Taarifa hiyo imesema kuwa kazi ya
ufunguaji njia imewezekana baada ya Wahandisi na Mafundi wa reli
kuyaondoa Mabehewa yaliopata ajali l kutoka relini na pia kuikarabati
sehemu iliyo haribika . Kazi hiyo imefanyika kuanzia usiku wa Januari
29, 2017 hadi mchana wa Januari 30, 2017.
Aidha treni ya abiria
iliyoahirisha safari ya kuondoka kwenda bara jana imeondoka leo saa
9:05 alasiri kutoka kituo kikuu cha Dar es Salaam kwenda bara..
Wakati huo huo imefahamika kuwa
msafiri mmoja aliyetambulikana kama Nd Basekena O. Bango kutoka
Bujumbura Burundi akiwa anasafiri kutoka Kigoma amelazwa katika
Hospitali ya Tumbi Kibaha mkoani wa Pwani kwa ajili ya matibabu zaidi.
Aligunduliwa kuwa amechanika mguu wake wa kulia hivyo basi kuhitaji
kushonwa mguu wake huo.
Taarifa kutoka Muhimbili
zinaeleza kulazwa kwa majeruhi wawili waliopokelewa hospitalini hapo
usiku wa Januari 29, 2017. Majeruhi wamefamika kuwa ni Nd. Stephania
Mbona (46) kutoka Kigoma alikuwa amekuja Muhimbili kuendelea na matibabu
ya ugonjwa wa tumbo, hata hivyo alitibiwa majeraha ya kawaida na
anaendelea kulazwa kwa ajili ya matibabu ya ugonjwa wake wa tumbo.
Mgonjwa wa pili Nd Alice Jovin
(37) mkazi wa Salasala Dar es Salaam alikuwa anatoka Kigoma kuja Dar es
Salaam amepata majeraha ya kawadia ametibiwa na alitarajiwa kuruhusiwa
leo asubuhi.
Kuhusu idadi ya wasafiri treni ya
Deluxe yenye uwezo wa kusafirisha abiria zaidi ya 1000 wakati inapata
ajali ilikuwa na abiria 480.
Aidha imefahamika kuwa ili
kufahamika hasara na sababu za ajali hiyo taarifa rasmi itatolewa baada
ya uchunguzi wa Kamati maalum inayoundwa kwa mujibu wa sheria,
taratibu na kanuni za uendeshaji reli za kimataifa. Taarifa hiyo
itatolewa baada ya wiki mbili.
Imetolewa na Afisi ya Uhusiano:
Kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa TRL
Ndugu Masanja Kungu Kadogosa
Januari 30, 2017
DAR ES SALAAM
No comments:
Post a Comment