Tuesday, January 3, 2017

UPASUAJI WA KUUNGANISHA MISHIPA YA DAMU KWA AJILI YA KUSAFISHIA DAMU KWA WAGONJWA WENYE MATATIZO YA FIGO WAFANYIKA KATIKA TAASISI YA MOYO YA JAKAYA KIKWETE (JKCI)


upasu
Daktari bingwa wa upasuaji wa moyo na mishipa ya damu ambaye pia ni Mkurugenzi wa huduma ya Upasuaji wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI)  Bashir Nyangasa na Dk. Sun Long wakimfunga bandeji  mgonjwa leo mara baada ya kumaliza kumfanyia upasuaji wa kuunganisha mishipa ya damu (AVF- Arterio Venous Fistula) kwa ajili ya kusafishia damu kwa wagonjwa wenye matatizo ya figo (Hemodialysis).
upasu-1
upasu-2
 Daktari bingwa  wa upasuaji wa kifua, moyo na mishipa ya damu wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) Wambura Wandwi (Kulia) na Dkt. Bingwa wa Upasuaji  Hussein  Hassan wakimfanyia mgonjwa leo upasuaji wa kuunganisha mishipa ya damu (AVF- Arterio Venous Fistula) kwa ajili ya kusafishia damu kwa wagonjwa wenye matatizo ya figo (Hemodialysis). Kushoto ni Afisa Muuguzi wa chumba cha upasuaji Sr. Elina Mulenda.
upasu-3
 Daktari bingwa wa upasuaji wa moyo na mishipa ya damu ambaye pia ni Mkurugenzi wa huduma ya Upasuaji wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI)  Bashir Nyangasa (aliyevaa kofia ya pinki) akiwaonyesha kitu Dkt. bingwa  wa upasuaji wa kifua, moyo na mishipa ya damu Wambura Wandwi (Kulia) na Dkt. Bingwa wa Upasuaji  Hussein  Hassan wakati wakimfanyia mgonjwa upasuaji wa kuunganisha mishipa ya damu (AVF- Arterio Venous Fistula) kwa ajili ya kusafishia damu kwa wagonjwa wenye matatizo ya figo (Hemodialysis).
Picha na Anna Nkinda – JKCI

No comments :

Post a Comment