Pages

Monday, January 30, 2017

TDL yajipanga kukuza zaidi biashara ya mvinyo nchini


ti1Mkurugenzi Mkuu wa TBL Group na Mkuu wa Kitengo cha Masoko Kanda ya Afrika Mashariki ,Robert Jarrin,(kushoto) akibadilishana mawazo na  mtaalamu wa uzalishaji wa  Dodoma Wine, Erik Schlunz  (kulia) wakati wa maonyesho ya kuonja Mvinyo yaliyoandaliwa na kampuni ya Tanzania Distilleries Limited (TDL) 
ti2
ti3
Mfanyakazi wa  wa kampuni ya Tanzania Distilleries Limited (TDL) ,Maleke Hans, akiwamiminia mvinyo chapa ya Dodoma wine baadhi ya wakazi wa jijini la Dar es Salaam, waliotembelea maonyesho hayo.
ti4 ti5
Baadhi ya wakazi wa jiji la Dar es Salaam, waliotembelea kwenye banda la Tanzania Distilleries Limited (TDL) wakihudumiwa kinywaji cha Dodoma wine
ti6
Uonjaji wa wine ukiendelea
ti7
Wananchi wakielezwa ubora wa mvinyo wa Dodoma Wine
ti8
Baadhi ya wakazi wa jiji la Dar es Salaam, waliotembelea kwenye banda la Tanzania Distilleries Limited (TDL) wakihudumiwa kinywaji cha Dodoma wine
ti9
Mvinyo uliwaleta pamoja wananchi waliohudhuria na kuwapatia fursa ya kufurahi na kubadilishana mawazo
……………………………………………………………
-Wakulima wa zabibu nchini kuendelea kunufaika
Wine bora  za aina mbalimbali zinazotengenezwa na kampuni ya Tanzania Distilleries Limited (TDL) maarufu kama Konyagi ambayo iko chini ya kampuni ya TBL Group zimekuwa kivutio kikubwa katika tamasha la kuonja mvinyo lililoandaliwa na kampuni hiyo na kufanyika katika hoteli ya Southernsun iliyopo jijini Dar es Salaam  jana.
Wananchi wengi waliohudhuria tamasha hilo ambalo hufanyika kila mwaka   walivutiwa na ubora wa mvinyo unaotengenezwa na TDL kwa kuwa na viwango vya hali ya juu na kukubalika katika masoko ya kimataifa.
Mmoja wa wananchi waliohudhuria tamasha hilo,Julius Kadege akiongea kwa niaba ya wenzake alisema kuwa inatia moyo kuona sekta ya mvinyo hapa nchini inazidi kukua na kuwa na chapa mbalimbali zenye viwango vya kimataifa
Meneja Chapa wa kampuni ya TDL,Warida Kimaro,alisema kuwa  mvinyo unaotengenezwa na kampuni hiyo hivi sasa unakubalika katika masoko mbalimbali ya hapa nchini na nje ya nchi na kampuni imejipanga kukabiliana na ushindani mkubwa uliopo katika masoko ya mvinyo.
“TDL Chini ya TBL Group tumejipanga kuhakikisha tunaendelea kuingiza sokoni bidhaa bora na  kukabiliana na  changamoto mbalimbali zilizopo kwenye masoko ikiwemo ushindani wa kibiashara na upatikanaji wa malighafi bora nchini pia tunahakikisha kupitia sekta hii ya mvinyo tunaboresha maisha ya watanzania kuwa bora kupitia kutuuzia malighafi”.Alisema.
Aliongeza kusema kuwa hadi kufikia sasa zaidi ya wakulima  700 wa zao la zabibu mkoani Dodoma wananufaika na  mpango wa kilimo shirikishi unaoendeshwa na TDL  ambao umeanza kuonyesha mafanikio kwa kuwawezesha wakulima kuongeza uzalishaji  katika mashamba yao ya zabibu.
Kimaro alisema kuwa mpango shirikishi na wakulima wa zabibu umeanza kutekelezwa katika vijiji vya Bihawana, Mpunguzi, Mvumi, Hombolo, Mbabala, Veyula, Makang’wa, Mzakwe na Mbalawala na jitihada zinafanyika kuhakikisha vijji vingi vinashiriki.
Alisema kuwa Chini ya mpango huo wakulima wanawezeshwa kupatiwa utaalamu wa kilimo kwa kushirikiana na taasisi ya Makutupora Viticulture Training and Research Center (MVTRC) ambapo mafanikio ya mpango huu yameanza kuleta mafanikio kwa wakulima kupatiwa elimu ya kilimo cha kisasa cha zao la zabibu,kupatiwa mbegu bora na za kisasa na kuanza kufanya utekelezaji kwa kutumia ushauri wa wataalamu wa kilimo.
Katika kuwapatia wakulima motisha wakulima ili wajiunge na  waweze kuboresha maisha yao kupitia kilimo cha zao la zabibu chini ya mpango huu alisema watoto wa wakulima wa  zabibu wamekuwa wakisaidiwa kielimu kupitia  mfuko unaojulikana kama Zabibu na Shule Kwanza

No comments:

Post a Comment