Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri
Mkuu, Jenista Mhagama akizungumza na waandishi wa habari (hawapo
pichani) leo Jijini Dar es Salaam kuhusu siku ya UKIMWI Duniani, kushoto
ni Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo, Dr. Hamis Mwinyimvua.
Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya
Kudhibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS), Dr. Leonard Maboko akifafanua juu
ya takwimu za maambukizi ya UKIMWI wakati wa mkutano na waandishi wa
habari uliofanyika leo jijini Dar es Salaam, kushoto ni Waziri wa Nchi,
Ofisi ya Waziri Mkuu, Jenista Mhagama.
…………………………………
Na Jacquiline Mrisho – MAELEZO
Utafiti
wa Viashiria vya Virusi vya UKIMWI (VVU) na Maralia (THMIS) wa mwaka
2011/2012 kwa upande wa Tanzania Bara vinaonyesha kuwa idadi kubwa ya
wanawake wameambukizwa ugonjwa huo kuliko wanaume.
Akizungumza
na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam, Waziri wa Nchi, Ofisi
ya Waziri Mkuu, Jenista Mhagama alisema takwimu zilizopo sasa
zinaonyesha kuwa asilimia 6.2 ya wanawake wameambukizwa ugonjwa wa
ukimwi ikilinganisha na asilimia 3.8 ya wanaume.
Waziri
Mhagama alisema kuwa kutokana na utafiti huo, maambukizi ya virusi vya
UKIMWI kwa upande wa Tanzania Bara ni asilimia 5.3 na inakadiriwa kuwa jumla
ya watanzania 1,538,382 wanaishi na VVU ambapo vijana wenye umri kati
ya 15-24 ni asilimia 10.6 na watoto walio chini ya miaka 15 ni 11.8.
“UKIMWI bado ni janga kubwa nchini Tanzania kwani takwimu zinaonyesha kuwa maambukizo mapya yanakadiriwa kufikia watu 48,000 kwa mwaka hali ambayo inaashiria kupoteza nguvu kazi kubwa katika nchi yetu”
Kwa
mujibu wa Waziri Mhagama alisema Tanzania itendelea kushirikiana na
nchi nyingine Duniani kuhakikisha wanatokomeza janga la ugonjwa huo ifikapo mwaka 2030.
Aliongeza
kuwa Serikali inaendelea kuwahamisha wananchi waendelee kujitokeza
kupima afya zao ili wajitambue na kujua namna ya kujilinda kwani Shirika
la Afya Duniani (WHO) linasisitiza nchi wanachama kuwaanzishia dawa
mara moja watu wote watakaopima na kugundulika kuwa na VVU.
Naye
Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS), Dr.
Leonard Maboko alisema kuwa kwa mwaka 2015 walioambukizwa VVU walikuwa
Watanzania 2,100,000 ambayo ni idadi kubwa ukilinganisha na idadi ya
sasa lakini pamoja na kushuka kwa idadi hiyo wananchi wanatakiwa kuendelea kujilinda mara dufu.
”Ingawa
maambukizi ya VVU yameshuka kutoka Watanzania 2,100,000 hadi 1,538,382,
Watanzania hatutakiwi kubweteka bali tunatakiwa tufanye jitihada za
pamoja kuhakikisha janga hili linafikia mwisho,”alisema Dr. Maboko.
MWISHO.
No comments :
Post a Comment