa habari. |
Wanafamilia wakiwa kwenye masikitiko.
IMEANDALIWA NA MADUKA ONLINE.
Famili ya mzee Isaya Neligwa wa
Mto wa Mbu Mkoani Arusha imesusia kuchukua maiti ya Jeremia Isaya
ambayo imehifadhiwa kwenye Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Geita ,huku
wakidai kupata maridhiano na jeshi la polisi kwani ajali hiyo
ilisababishwa na gari ya polisi yenye nambari za usajili PT 4026
iliyomgonga na kusababisha kifo chake.
Tukio hilo la ajali lilitokea
tarehe 12 mwezi wa pili majira ya saa 12:30 jioni Kwenye eneo la
Mwatulole kata ya Buhalahala ambapo gari la kikosi cha kutuliza ghasia
(FFU) likitokea Kasamwa kuja mjini Geita lilimgonga kijana huyo wakati
alipokuwa akivuka barabara kwanda upande mwingine.
Moja kati ya wanafamilia ,Bw
Elineema Mafie,akizungumza ,amesema kuwa msaidizi wa mkuu wa kitengo
cha usalama barabarani alimpigia simu jana na kumwambia kwamba
suala hilo jeshi la polisi halihusiki na kwamba kutokana na maelezo
hayo kutoka kwa polisi na kugoma kukaa na kuzungumzia mwafaka wa
jambo hilo wamegoma kuzika na kwamba hadi pale serikali itakapoingilia
kati.
“Sisi kama familia
tumesikitishwa na kitendo cha polisi kumemgonga kijana wetu na ushahidi
tunao lakini jambo la kusikitisha msaidizi wa mkuu wa kikosi cha usalama
barabarani Mkoani hapa alinipigia simu jana na kuniambia kuwa wao
hawahusiki na suala hili sisi tunasema kuwa hatuna ugomvi na Polisi
nadhani ni vyema tukae nao na kufanya mazunmgumzo ambayo
yatatoa mwafaka wa jambo hili kama watagoma sisi hatutazika hadi pale
serikali itakapoingilia kati”Alisema Mafie.
Baba wa Marehemu,Mzee Isaya
Neligwa, ameelezea kuwa taarifa za kijana wake kufariki alizipata kutoka
kwenye mtandao wa kijamii wa whatsapp kuwa kijana wao amefariki kwa
kugongwa na gari na kutokana na hiyo taarifa ilibidi wafatilie kujua
kama kuna ukweli wa habari ya kijana wake kupoteza uhai.
“Kuna Binti ambaye yupo Dar es
salaam aliona kwenye mtandao wa whatsapp kuwa mzazi au ndugu wa Jeremiah
anatafutwa na kwamba kijana huyo amefariki na kutokana na kwamba na
yeye alikuwa ni mkazi wa mto wa mbu ilibidi atume ndugu zake waje wanipe
taarifa na baada ya kufika tuliwasiliana na Binti ndipo aliponipa
maelekezo ya kufika kwenye hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Geita na
nilipofika nilishuhudia kuwa ndio yeye kiukweli nina masikitiko makubwa
sana kutokana na tukio hili”Alisema Mzee Neligwa kwa masikitiko
Kamanda wa Polisi Mkoani
Geita,Mponjoli Mwabulambo ,alikiri kutokea kwa tukio hilo na
kwamba wanaendelea na uchunguzi wa tukio hilo huku wakimshikilia askari
aliyekuwa akiendesha gari hilo aliyefahamika kwa jina la Kosntebo
Daniel.
Mwili wa Jeremiah Isaya ambao
hadi sasa upo katika chumba cha kuhifadhia maiti kwenye hospitali ya
rufaa ya Geita,kwa siku 17 tangu afariki Dunia na hakuna mwafaka ambao
umekwisha kupatikana kutoka kwa ndugu na jeshi la Polisi Mkoani Hapa.
No comments :
Post a Comment