Mtaalamu
wa lishe katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Mariam Nyamwaira
akizungumza na waandishi wa habari leo kuhusu maadhimisho ya wiki ya
lishe ambayo yameanza leo Januari 30, 2017 na yatahitimishwa Februari 03, mwaka huu. Kulia ni Mtaalamu wa Lishe, Elizabeth Lyimo wa hospitali hiyo.
Mtaalamu wa lishe katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Mariam Nyamwaira akizungumza na waandishi wahabari leo.
…………………………………………………………..
Hospitali
ya Taifa Muhimbili (MNH) inaadhimisha wiki ya lishe kwa lengo la kutoa
elimu kwa jamii juu ya umuhimu wa kuzingatia lishe bora ikiwamo kupima
wingi wa mafuta mwilini.
Maadhimisho hayo yana lenga kupunguza magonjwa yasiyoambukiza kama vile kisukari, magonjwa ya moyo, magonjwa ya figo na saratani.
Mtaalam wa lishe kutoka katika hospitali hiyo, Mariam Nyamwaira amesema katika maadhimisho hayo,
wataalamu wa lishe watapata fursa ya kutoa ushauri kuhusu suala la
lishe, uhusiano wa lishe na mazoezi, kupima urefu na uzito pamoja na
kupima wingi wa mafuta mwilini .
“Lengo
ni kuweka uelewa wa suala la lishe kwani ulaji usiofaa unachangia kwa
kiasi kikubwa watu kupata magonjwa yasiyoambukiza hivyo kupitia wiki hii
tunatoa huduma bure na endapo mtu akibainika kwamba katika hali
hatarishi tutamuingiza kwenye kliniki zetu ambazo zinafanyika hapahapa Muhimbili ,”amesema Bi Nyamwaira.
Leo
jumla ya watu 78 wamepimwa wingi wa mafuta mwilini na kupewa ushauri wa
lishe bora na kati ya hao asilimia 85 wapo hatarini kupata magonjwa
yasioambukiza kutokana na kuzidi uzito.
Maadhimisho hayo yameanza Januari 30, 2017 na yatahitimishwa Februari 03, 2017
No comments :
Post a Comment