Pages

Monday, January 2, 2017

MAGUFULI AWATAKA WAKUU WA WILAYA NA MIKOA KUONDOA UTITIRI WA KODI KATIKA MAZAO


magu1
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa pamoja na balozi wa Uingereza hapa nchini Sarah Cooke (kushoto) wakiweka jiwe la msingi katika ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Wavulana Ihungo mkoani Kagera. Shule hiyo inajengwa upya kufatia kuathirika na tetemeko la Ardhi lililotokea mkoani humo.
magu2
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akitazama wakati Balozi wa Uingereza hapa nchini Sarah Cooke alipokuwa akibonyeza kitufe kuashiria uzinduzi wa mradi wa ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Wavulana Ihungo mkoani Kagera. Wakwanza kushoto ni Waziri wa Elimu Profesa Joyce Ndalichako.
magu3
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Balozi wa uingereza hapa nchi Sarah Cooke wakikagua ujenzi wa majengo ya Shule ya Sekondari ya Wavulana Ihungo mkoani Kagera.
magu4
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Majengo nchini (TBA) Elius Mwakalinga akitoa maelezo ya mradi huo kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli wakati wa ukaguzi.
magu5
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Majengo nchini Elius Mwakalinga akitoa maelezo ya mradi huo kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli wakati wa ukaguzi.
magu6
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mbunge wa Bukoba mjini(CHADEMA) Wilfred Lwakatare mara baada ya kuwasili katika shule ya Sekondari Ihungo mkoani Kagera
magu7
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Charles Masinde mmoja wa wanachi mkoani Kagera aliyeamua kujenga nyumba yake mwenyewe mara baada ya tetemeko. Rais Dkt. Magufuli amemuahidi mwananchi huyo kuwa atampatia mabati 30 kwa ajili ya kuezekea nyumba yake.
magu8
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifafanua jambo wakati alipokuwa akikagua majengo ya shule ya Sekonadri ya Wavulana Ihungo ambayo yanajengwa na Wakala wa Majengo Tanzania (TBA).
magu9
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisaini Kitabu cha wageni pamoja na balozi wa Uingereza hapa nchini Sarah Cooke mara baada ya kuwasili katika uwanja wa mkutano katika Shule ya Sekondari Ihungo.
magu10
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Mkuu wa mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Salum Kijuu.
magu11
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwahutubia wananchi wa maeneo ya Ihungo Sekondari Mkoani Kagera  hawapo pichani mara baada ya kukagua na kuweka jiwe la msingi katika Shule ya Sekondari Ihungo.
magu12
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mkuu wa mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Salum Kijuu wakitoka kwenye ukaguzi wa shule ya Sekondari Omumwani mkoani Kagera. PICHA NA IKULU
……………………………………………………………….
Na Daudi Manongi – MAELEZO.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amewataka Wakuu wa Mikoa,Wilaya na Wakurugenzi wa Halmashauri kuondoa utitiri wa kodi uliopo kwenye Mazao ili wakulima waweze kunufaika kutokana na kujiongezea kipato.

Agizo hilo alimetolewa leo wakati akihutubia wakazi wa Wilaya ya Bukoba na watanzania kwa ujumla akiwa katika ziara ya kikazi ya siku mbili Mkoani Kagera.
“Nawaagiza Wakuu wa Mikoa,Wilaya pamoja na Wakurugenzi wa Halmashauri kupitia upya Kodi zilizopo katika bidhaa mbalimbali kama Kahawa na Pamba, hakikisheni mnaondoa utitiri huu wa Kodi ili wafanyabiashara hawa wafaidike na mazao yao,” Alisema Rais Magufuli.
Aidha Rais Magufuli amewaahidi watanzania kuwa atahakikisha anafanya kazi usiku na mchana bila kujali itikadi, dini na makabila ili kuhakikisha nchi inasonga mbele katika nyanja zote za kimaendeleo.
Akizungumzia maendeleo ya michango mbalimbali kwa ajili ya wathirika wa tetemeko la Ardhi mkoani Kagera Rais Magufuli amesema kuwa mpaka sasa simenti iliyochangwa ni zaidi ya tani 30,600 na mabati zaidi ya elfu 31,000 ambapo wananchi wameshaanza kupewa na kujengea.
Amewahimiza wananchi walioathirika na tetemeko la Ardhi kutotegemea Serikali kuwafanyia kila kitu na badala yake waanze kujenga na watumie msimu huu wa mvua kulima ili kujipatia chakula.
Pia Rais Magufuli amewashukuru na kuwapongeza wahisani waliochangia Maafa ya Kagera na kuwataka kuendelea na moyo huo katika kulijenga Taifa letu.

No comments:

Post a Comment