Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa pamoja na balozi wa Uingereza
hapa nchini Sarah Cooke (kushoto) wakiweka jiwe la msingi katika ujenzi
wa Shule ya Sekondari ya Wavulana Ihungo mkoani Kagera. Shule hiyo
inajengwa upya kufatia kuathirika na tetemeko la Ardhi lililotokea
mkoani humo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akitazama wakati Balozi wa Uingereza
hapa nchini Sarah Cooke alipokuwa akibonyeza kitufe kuashiria uzinduzi
wa mradi wa ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Wavulana Ihungo mkoani
Kagera. Wakwanza kushoto ni Waziri wa Elimu Profesa Joyce Ndalichako.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Balozi wa uingereza hapa nchi
Sarah Cooke wakikagua ujenzi wa majengo ya Shule ya Sekondari ya
Wavulana Ihungo mkoani Kagera.
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa
Majengo nchini (TBA) Elius Mwakalinga akitoa maelezo ya mradi huo kwa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli wakati
wa ukaguzi.
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa
Majengo nchini Elius Mwakalinga akitoa maelezo ya mradi huo kwa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli wakati wa
ukaguzi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mbunge wa Bukoba
mjini(CHADEMA) Wilfred Lwakatare mara baada ya kuwasili katika shule ya
Sekondari Ihungo mkoani Kagera
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Charles Masinde mmoja
wa wanachi mkoani Kagera aliyeamua kujenga nyumba yake mwenyewe mara
baada ya tetemeko. Rais Dkt. Magufuli amemuahidi mwananchi huyo kuwa
atampatia mabati 30 kwa ajili ya kuezekea nyumba yake.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifafanua jambo wakati alipokuwa
akikagua majengo ya shule ya Sekonadri ya Wavulana Ihungo ambayo
yanajengwa na Wakala wa Majengo Tanzania (TBA).
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisaini Kitabu cha wageni pamoja na
balozi wa Uingereza hapa nchini Sarah Cooke mara baada ya kuwasili
katika uwanja wa mkutano katika Shule ya Sekondari Ihungo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Mkuu wa mkoa wa
Kagera Meja Jenerali Mstaafu Salum Kijuu.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwahutubia wananchi wa maeneo ya
Ihungo Sekondari Mkoani Kagera hawapo pichani mara baada ya kukagua na
kuweka jiwe la msingi katika Shule ya Sekondari Ihungo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mkuu wa mkoa wa Kagera Meja
Jenerali Mstaafu Salum Kijuu wakitoka kwenye ukaguzi wa shule ya
Sekondari Omumwani mkoani Kagera. PICHA NA IKULU
……………………………………………………………….
Na Daudi Manongi – MAELEZO.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amewataka Wakuu wa Mikoa,Wilaya
na Wakurugenzi wa Halmashauri kuondoa utitiri wa kodi uliopo kwenye
Mazao ili wakulima waweze kunufaika kutokana na kujiongezea kipato.
Agizo hilo alimetolewa leo wakati
akihutubia wakazi wa Wilaya ya Bukoba na watanzania kwa ujumla akiwa
katika ziara ya kikazi ya siku mbili Mkoani Kagera.
“Nawaagiza Wakuu wa Mikoa,Wilaya
pamoja na Wakurugenzi wa Halmashauri kupitia upya Kodi zilizopo katika
bidhaa mbalimbali kama Kahawa na Pamba, hakikisheni mnaondoa utitiri huu
wa Kodi ili wafanyabiashara hawa wafaidike na mazao yao,” Alisema Rais
Magufuli.
Aidha Rais Magufuli amewaahidi
watanzania kuwa atahakikisha anafanya kazi usiku na mchana bila kujali
itikadi, dini na makabila ili kuhakikisha nchi inasonga mbele katika
nyanja zote za kimaendeleo.
Akizungumzia maendeleo ya
michango mbalimbali kwa ajili ya wathirika wa tetemeko la Ardhi mkoani
Kagera Rais Magufuli amesema kuwa mpaka sasa simenti iliyochangwa ni
zaidi ya tani 30,600 na mabati zaidi ya elfu 31,000 ambapo wananchi
wameshaanza kupewa na kujengea.
Amewahimiza wananchi
walioathirika na tetemeko la Ardhi kutotegemea Serikali kuwafanyia kila
kitu na badala yake waanze kujenga na watumie msimu huu wa mvua kulima
ili kujipatia chakula.
Pia Rais Magufuli amewashukuru na
kuwapongeza wahisani waliochangia Maafa ya Kagera na kuwataka kuendelea
na moyo huo katika kulijenga Taifa letu.
No comments :
Post a Comment