Daktari bingwa wa upasuaji wa moyo
na mishipa ya damu ambaye pia ni Mkurugenzi wa huduma ya Upasuaji wa
Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) Bashir Nyangasa na Dk. Sun
Long wakimfunga bandeji mgonjwa leo mara baada ya kumaliza kumfanyia
upasuaji wa kuunganisha mishipa ya damu (AVF- Arterio Venous Fistula)
kwa ajili ya kusafishia damu kwa wagonjwa wenye matatizo ya figo
(Hemodialysis).
Daktari bingwa wa upasuaji wa
kifua, moyo na mishipa ya damu wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete
(JKCI) Wambura Wandwi (Kulia) na Dkt. Bingwa wa Upasuaji Hussein
Hassan wakimfanyia mgonjwa leo upasuaji wa kuunganisha mishipa ya damu
(AVF- Arterio Venous Fistula) kwa ajili ya kusafishia damu kwa wagonjwa
wenye matatizo ya figo (Hemodialysis). Kushoto ni Afisa Muuguzi wa
chumba cha upasuaji Sr. Elina Mulenda.
Daktari bingwa wa upasuaji wa
moyo na mishipa ya damu ambaye pia ni Mkurugenzi wa huduma ya Upasuaji
wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) Bashir Nyangasa (aliyevaa
kofia ya pinki) akiwaonyesha kitu Dkt. bingwa wa upasuaji wa kifua,
moyo na mishipa ya damu Wambura Wandwi (Kulia) na Dkt. Bingwa wa
Upasuaji Hussein Hassan wakati wakimfanyia mgonjwa upasuaji wa
kuunganisha mishipa ya damu (AVF- Arterio Venous Fistula) kwa ajili ya
kusafishia damu kwa wagonjwa wenye matatizo ya figo (Hemodialysis).
Picha na Anna Nkinda – JKCI
No comments:
Post a Comment