Sunday, December 4, 2016

MAJALIWA AZINDUA KIWANDA CHA PLASTIC CHA LODHIA JIJINI ARuSHA






Mwenyekiti wa Kampuni ya Lodhia Group Bw. Arun Lodhia akimpokea Waziri Mkuu wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa ili kuzindua kiwanda cha Lodhia Plastic kinachotengeneza Mabomba ya Maji ,kilichopo Njiro jijini Arusha Leo, 3 Disemba 2016.
Mwenyekiti wa Kampuni ya Lodhia Group Bw. Arun Lodhia akitoa maelezo kwa Waziri Mkuu wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa wakati alipofika kuzindua kiwanda cha Lodhia Plastic kinachotengeneza Mabomba ya Maji ,kilichopo Njiro jijini Arusha Leo, 3 Disemba 2016.
Mwenyekiti wa Kampuni ya Lodhia Group Bw. Arun Lodhia (wa kwanza kushoto waliokaa) akiteta jambo na Waziri Mkuu wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa akifuatiwa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo na Naibu waziri wa kilimo ,Mifugo na Uvuvi Mhe. William Ole Nasha wakati walipofika kuzindua kiwanda cha Lodhia Plastic kinachotengeneza Mabomba ya Maji ,kilichopo Njiro jijini Arusha Leo, 3 Disemba 2016.
Waziri Mkuu wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa akikata utepe tayari kwa uzinduzi wa kiwanda cha Lodhia Plastic kinachotengeneza Mabomba ya Maji ,kilichopo Njiro jijini Arusha Leo, 3 Disemba 2016.
Kutoka Kushoto (mwenye suti bluu) ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Lodhia Group Bw. Sailesh Pandit, Mwenyekiti wa kampuni ya Lodhia Group Bw. Arun Lodhia wakiongozana na Waziri Mkuu wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa ndani ya kiwanda cha Lodhia Plastic kinachotengeneza Mabomba ya Maji ,kilichopo Njiro jijini Arusha Leo, 3 Disemba 2016.
Waziri Mkuu wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuzindua kiwanda cha Lodhia Plastic kinachotengeneza Mabomba ya Maji ,kilichopo Njiro jijini Arusha Leo, 3 Disemba 2016.
Mwenyekiti wa Kampuni ya Lodhia Group Bw. Arun Lodhia akimkaribisha Waziri Mkuu wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa ili kuongea na hadhara iliyopo kwenye kiwanda hicho mara baada ya kuzindua kiwanda kinachotengeneza Mabomba ya Maji ,kilichopo Njiro jijini Arusha Leo, 3 Disemba 2016.
Waziri Mkuu wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa akiongea machache mara baada ya kuzindua kiwanda cha Lodhia Plastic kinachotengeneza Mabomba ya Maji ,kilichopo Njiro jijini Arusha Leo, 3 Disemba 2016.
Waziri Mkuu wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa akizindua jiwe la msingi katika kiwanda cha Lodhia Plastic kinachotengeneza Mabomba ya Maji ,kilichopo Njiro jijini Arusha Leo, 3 Disemba 2016.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Lodhia Group Bw. Sailesh Pandit akiagana na Waziri Mkuu wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa mara baada ya kuzindua kiwanda cha Lodhia Plastic kinachotengeneza Mabomba ya Maji ,kilichopo Njiro jijini Arusha Leo, 3 Disemba 2016.
Mwenyekiti wa kampuni ya Lodhia Group Bw. Arun Lodhia akiagana na Waziri Mkuu wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa mara baada ya kuzindua kiwanda cha Lodhia Plastic kinachotengeneza Mabomba ya Maji ,kilichopo Njiro jijini Arusha Leo, 3 Disemba 2016.


Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Lodhia Group Bw. Sailesh Pandit akisoma risala mbele ya Mgeni rasmi ambaye niWaziri Mkuu wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa ndani ya kiwanda cha Lodhia Plastic kinachotengeneza Mabomba ya Maji ,kilichopo Njiro jijini Arusha Leo, 3 Disemba 2016. Picha zote Gadiola Emanuel

habari na Woinde Shizza , Arusha.

Halmashauri za majiji, manispaa na miji wametakiwa kutumia mabomba ya maji yanayozalishwa nchini badala ya kuagiza bidhaa hiyo toka nje ili kuweza kuvinufaisha viwanda vya ndani.


