Pages

Tuesday, January 3, 2017

MANCHESTER CITY YAIBUKA NA USHINDI IKIWA NA WACHEZAJI 10 UWANJANI

MANCHESTER UNITED YAFUNGANA POINTI NA TOTTENHAM SPURS KATIKA NAFASI YA TANO

PENATI MBILI ZA JERMAIN DEFOE ZAINYIMA USHINDI LIVERPOOL

Jermain Defoe amefunga penati mbili wakati Sunderland ikitokea nyuma mara mbili na kupata pointi katika mchezo dhidi ya Liverpool iliyokatika nafasi ya pili katika msimamo wa Ligi Kuu ya Uingereza

Liverpool ilipata goli la kuongoza kupitia kwa Daniel Sturridge kwa kichwa cha kubetua baada ya kuzembea kwa Dejan Lovren. Sunderland walisawazisha dakika sita baadaye kupitia kwa penati iliyopigwa na Defoe.

Sadio Mane aliwafungia wageni Liverpool goli la pili kwa shuti la kumalizia la karibu, lakini baadaye Mane akashika mpira na Defoe tena bila ajizi akatumbukiza mpira wavuni kwa mkwaju wa penati.
                                    Daniel Sturridge akiwa ameubetua kwa kichwa mpira uliojaa wavuni
                Jermain Defoe akiwa amejipinda kuachia shuti la mkwaju wa penati na kufunga

No comments:

Post a Comment