Akizungumza mapema leo Mwenyekiti wa City Mussa Mapunda
amesema kuwa, ameshtushwa na taarifa ya kifo cha mchezaji huyo aliyekuwa
nguzo kubwa katika mafanikio iliyopata mbeya City tangu ilipanda
daraja na kucheza ligi kuu ya Vodacom.
Binafsi nimeshtushwa na taarifa hizo,Burhan alikuwa sehemu ya mafanikio ya kikosi chetu tangu alipojiunga nasi akitokea Prisons,baada ya kuhamia klabu nyingine tulikuwa tukiwasiliana nae mara kwa mara na kutoa mchango wake pale alipoona pana umuhimu wa kufanya hivyo,hatuna namna nyingine ni kumshukuu Mungu kwa sababu yote ni kazi yake na tunamuomba ampumzishe kwa amani ameni.Kwa upande wao wachezaji Hassan Mwasapili na John Kabanda ambao walicheza pamoja na Marehemu David Burhan kwenye kikosi cha City wameeleza kusikitishwa kwao na taarifa za kifo hicho, huku wakikumbuka namna walivyokuwa wakiishi nae wakati wa uhai wake.
Kwa niaba ya klabu naomba kutoa salamu za pole kwa familia ndugu,jamaa pamoja na wadua wote wa soka, kwa sasa tunaendelea kufanya mawasilino na wana familia ili kujua taratibu zote na klabu itashiriki mazishi ya mpendwa wetu.
No comments:
Post a Comment