Hayo yamebainishwa na waziri mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa wakati akizindua kiwanda cha kutengeneza mabomba ya Plastic ya maji yenye ukubwa wa aina mbalimbali (Lodhia Plastics ) kilichopo njiro jijini hapa.

Alisema kuwa haiana haja ya halmashauri au majiji kuagiza bidhaa mbalimbali nje ya nchi wakati nchi yetu inaviwanda vya kutosha vya kutengeneza bidhaa hizo.



“Sioni sababu ya wahandisi wa Halmashauri na washauri elekezi halmashauri kushinikiza wakandarasi wa hapa Arusha kwenda kununua mabomba ya maji nje ya mkoa wakati hapa kuna kiwanda kama Lodhia ambacho kinatengeneza hizo bidhaa kwakweli hii labda iwe ni chuki tu”alisema Majaliwa ambaye ameanza ziara ya siku nane mkoani Arusha.



Alisema ni muhimu kwa halmashauri kununua mabomba hayo kwa matumizi ya miradi ya maji na kuunga mkono juhudi zinazofanywa na wawekezaji wa ndani.



“Washauri wa miradi mbalimbali acheni chuki …waache wakandarasi wanunue bidhaa bora zilizothibitishwa na Shirika la Viwango la Taifa (TBS) na Shirika la Viwango la Kimataifa (ISO),” alisema.

Aidha alitoa mfano, kwa upande wa Mkoa wa Arusha kuna mpango wa kujenga mradi mkubwa wa maji utakaogharimu dola za Marekani milioni 200, na katika utekelezaji wake ni lazima watoe kipaumbele cha kutumia mabomba yanayozalishwa na kiwanda hicho.

Mradi huo ukikamilika unatarajiwa kumaliza kero ya maji kwa wakazi wa jijini hapa.

Alisisiza haoni umuhimu wa halmashauri na wakandarasi kununua mabomba kutoka nje ya Arusha au nje ya nchi wakati kuna mabomba yanayozalishwa na wawekezaji wazawa na yanakidhi viwango.

“Serikali yetu itaendelea kuwaenzi na kuwalinda wawekezaji wote wa ndani ambao wamekuwa msaada mkubwa wa kutoa ajira ambayo ni janga kwa taifa na dunia kwa ujumla”alisema Majaliwa.

Awali Mwenyekiti wa Bodi ya Lodhia Group, Arun Lodhia, alisema serikali ichukue nafasi ya kuzungumza na wenye viwanda mara kwa mara ili kujua matatizo yao na kuyatafutia ufumbuzi.

Alisema viwanda chini ya kampuni hiyo, vinazalisha bidhaa nyingi zenye ubora lakini makampuni yanashindwa kununua na kupenda zaidi kununua bidhaa za nje.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa kiwanda hicho, Sailesh Pandit, alisema kwamba wanashindwa kuuza mabomba ya maji na malighafi nyingine katika miradi mikubwa ya maji iliyopo mkoani Arusha.

Alisema wanashindwa kufanya hivyo licha ya bidhaa zao kuwa na TBS na ISO kutokana na hujuma wanazofanyiwa na baadhi ya wahandisi na washauri elekezi wa miradi.

“Imeshatokea mara kadhaa kwa wakandarasi wanaotekeleza miradi kuzuiwa kununua mabomba ya maji kutoka Lodhia Plastics na badala yake hulazimishwa kununua mabomba kutoka nje ya mkoa hivyo kuwasababishia gharama za ziada,” alisema.

Kuhusu ajira, alisema kiwanda hicho kimetoajiri Watanzania kati ya 1, 200 hadi 1, 300 lakini pia Watanzania zaidi ya 500 wananufaika kutokana na kushiriki katika utoaji wa huduma mbalimbali kiwandani hapo.

Alisema mtandao wa viwanda vinne vinavyomilikiwa na kampuni ya Lodhia Group wanalipa kodi wastani wa Sh. bilioni 20 kwa mwaka.

Kwa upande wao, baadhi ya makandarasi, Samuel Lugemalila wa Kampuni ya Vest Tanzania Ltd na Kastuli Mandange kutoka Fraju Group Ltd na Maxmilian Iranghay wa kampuni Wining Spirit Construction Ltd, walitoa ushuhuda kuhusu namna washauri waelekezi na watumishi wengine wanavyowakataza kununua bidhaa za Lodhia Plastics na kuwataka wanunue zinazotengenezwa nje ya mkoa.

