Na Masanja Mabula –Pemba ..
SAKATA la uuzwaji wa trekta lililonunuliwa kwa ajili ya mradi wa PADEP na wananchi wa shehia ya Mtemnai na Mlindo Wilaya ya Micheweni , limechukua sura mpya baada ya kudaiwa kwamba kilichouzwa sio trekta bali ni mabaki ya trekta na yaliuzwa kama chuma chakavu .
Fundi aliyekuwa akisimamia matrekta ya Mradi wa PADEP Pemba Haji Mussa aliyasema hayo kwenye kikao kilichowashirikisha wawakilishi
wa wananchi wa shehia hizo , masheha wa shehia , maafisa kutoka Wizara
ya Kilimo Pemba pamoja na kamati ya Ulinzi na usalama ya Wilaya hiyo .
“Ni lazima tufahamu kwamba kilichouzwa sio trekta bali ni mabaki ya trekta , kwani trekta hilo lilikuwa scraper
baada ya kukaa chini ya mwembe kwa kipindi cha miaka miwili bila ya
kufanya kazi na hapa nimekuja na picha zake kama ushahidi wa haya
”alieleza.
Katika
kikao hicho ambacho kilifanyika katika ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya
Mkuu wa Wilaya hiyo ambapo maelezo hayo yalipingwa na baadhi ya wananchi
ambao walihoji kama yaliyouzwa ni mabaki ya trekta , yaliwezaje kufika
mkoani na kusafirishwa .
Akizungumza kwenye kikao hicho , Salim Ali alisema kuwa trekta hilo lilikuza ni zima na liliendeshwa hadi Mkoani ambako lilisafirishwa hadi Mkoa wa Pwani na kwamba maelezo yaliyotolewa hayana ukweli kinachofanyikwa ni kutaka kuhalalisha biashara iliyofanywa na wachache kwa maslahi yao binafsi .
Alifahamisha
kwamba hilo trekta lilikuwa ni wananchi wa Shehia ya Mtemani na Mlindo
ambao ndiyo waliokuwa wasimamizi , lakini limeuzwa na wachache kinyume
na utaratibu sisi tunahesabu kwamb a trekta la jamii limebwa .
“hilo
trekta lilikuwa ni la wananchi lakini uuzwaji wake walioshiriki ni
wachache na fedha ambazo limuzwa haziendani na thamani yake , kitu
chenye thamani ya shilingi milioni 50 , linauzwa kwa shilingi milioni 10
, haiingii akailini naiomba serikali ya Wilaya iliangalie hili kwa
umakini zaidi ”alifahamisha .
Aliyekuwa mshauri
mwelekezi wa miradi ya PADEP Wilaya hiyo Amuor Juma Mohammed alisema
kwamba Trekta hilo lilikuwa ni mali ya wananchi wa Shehia ya Mtemani na
Mlindo ambao waliunda kamati ya kusimamia uendeshaji wake , halikuwa la
mradi kama inavyodaiwa na wachache .
Alisema
kwamba akiwa ni mshauri mwelekezi wa Mradi wa PADEP wilaya hiyo ,
hakukuwa na taarifa wala hakushirikishwa kwenye suala la uuzwaji wa
trekta hilo .
Akitoa
maamuzi ya kikao hicho Mkuu wa Wilaya hiyo Abeid Juma Ali ameliagiza
Jeshi la Polisi Wilayani humo kuendelea kufanya uchunguzi juu ya sakata
hilo na kutaka uchunguzi huo ukamilike ndani ya mwezi wa ujao .
Aidha
Mkuu huyo wa Wilaya amewataka wananchi wa shehia hizo kuendelea kuwa
wastahamilivu juu ya sakata hilo wakati Jeshi la Polisi linaendelea na
uchunguzi ili kubaini uhalali wa suala hilo .
“
Naliomba Jeshi la Polisi liendelee na uchunguzi juu ya sakata hili ,
naomba uchunguzi huo ukamilike ndani ya mwezi ujao ili tuone ni
anayestahili kubeba lawama ”alisema .
Hata hivyo fedha ambazo zilipatikana baada
ya kuuzwa trekta hilo ambazo ni shilingi milioni 10 zimerejeshwa
Serikalini kutoka mikononi mwa wananchi waliohusika na uuzaji huo .
No comments:
Post a Comment