Mkurugenzi
Mkuu wa TBL Group na Mkuu wa Kitengo cha Masoko Kanda ya Afrika
Mashariki ,Robert Jarrin,(kushoto) akibadilishana mawazo na mtaalamu wa uzalishaji wa Dodoma Wine, Erik Schlunz (kulia) wakati wa maonyesho ya kuonja Mvinyo yaliyoandaliwa na kampuni ya Tanzania Distilleries Limited (TDL)
Mfanyakazi wa wa
kampuni ya Tanzania Distilleries Limited (TDL) ,Maleke Hans,
akiwamiminia mvinyo chapa ya Dodoma wine baadhi ya wakazi wa jijini la
Dar es Salaam, waliotembelea maonyesho hayo.
Baadhi
ya wakazi wa jiji la Dar es Salaam, waliotembelea kwenye banda la
Tanzania Distilleries Limited (TDL) wakihudumiwa kinywaji cha Dodoma
wine
Uonjaji wa wine ukiendelea
Wananchi wakielezwa ubora wa mvinyo wa Dodoma Wine
Baadhi
ya wakazi wa jiji la Dar es Salaam, waliotembelea kwenye banda la
Tanzania Distilleries Limited (TDL) wakihudumiwa kinywaji cha Dodoma
wine
Mvinyo uliwaleta pamoja wananchi waliohudhuria na kuwapatia fursa ya kufurahi na kubadilishana mawazo
……………………………………………………………
-Wakulima wa zabibu nchini kuendelea kunufaika
Wine bora za
aina mbalimbali zinazotengenezwa na kampuni ya Tanzania Distilleries
Limited (TDL) maarufu kama Konyagi ambayo iko chini ya kampuni ya TBL
Group zimekuwa kivutio kikubwa katika tamasha la kuonja mvinyo
lililoandaliwa na kampuni hiyo na kufanyika katika hoteli ya Southernsun
iliyopo jijini Dar es Salaam jana.
Wananchi wengi waliohudhuria tamasha hilo ambalo hufanyika kila mwaka walivutiwa
na ubora wa mvinyo unaotengenezwa na TDL kwa kuwa na viwango vya hali
ya juu na kukubalika katika masoko ya kimataifa.
Mmoja
wa wananchi waliohudhuria tamasha hilo,Julius Kadege akiongea kwa niaba
ya wenzake alisema kuwa inatia moyo kuona sekta ya mvinyo hapa nchini
inazidi kukua na kuwa na chapa mbalimbali zenye viwango vya kimataifa
Meneja Chapa wa kampuni ya TDL,Warida Kimaro,alisema kuwa mvinyo
unaotengenezwa na kampuni hiyo hivi sasa unakubalika katika masoko
mbalimbali ya hapa nchini na nje ya nchi na kampuni imejipanga
kukabiliana na ushindani mkubwa uliopo katika masoko ya mvinyo.
“TDL Chini ya TBL Group tumejipanga kuhakikisha tunaendelea kuingiza sokoni bidhaa bora na kukabiliana na changamoto
mbalimbali zilizopo kwenye masoko ikiwemo ushindani wa kibiashara na
upatikanaji wa malighafi bora nchini pia tunahakikisha kupitia sekta hii
ya mvinyo tunaboresha maisha ya watanzania kuwa bora kupitia kutuuzia
malighafi”.Alisema.
Aliongeza kusema kuwa hadi kufikia sasa zaidi ya wakulima 700 wa zao la zabibu mkoani Dodoma wananufaika na mpango wa kilimo shirikishi unaoendeshwa na TDL ambao umeanza kuonyesha mafanikio kwa kuwawezesha wakulima kuongeza uzalishaji katika mashamba yao ya zabibu.
Kimaro
alisema kuwa mpango shirikishi na wakulima wa zabibu umeanza
kutekelezwa katika vijiji vya Bihawana, Mpunguzi, Mvumi, Hombolo,
Mbabala, Veyula, Makang’wa, Mzakwe na Mbalawala na jitihada zinafanyika
kuhakikisha vijji vingi vinashiriki.
Alisema
kuwa Chini ya mpango huo wakulima wanawezeshwa kupatiwa utaalamu wa
kilimo kwa kushirikiana na taasisi ya Makutupora Viticulture Training
and Research Center (MVTRC) ambapo mafanikio ya mpango huu yameanza
kuleta mafanikio kwa wakulima kupatiwa elimu ya kilimo cha kisasa cha
zao la zabibu,kupatiwa mbegu bora na za kisasa na kuanza kufanya
utekelezaji kwa kutumia ushauri wa wataalamu wa kilimo.
Katika kuwapatia wakulima motisha wakulima ili wajiunge na waweze kuboresha maisha yao kupitia kilimo cha zao la zabibu chini ya mpango huu alisema watoto wa wakulima wa zabibu wamekuwa wakisaidiwa kielimu kupitia mfuko unaojulikana kama Zabibu na Shule Kwanza
No comments :
Post a Comment