Afisa Mkuu wa Mauzo kutoka
Kampuni hiyo Peter Ngota akizungumza a waandishiwa habari kwenye ukumbi
wa Idara ya Habari Maelezo leo wakati akitangaza udhamini wa timu hiyo
katika michezo ya vyuo vikuu katika mpira wa ufukweni Katikati ni Jully
Mwakalebela na kulia ni Mkuu wa mashindano hayo John Mwansasu.
……………………………………………………………………………..
Na. Lilian Lundo – MAELEZO
Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL)
imedhamini mashindano ya Soka la ufukweni kwa wanafunzi wa Vyuo Vikuu
vilivyopo Jijini Dar es Salaam yanayotarajiwa kufanyika katika fukwe za
Coco Januari 07 mwaka huu.
Afisa Mkuu wa Mauzo kutoka
Kampuni hiyo Peter Ngota ameyasema hayo leo, Jijini Dar es Salaam
alipokuwa akiongea na waandishi wa habari juu ya udhamini huo.
Aliendelea kwa kusema kuwa,
mashindano hayo yanawalenga wanafunzi wa Vyuo Vikuu vilivyopo Jijini Dar
es Salaam ambao ni wadau wakubwa wa Kampuni ya TTCL kupitia huduma
ambazo wanazitoa kama vile vifurushi vya intanenti, dakika pamoja na
ujumbe mfupi.
“Tumeamua kudhamini mashindano
hayo kwa wanafunzi hao kutokana na umuhimu wa michezo kwao katika
kuwajengea amani, furaha na afya njema ambavyo vitawawezesha kufanya
vizuri katika masomo yao na hata kuwa wabunifu katika maeneo wanayosomea
na kupelekea nchi kufikia uchumi wa kati,” alifafanua Ngota.
Kwa upande wake kocha Mkuu wa
mashindano hayo John Mwansasu ameishukuru Kampuni ya TTCL kwa kudhamini
mashindano hayo ambayo bado hayajapata umaarufu mkubwa hapa nchini.
Aidha amesema kuwa, ili kuwapa
uzoefu washiriki wa mashindano hayo, kutakuwepo na wachezaji ambao
walichezea timu za Simba na Yanga ambao pia watacheza kutokana na timu
ambazo walikuwa wakichezea.
Vilevile Mwansasu amesema kuwa,
wataendelea kushirikiana na Kampuni ya TTCL ili kusambaza mchezo huo
katika mikoa yote ya Tanzania.
Vyuo vilivyothibitisha ushiriki
wa mashindano hayo mpaka sasa ni Chuo cha Biashara (CBE), Chuo Kikuu cha
Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere, Chuo Kikuu Huria (OUT), Chuo cha
Usimamizi wa Fedha (IFM), Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) pamoja na
Taasisi ya Teknolojia Dar es salaam (DIT). Mashindano hayo hayatakuuwa
na kiingilio na yataanza saa 3:00 asubuhi
No comments :
Post a Comment