Walisema kitendo hicho kinawashababisha kushindwa kukamilisha miradi yao kwa wakati na kuwaongezea gharama kubwa.
Aidha waliiomba serikali kuondoa urasimu kwa wahasibu kulipa malipo kwa wakati licha ya miradi kukaguliwa na kupata cheti cha uhakiki wa kazi.


 Mlimbwende anayeshikilia Taji la Urembo la Mkoa wa Dodoma (Miss Dodoma 2016/17), Anna Nitwa (wa pili kulia) akiwa na Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini ambaye pia ni Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira, Anthony Mavunde (wa pili kushoto) pamoja na madaktari wakati wakielekea kwenye Wodi ya Wazazi wanaojifungua Watoto kabla ya wakati (Njiti), katika Hospitali ya Mkoa wa Dodoma, Desemba 1, 2016.

Mrembo huyo ambaye aliguswa na hali aliyoikuta hapo awali wakati alipotembelea Wodi ya Wazazi wanaojifungua Watoto kabla ya wakati (Njiti) hasa pale alipoona mazingira ya choo cha kina Mama hao kuwa si ya kuridhisha kwa afya ya mama na Mtoto na ikizingatiwa kuwa watoto hao wanahitaji uangalizi wa hali ya juu, alijitolea kukikarabati Choo hicho na Desemba 1, 2016 alikikabidhi kwa uongozi wa Hospitali hiyo ya Mkoa wa Dodoma.

Akizungumza mbele ya wanahabari pamoja na uongozi wa Hospitali hiyo, Mrembo Anna Nitwa alisema "Siku ya Novemba 4, 2016 nilitembelea Wodi ya Watoto Njiti wakati wa kujiandaa na siku ya maadhimisho ya watoto wazaliwao kabla ya wakati ambayo ilikua Novemba 17, Niliona mazingira ya choo kilichokua kinatumiwa na Wazazi wa Watoto Njiti pamoja na wauguzi wao, hakikua katika hali nzuri. Hivyo niliahidi kushirikiana na washikadau mbalimbali ili kuweza kukarabati.

Aliendelea kusema kuwa "Wazazi wangu pamoja na watu wachache walioguswa waliweza kushirikiana nami kuchangia fedha za kukarabati choo hicho, na kazi ya ukarabati imekamilika na sasa nimekikabidhi.

Kwa Upande wa Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini ambaye pia ni Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira, Anthony Mavunde aliyeambatana na Mrembo huyo Hospitalini hapo, alimpongeza kwa kazi nzuri aliyoifanya na kumuahidi kuijenga korido ambayo itaunganisha Wodi hiyo na choo ili kuwasaidia wakina mama hao kuwa katika mazingira ya ulinzi hasa nyakati za usiku, kwani kwasasa choo hicho kipo kwa nje ya wodi hiyo, hivyo korido ikijengwa itawasaidia sana. 
Kwa upange wake Mganga Mkuu wa Hospitali ya Dodoma,Dkt. James Charles alitoa shukrani kwa Mrombo huyo kwa jitihada zake za kufanikisha ukarabati huo, na hasa kwa moyo wake wa kujitolea, na kuwaomba Watanzania wengine kujitolea kufanikisha mahitaji mengine Hospitalini hapo.
Mlimbwende anayeshikilia Taji la Urembo la Mkoa wa Dodoma (Miss Dodoma 2016/17), Anna Nitwa (kushoto) na Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini ambaye pia ni Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira, Anthony Mavunde (katikati) wakiwa katika Wodi ya Wazazi wanaojifungua Watoto kabla ya wakati (Njiti), katika Hospitali ya Mkoa wa Dodoma, Desemba 1, 2016.
Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini ambaye pia ni Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira, Anthony Mavunde akiangalia namna Choo hicho kilivyokarabatiwa kwa jitihada za Miss Dodoma 2016/17, Anna Nitwa.
Kinavyoonekana kwa ndani.
Mlimbwende anayeshikilia Taji la Urembo la Mkoa wa Dodoma (Miss Dodoma 2016/17), Anna Nitwa akiwa amewabeba watoto Mapacha, wakati alipotembelea Wodi ya Wazazi wanaojifungua Watoto kabla ya wakati (Njiti), katika Hospitali ya Mkoa wa Dodoma, Desemba 1, 2016.

