Waziri wa Mambo ya Katiba na
Sheria Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe akikata utepe kuzindua rasmi Makao
Makuu ya Wizara yaliyopo katika jengo la Masomo ya Biashara na Sheria
katika Chuo Kikuu cha Dodoma ambako Wizara imehamia rasmi makao maku ya
Serikali mkoani Dodoma
Katibu Mkuu Prof sifuni Mchome
akitoa maelezo mafupi kwa Mhe. Waziri Dkt Mwakyembe mara baada ya kukata
utepe na kuzindua rasmi ofisi za wizara mjini Dodoma
Katibu Mkuu Prof sifuni Mchome
akitoa maelezo mafupi kwa Mhe. Waziri Dkt Mwakyembe mara baada ya kukata
utepe na kuzindua rasmi ofisi za wizara mjini Dodoma
Mhe. Waziri Dkt Mwakyembe
akitia saini kitabu cha wageni mara baada ya kukata utepe na kuingia
ndani ya jengo la Wizara ambako alizindua rasmi ofisi za wizara mjini
Dodoma
Mhe. Waziri Dkt Mwakyembe
katika picha ya pamoja na watumishi na wageni wake mara baada ya
kuzindua rasmi ofisi za wizara mjini Dodoma ambako wizara imehamia
rasmi mkoani Dodoma
Mhe. Waziri Dkt Mwakyembe
aksalimiana na viongozi mbalimbali kabla ya kukata utepe na kuingia
ndani ya jengo la Wizara ambako alizindua rasmi ofisi za wizara mjini
Dodoma
……………………………………………………………………..
Waziri wa Mambo ya Katiba na
Sheria Dkt. Harrison Mwakyembe amezindua rasmi Ofisi za wizara yake
mkoani Dodoma na kuwataka Watumishi wa wizara waliohamia Makao Makuu ya
Serikali, Dodoma kutekeleza majukumu yao kama inavyotakiwa.
Dkt Mwakyembe amezindua rasmi
makao makuu ya Wizara ya Mambo ya Katiba na Sheria yaliopo mkoani Dodoma
katika viunga vya Chuo Kikuu cha Dodoma baada ya wizara hiyo na
watumishi wake 31 kuhamia rasmi makao makuu ya Serikali mkoani Dodoma.
Baada ya uzinduzi huo Mhe.
Mwakyembe alisema kitendo cha kuhamia mkoani DODOMA ni utekelezaji wa
agizo la kuhamia makao makuu ya Serikali ambalo lilitolewa mwezi Julai
mwaka 2016 na hivyo watumishi wanapaswa kutekeleza majukumu yao na
kuwahudumia wananchi kama walivyokuwa Dar es salaam.
Uzinduzi huo ulihudhuriwa na Jaji
Mfawidhi Kanda ya Dodoma, Mkuu wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali
kanda ya Dodoma, Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Dodoma, Prof Kikula na
watumishi 31 wa wizara ambao wamehamia Dodoma katika awamu ya kwanza ya
utekelezaji wa agizo hilo la Serikali.
Awamu ya Kwanza yenye watumishi
31 wa wizara wakiongozwa na Waziri Dkt Dkt. Harrison Mwakyembe, Katibu
Mkuu Prof. Sifuni Mchome na Naibu Katibu Mkuu Bw. Amon Mpanju imehamia
rasmi mkoani Dodoma. Awamu ya pili na ya tatu zitafuata utaratibu ambao
umewekwa na zoezi hilo linatarajiwa kukamilika mapema mwaka 2018.
Kufuatia kuhama rasmi kwa ofisi
za wizara sasa mawasiliano yote yatafanywa kupitia anuani ya Katibu Mkuu
Sanduku la Posta 315 Dodoma, namba ya simu ni 026 2321680, nukushi ni
026 2321679 na baru pepe ni ile ile ya km@sheria.go.tz
No comments :
Post a Comment