Saturday, December 3, 2016

WATUMISHI WATAKAOBAINIKA KULA FEDHA ZA MIRADI KUTIMULIWA

chapaaa
Na Mahmoud Ahmad Arusha
SERIKALI imsisitiza kuwa haitasita kuwatimua watumishi watakaobainika kula feha za miradi ya maendeleo na kukwamisha isikamilike kwa kuwa dhamira ya serikali ni kuwatumikia wananchi wote bila kujali itikadi katika kuboresha maisha yao.
Waziri mkuu ,Kassim Majaliwa, ameyasema hayo Desemba 2   jijini Arusha, alipokuwa akihutubia mkutano wa hadhara kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid, na kusisitiza kuwa serikali inaendelea kuwakumbusha watumishi wa serikali majukumu yao ya kutoa huduma bila upendeleo kwa wananchi wake na akawataka wananchi wasisite kutoa taarifa  iwapo hawatapatiwa huduma stahiki kwa wakati.
Amewataka watumishi wote wa serikali kuhakikisha Wanaisoma Ilani ya uchaguzi ya ccm na kuitekeleza hata kama hawaipendi cccm lazima waitekeleze kwa vitendo na si vinginevyo.
Waziri mkuu ameagiza kuanzia keso Jumapili magari aina ya Noah, kufanya huduma ya kusafirisha abiria kutoka maeneno mbalimbali ya nchi kwa kuwa magari hayo yametengenezwa yana uwezo wa kubeba abiria na haelewi kwa nini Sumatra ilikuwa ikiyazuia.
Kuhusu eneo la soko la Kilombero, ambalo lilitolewa bila kufuata taratibu na kumilikishwa kwa mtu binafsi  amesema ardhi ni mali ya serikali na eneo hilo kuanzia leo Desemba 2 ni mali ya serikali  mara baada ya kushinda kesi na akaiagiza halmashauri ya jiji la Arusha, ikamilishe mchakato wa tathimini na kulijenga kwa ajili ya wananchi kufanyia biashara .
Kuhusu maji amesema serikali imetoa shilingi bilioni 476 kwa ajili ya upatikanaji wa maji  Arusha na  tayari shilingi bilioni 2.6  zimeshakabidhiwa mamlaka ya maji safi na taka AUWSA.
Amesema serikali inaendelea kujenga bara bara za lami nchini kote na tayari wakandarasi wa bara bara wameshalipwa madai yao .
Amemuagiza meneja wa Tanesco mkoa wa Arusha, kuhakikisha umeme haukatika katika mkoa huo kwa kuwa tayari serikali imeshatoa fedha za kuboresha mfumo wa umeme .
Katika hatua nyingine Wazirri mkuu amekabidhi pikipiki maarufu Boda boda 200 kwa vijana wa maeneo mbalimbali ya jiji la Arusha wakiwemo walemavu kwa  ajili ya kuzitumia kuwawezesha kiuchumi.

No comments :

Post a Comment