 Mwalimu Tuhobwike Mwinuka Mwakatumbula enzi za uhai wake.

 Jeneza lenye mwili wa mwalimu Tuhobwike Mwinuka Mwakatumbula likiwa ndani ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Usharika wa Wazo Hili Dar es Salaam leo asubuhi wakati wa ibada ya kuuaga mwili huo.
 Mume wa marehemu, Samuel Mwakatumbula akimbusu mke wake wakati wa ibada hiyo ya kumuaga mpendwa wake. Kushoto ni mtoto wake Kelvin.
Binamu wa marehemu, Nobert Nselu (kulia) akimsaidia rafiki wa karibu wa marehemu mama Malugu wakati mwili wa marehemu ukiwasili nyumbani kwake.
 Rafiki wa marehemu mama Malugu (katikati) akisaidiwa.
 Waombolezaji wakiwa msibani nyumbani kwa marehemu 
Wazo Hill.

 Ni huzuni kubwa 
 Wakina mama wakiwa na maua wakati wakisubiri mwili wa marehemu kuingizwa ndani.
 Geneza lenye mwili wa marehemu likiingizwa nyumbani kwake. 

 Mume wa marehemu Samuel Mwakatumbula akimuaga mke wake
 Mtoto mkubwa wa marehemu Nico Mwakatumbula (katikati), akisaidiwa baada ya kutoa heshima za mwisho kwa mama yake.
 Waombolezaji wakiingiza jeneza lenye mwili wa marehemu katika Kanisa la KKKT Usharika wa Wazo Hill.
 Mwili ukiwa kanisani.
 Mume wa marehemu akiwa na watoto wake. Kutoka kulia ni Gloria, Kelvin na Nico.
 Wanafamilia wakiwa katika ibada hiyo ya kumuaga mpendwa wao.
 Waumini wa kanisa hilo wakiwa kwenye ibada hiyo.N a Dotto Mwaibale

MWALIMU Tuhobwike Mwinuka Mwakatumbula wa Shule ya Msingi Kumbukumbu katika Manispaa ya Kinondoni amefariki dunia wakati akiwa katika mkutano wa Chama Cha Walimu Tanzania (CWT) na viongozi wa Idara ya Elimu wa manispaa hiyo.

Kifo cha mwalimu huyo kimetokea Desemba 1, 2016 Siku ya Ijumaa majira ya jioni wakati viongozi hao walipokuwa wakimalizia ziara yao ya kutembelea shule mbalimbali katika manispaa hiyo.

Akizungumza na Jambo Leo mume wa marehemu Samuel Mwakatumbula alisema mke wake hakuwa na tatitizo lolote la kiafya na siku ya tukio hilo aliamka salama na kumuaga kuwa anawahi kwenye mkutano huo.

"Siku chache kabla ya kifo chake mke wangu aliniambia alikuwa hajisikii vizuri kwani alikuwa na uchovu wa kawaida" alisema Mwakatumbula.

Mwakatumbula alisema alipigiwa siku na kuambiwa kuwa mke wake alianguka ghafla wakati mkutano ukiendelea na kupoteza fahamu ambapo alikimbizwa Hospitali ya Mount Mkombozi iliyopo maeneo ya Morocco ambapo waliambiwa tayari alikuwa amefariki.

Mwili wa marehemu ulisafirishwa jana kwenda Kiwira wilayani Rungwe mkoani Mbeya kwa maziko yatakayofanyika leo marehemu ameacha mume na watoto watatu, Nico, Kelvin na Gloria.

 Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme nchini Tanzania, (TANESCO), Mhandisi Felchesmi Mramba, (aliyenyoosha kidole), akifafanua jambo wakati wahariri na waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari walipotembelea kituo cha kupoza na kusambaza umeme cha Ilala-Mchikichini jijini Dar es Salaam, wakati wa ziara ya wahariri kutembelea miradi ya ukarabati wa miundombinu ya usambazaji umeme jijini Dar es Salaam, Desemba 3, 2016.
Mhandisi Mramba akiwa na wahariri na waandishi kwenye kituo cha kupoza na kusambaza umeme cha City Centre

