OLIVIER GIROUD KAMA 'MKHI' WA MAN U ATUMBUKIZA GOLI TAMU
Goli tamu la Olivier Giroud
alilolifunga kwa mpira wa kisigino kwa nyuma limechochea ushindi wa
Arsenal wa magoli 2-0 dhidi ya Crystal Palace na kukwea hadi katika
nafasi ya tatu ya msimamo wa ligi.
Mfaransa Giroud alilazimika kujaribu
bahati kwa kupiga mpira kwa mtindo wa shuti la Nge baada ya pande la
Alexis Sanchez kupitia nyuma yake.
Arsenal ilipata goli lake la pili
kupitia kwa Alex Iwobi aliyefunga kwa mpira wa kichwa, kabla ya
Palace kupoteza nafasi nzuri ya kufunga iliyookolewa na kipa Petr
Cech.
Olivier Giroud akifunga goli la kwanza la Arsenal kwa shuti la Nge
Alex Iwobi akifunga goli kwa mpira wa kichwa
No comments :
Post a Comment