Friday, December 30, 2016

SAKATA LA UUZWAJI WA TREKTA WACHUKUA SURA MPYA VISIWANI PEMBA

trekta
Na  Masanja Mabula –Pemba ..
SAKATA la uuzwaji wa trekta lililonunuliwa  kwa ajili ya mradi wa PADEP na wananchi wa shehia ya Mtemnai na Mlindo Wilaya ya  Micheweni   , limechukua sura mpya baada ya kudaiwa kwamba kilichouzwa sio trekta bali ni mabaki ya trekta na yaliuzwa kama chuma chakavu .
Fundi aliyekuwa akisimamia matrekta ya Mradi wa PADEP Pemba Haji Mussa aliyasema hayo kwenye kikao kilichowashirikisha  wawakilishi wa wananchi wa shehia hizo , masheha wa shehia , maafisa kutoka Wizara ya Kilimo Pemba pamoja na kamati ya Ulinzi na usalama ya Wilaya hiyo .
“Ni lazima tufahamu kwamba kilichouzwa sio trekta bali ni mabaki ya trekta , kwani trekta hilo lilikuwa  scraper baada ya kukaa chini ya mwembe kwa kipindi cha miaka miwili bila ya kufanya kazi na hapa nimekuja na picha zake kama ushahidi wa haya ”alieleza.
 Katika kikao hicho ambacho kilifanyika katika ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Mkuu wa Wilaya hiyo ambapo maelezo hayo yalipingwa na baadhi ya wananchi ambao walihoji kama yaliyouzwa ni mabaki ya trekta , yaliwezaje kufika mkoani na kusafirishwa .
Akizungumza kwenye kikao hicho , Salim Ali alisema kuwa trekta hilo lilikuza ni zima na liliendeshwa  hadi Mkoani ambako lilisafirishwa hadi Mkoa wa Pwani na kwamba  maelezo yaliyotolewa hayana ukweli kinachofanyikwa ni kutaka kuhalalisha biashara iliyofanywa  na wachache kwa maslahi  yao binafsi .
Alifahamisha kwamba hilo trekta lilikuwa ni wananchi wa Shehia ya Mtemani na Mlindo ambao ndiyo waliokuwa wasimamizi , lakini limeuzwa na wachache kinyume na utaratibu sisi tunahesabu kwamb a trekta la jamii limebwa .
“hilo trekta lilikuwa ni la wananchi lakini uuzwaji wake walioshiriki ni wachache na fedha ambazo limuzwa haziendani na thamani yake , kitu chenye thamani ya shilingi milioni 50 , linauzwa kwa shilingi milioni 10 , haiingii akailini naiomba serikali ya Wilaya iliangalie hili kwa umakini zaidi ”alifahamisha .
Aliyekuwa  mshauri mwelekezi wa miradi ya PADEP Wilaya hiyo Amuor Juma Mohammed alisema kwamba Trekta hilo lilikuwa ni mali ya wananchi wa Shehia ya Mtemani na Mlindo ambao waliunda kamati ya kusimamia uendeshaji wake , halikuwa la mradi kama inavyodaiwa na wachache .
Alisema kwamba akiwa ni mshauri mwelekezi wa Mradi wa PADEP wilaya hiyo , hakukuwa na taarifa wala hakushirikishwa kwenye suala la uuzwaji wa trekta hilo .
Akitoa maamuzi ya kikao hicho Mkuu wa Wilaya hiyo Abeid Juma Ali ameliagiza Jeshi la Polisi Wilayani humo kuendelea kufanya uchunguzi juu ya sakata hilo na kutaka uchunguzi huo ukamilike ndani ya mwezi wa ujao .
Aidha Mkuu huyo wa Wilaya amewataka wananchi wa shehia hizo kuendelea kuwa wastahamilivu juu ya sakata hilo wakati Jeshi la Polisi linaendelea na uchunguzi ili kubaini uhalali wa suala hilo .
“ Naliomba Jeshi la Polisi liendelee na uchunguzi juu ya sakata hili , naomba uchunguzi huo ukamilike ndani ya mwezi ujao ili tuone ni anayestahili kubeba lawama ”alisema .
Hata hivyo fedha ambazo zilipatikana  baada ya kuuzwa trekta hilo ambazo ni shilingi milioni 10 zimerejeshwa Serikalini kutoka mikononi mwa wananchi waliohusika na uuzaji huo .

No comments :

Post a Comment