PENATI MBILI ZA JERMAIN DEFOE ZAINYIMA USHINDI LIVERPOOL
Jermain Defoe amefunga penati mbili
wakati Sunderland ikitokea nyuma mara mbili na kupata pointi katika
mchezo dhidi ya Liverpool iliyokatika nafasi ya pili katika msimamo
wa Ligi Kuu ya Uingereza
Liverpool ilipata goli la kuongoza
kupitia kwa Daniel Sturridge kwa kichwa cha kubetua baada ya kuzembea
kwa Dejan Lovren. Sunderland walisawazisha dakika sita baadaye
kupitia kwa penati iliyopigwa na Defoe.
Sadio Mane aliwafungia wageni
Liverpool goli la pili kwa shuti la kumalizia la karibu, lakini
baadaye Mane akashika mpira na Defoe tena bila ajizi akatumbukiza
mpira wavuni kwa mkwaju wa penati.
Daniel Sturridge akiwa ameubetua kwa kichwa mpira uliojaa wavuni
Jermain Defoe akiwa amejipinda kuachia shuti la mkwaju wa penati na kufunga
No comments :
Post a Comment