Sehemu ya Majengo ya Kituo cha
Taaluma ya Uhasibu (Accountancy Profession Center-APC) cha Bodi ya
Uhasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA) kilichofunguliwa na Waziri wa Fedha
na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb) kwa niaba ya Waziri Mkuu Mhe.
Kassim Majaliwa, katika eneo la Bunju, Nje kidogo ya Jiji la Dar es
salaam
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe.
Dkt. Philip Mpango (Mb), akiwasili katika viunga vya kituo cha Taaluma
ya Uhasibu (APC) cha Bodi ya Uhasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA) katika
aneo la Bunju nje kidogo ya Jiji la Dar es salaam na kulakiwa na
Mwenyekiti wa Bodi ya NBAA Prof. Isaya Jairo (Katikati) na Mwenyekiti wa
Bodi ya Mfuko wa Pensheni wa watumishi wa Serikali-GEPF, Bi. Joyce
Shaidi
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe.
Dkt. Philip Mpango (Mb), akisalimiana na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa
Hesabu za Serikali (CAG) Prof. Musa Juma Assad, kabla ya kuzindua Kituo
cha Taaluma ya Uhasibu (APC) cha Bodi ya Uhasibu na Wakaguzi wa Hesabu
(NBAA) kwa niaba ya Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa, katika eneo la
Bunju nje kidogo ya Jiji la Dar es salaam.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe.
Dkt. Philip Mpango (Mb) (wa tatu kutoka kulia) akiambatana na
wakandarasi waliojenga Kituo cha Taaluma ya Uhasibu (APC) pamoja na
wajumbe wa Bodi na Uongozi wa NBAA, kukagua baadhi ya miundombinu ya
kisasa iliyopo katika kituo hicho kilichopo katika eneo la Bunju, Nje
kidogo ya Jiji la Dar es salaam.
Waziri wa Fedha na Mipango. Mhe.
Dkt. Philip Mpango (Mb), akikata utepe kuashiria kufunguliwa rasmi kwa
Kituo cha Taaluma ya Uhasibu (APC) cha Bodi ya Wahasibu na Wakaguzi wa
Hesabu (NBAA) kwaniaba ya Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa, katika eneo
la Bunju, nje kidogo ya Jiji la Dar es salaam.
Baadhi ya wadau walioshuhudia
Waziri wa Fedha na Mipango. Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb), akifungua
rasmi Kituo cha Taaluma ya Uhasibu (APC) cha Bodi ya Wahasibu na
Wakaguzi wa Hesabu (NBAA) kwaniaba ya Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa,
katika eneo la Bunju, nje kidogo ya Jiji la Dar es salaam. Kituo hicho
kimegharimu shilingi Bilioni 33.
Meza Kuu wakiongozwa na Waziri wa
Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb), (wa nne kutoka kulia)
wakiimba Wimbo wa Taifa kabla ya kuanza hotuba mbalimbali, baada ya
kufunguliwa rasmi kwa Kituo cha Taaluma ya Uhasibu (APC) cha Bodi ya
Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA) kilichojengwa eneo la Bunju, nje
kidogo ya Jiji la Dar es salaam.
Wasanii, Mrisho Mpoto na Banana
Zoro, wakitumbuiza wakati wa tukio la kufunguliwa rasmi kwa Kituo cha
Taaluma ya Uhasibu (APC) cha Bodi ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu
(NBAA) kilichojengwa eneo la Bunju, nje kidogo ya Jiji la Dar es
salaam.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe.
Dkt Philip Mpango (Mb), akihutubia baada ya kufunguliwa rasmi kwa Kituo
cha Taaluma ya Wahasibu (APC) kilichojengwa na Bodi ya taifa ya Wahasibu
na Wakaguzi wa Hesabu katika eneo la Bunju, nje kidogo ya Jiji la Dar
es salaam, ambacho ujenzi wake umegharimu shilingi Bilioni 33.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe.
Dkt Philip Mpango (Mb), akihutubia baada ya kufungua rasmi kwaniaba ya
Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa, Kituo cha Taaluma ya Wahasibu (APC)
kilichojengwa na Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu katika
eneo la Bunju, nje kidogo ya Jiji la Dar es salaam, kilichogharimu
shilingi Bilioni 33.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe.
Dkt Philip Mpango (Mb), akimkabidhi Tuzo, Mwenyekiti wa Bodi ya Wahasibu
na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA), Prof. Isaya Jairo, ikiwa ni ishara ya
kutambua mchango wake katika kufanikisha ujenzi wa Kituo cha Taaluma ya
Wahasibu (APC) kilichojengwa na Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa
Hesabu (NBAA), katika eneo la Bunju nje kidogo ya Jiji la Dar es salaam
na kugharimu shilingi Bilioni 33.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe.
Dkt Philip Mpango (Mb), akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Bodi
(NBAA) baada ya kuhitimishwa kwa tukio la kufunguliwa rasmi kwa Kituo
cha Taaluma ya Wahasibu (APC) kilichojengwa na Bodi ya Taifa ya Wahasibu
na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA), katika eneo la Bunju nje kidogo ya Jiji
la Dar es salaam na kugharimu shilingi Bilioni 33.
Picha zote na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Fedha na Mipango
No comments :
Post a Comment