Pages

Monday, January 30, 2017

Wiki ya Lishe, Muhimbili Yapima Wingi wa Mafuta Mwilini


him1
Mtaalamu wa lishe katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Mariam Nyamwaira akizungumza na waandishi wa habari leo kuhusu maadhimisho ya wiki ya lishe ambayo yameanza leo Januari 30, 2017  na yatahitimishwa Februari 03, mwaka huu. Kulia ni Mtaalamu wa Lishe, Elizabeth Lyimo wa hospitali hiyo.
him2
Mtaalamu wa lishe katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Mariam Nyamwaira akizungumza na waandishi wahabari leo.
…………………………………………………………..
 
Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) inaadhimisha wiki ya lishe kwa lengo la kutoa elimu kwa jamii juu ya umuhimu wa kuzingatia lishe bora ikiwamo kupima wingi wa mafuta mwilini.
 
Maadhimisho hayo  yana lenga  kupunguza magonjwa yasiyoambukiza kama vile kisukari, magonjwa ya moyo, magonjwa ya figo na saratani.
 
Mtaalam wa lishe kutoka katika hospitali hiyo, Mariam Nyamwaira amesema  katika maadhimisho  hayo, wataalamu wa lishe watapata fursa ya kutoa ushauri kuhusu suala la lishe, uhusiano wa lishe na mazoezi, kupima urefu na uzito pamoja na kupima wingi wa mafuta mwilini .
 
“Lengo ni kuweka uelewa wa suala la lishe kwani ulaji usiofaa unachangia kwa kiasi kikubwa watu kupata magonjwa yasiyoambukiza hivyo kupitia wiki hii tunatoa huduma bure na endapo mtu akibainika kwamba katika hali hatarishi tutamuingiza kwenye kliniki zetu  ambazo zinafanyika hapahapa Muhimbili ,”amesema Bi Nyamwaira.
 
Leo jumla ya watu 78 wamepimwa wingi wa mafuta mwilini na kupewa ushauri wa lishe bora na kati ya hao asilimia 85 wapo hatarini kupata magonjwa yasioambukiza kutokana na kuzidi uzito.
Maadhimisho hayo yameanza Januari 30, 2017  na yatahitimishwa Februari 03, 2017

No comments:

Post a Comment