Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri
Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana,Ajira na watu wenye ulemavu Mhe.Jenister
Mhagama akimskiliza Rais wa TUCTA Bw.Tumaini Nyamghokya wakati viongozi
wapya wa TUCTA walipomtembelea Ofisini kwake Magogoni Jijini Dar es
Salaam.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri
Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana,Ajira na watu wenye ulemavu Mhe.Jenister
Mhagama akizungumza na uongozi mpya wa Shirikisho la vyama vya
wafanyakazi nchini(TUCTA) ofisini kwake Magogoni Jijini Dar es
Salaam.Waziri uyo amehaidi kuwapa ushirikiano wa kutosha viongozi hao
ili kuleta tija na ufanisi katika sekta ya kazi.
……………………………………………………………………..
Na Daudi Manongi-MAELEZO
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri
Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na watu wenye ulemavu, Jenister
Mhagama amesema Serikali itaendelea kutoa ushirikiano wa kutosha kwa
viongozi wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Nchini (TUCTA) ili
kuleta tija na ufanisi katika sekta ya kazi.
Waziri Mhagama aliyasema hayo leo
Jijini Dar es Salaam wakati wa mkutano wake na Viongozi hao wa TUCTA
waliofika ofisini kwake kwa ajili ya kujitambulisha mara baada ya
kumalizika kwa uchaguzi wa shirikisho hilo.
“Tumefarijika sana kwa TUCTA
kupata uongozi mpya ambao tuna uhakika wanachama wamezingatia masuala
muhimu katika uchaguzi wao ikiwemo weledi na kutazama dira ya sekta ya
wafanyakazi nchini”.
Aidha aliongeza kuwa Viongozi hao
wana jukumu kubwa la kuleta tija na maendeleo chanya katika sekta ya
kazi nchini na kuhimiza kuwa wafanyakazi ni rasilimali muhimu katika
kuleta maendeleo ya nchi.
Kwa mujibu wa Mhagama ameahidi
Viongozi hao kufanya kikao kazi mapema iwezekanavyo kwani uchaguzi
umekwisha na sasa kilichobaki ni kufanya kazi.
Pia amesisitiza ushirikiano wa
kudumu kati ya Serikali, Waajiri na wafanyakazi ambao utasaidia kwa
kiasi kikubwa kutatua migogoro iliyopo.
Kwa upande wake Rais wa TUCTA,
Tumaini Nyamghokya alimshukuru Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kwa kusimamia
utu wa mtumishi kwa kuhaidi kuwalinda kutokana na baadhi ya viongozi
kutoa lugha zisizosahihi.
Aidha, ameishukuru Serikali kwa kuwa karibu nao kwa muda wote na kuhaidi kuendeleza ushirikiano huo ili kuleta tija katika kazi.
No comments :
Post a Comment