NA K-VIS BLOG/KHALFAN SAID
WAHARIRI wa vyombo vya habari nchini, wametembelea miradi ya ukarabati wa miundombinu ya usambazaji umeme jijini Dar es Salaam leo Desemba 3, 2016, ili kujionea hatua zinazochukuliwa na shirika hilo katika kuboresha hali ya upatikanaji umeme jijini.
Akiongea wakati wa ziara hiyo ambayo iliwawezesha wahariri hao kutembelea vituo vya kupoza na kusambaza umeme vya Muhimbili, kituo kipya cha City Centre, kituo cha Sokoine Drive, kituo cha Ilala Mchikichini na kituo cha kuratibu na kudhibiti mifumo ya umeme jijini kilichoko Mikocheni.
“Dhana ya kujenga uchumi wa viwanda ni dhana inayotekelezeka na ushahidi wa wazi ni kiasi cha uwekezaji uliowekwa na serikali kwenye sekta ya umeme,” alisema Mhandisi Mramba.
Alisema hivi miradi hiyo ya kuboresha miundombinu ya umeme jijini Dar es Salaam inayotekelezwa na Serikali kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo imehusisha ufungaji wa vifaa vipya kabisa.
“Tumeona kituo hiki cha Ilala, upanuzi mkubwa unafanyika hapa kwa ushirikiano na serikali ya Japan, City centre kinatekelezwa kwa ushirikiano na serikali ya Japan na Finland, kituo cha Sokoine kwa ushirikiano na African Development Bank, kituo kipya cha Muhimbili kwa ajili ya kutoa huduma kwenye hospitali ya taifa Muhimbili, Taasisi ya Moi na Taasisi ya Jakaya Kikwete, pamoja na chuo kikuu cha Muhimbil Kituo cha kudhibiti mifumo ya umeme cha Mikocheni kinachosimamia mifumo yote ya umeme kwa jumla ukilinganisha  vituo vyote vya distribution, (usambazaji), ukaunganisha na vituo vya uzalishaji umeme kama vile Kinyerezi I na II, ukaunganisha na vituo vya transmission (kusafirisha) Backborne, Makambako-Songea na miradi mingine mingi, vitafanya nchi yetu iweze kupata umeme wa kutosha.” Alifafanua.
Mhandisi Mramba pia aliwaambia wahariri hao kuwa agizo alilolitoa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Kikwete, wa kupeleka umeme kwenye kiwanda cha Bakhresa kilichoko Mwandege tayari umeme umeshafika.
Mhandisi Mramba amesema, kwa sasa TANESCO inatekeleza miradi mbalimbali ya umeme kote nchini ili kuhakikisha taifa linapata umeme wa uhakika na ulio bora.
Miradi hii ya Dar es Salaam, itakamilika ifikapo Aprili mwakani, alisema Mhandisi Mramba.
Akielezea lengo la ziara hiyo, Kaimu Meneja Uhusiano wa TANESCO, Leila Muhaji alisema, ni kuwawezesha wahariri kuona na kuwafahamisha wananchi jinsi serikali ilivyofanya uwekezaji mkubwa wa katika sekta ya umeme. “Mnaweza kuona kwamba umeme unaopatikana sasahivi ni bora zaidi ukilinganisha na ule uliokuwa ukipatikana miaka michache ya nyuma,” Alisema.
Aidha Mhandisi Mramba alisema miradi ya TANESCO inayotekelezwa hivi sasa nchi nzima ina thamani ya zaidi ya shilingi Trilioni 5 za kitanzania.

 Meneja Mwandamizi wa Usambazaji Umeme wa Shirika la Umeme Tanzania, (TANESCO), ambaye pia ndiye Meneja wa  Mradi wa kuimarisha miundombinu ya Umeme, Injinia Theodory Bayona, (kulia), akielezea hatua iliyofikiwa hadi sasa ya uboreshaji miundombinu ya umeme jijini Dar es Salaam
Meneja Mwandamizi wa Shirika hilo kanda ya Dar es Salaam na Pwani Mhandisi, Mahende Mgaya.
Meneja Mwandamizi wa Miradi ya Usafirishaji na Usambazaji Umeme wa Shirika hilo, Mhandisi Gregory Chegere


Kituo cha City Centre.
 Mhandisi Mramba akiwa na wahariri na waandishi wa habari kwenye gari wakati wa ziara hiyo
Mhandisi Mramba, akifafanua jambo wakati wahariri na waandishi walipotembelea kituo cha City Centre.

No comments :

Post a Comment