Mwenyekiti wa Kampuni ya Lodhia Group Bw. Arun Lodhia akimpokea Waziri
Mkuu wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa
ili kuzindua kiwanda cha Lodhia Plastic kinachotengeneza Mabomba ya Maji
,kilichopo Njiro jijini Arusha Leo, 3 Disemba 2016.
Mwenyekiti
wa Kampuni ya Lodhia Group Bw. Arun Lodhia akitoa maelezo kwa Waziri Mkuu wa
Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa wakati alipofika
kuzindua kiwanda cha Lodhia Plastic kinachotengeneza Mabomba ya Maji
,kilichopo Njiro jijini Arusha Leo, 3 Disemba 2016.
Mwenyekiti
wa Kampuni ya Lodhia Group Bw. Arun Lodhia (wa kwanza kushoto
waliokaa) akiteta jambo na Waziri Mkuu wa
Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa
akifuatiwa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo na Naibu waziri
wa kilimo ,Mifugo na Uvuvi Mhe. William Ole Nasha wakati walipofika
kuzindua kiwanda cha Lodhia Plastic kinachotengeneza Mabomba ya Maji
,kilichopo Njiro jijini Arusha Leo, 3 Disemba 2016.
Waziri
Mkuu wa
Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa akikata
utepe tayari kwa uzinduzi wa kiwanda cha Lodhia Plastic
kinachotengeneza Mabomba ya Maji ,kilichopo Njiro jijini Arusha Leo, 3
Disemba 2016.
Kutoka Kushoto (mwenye suti bluu) ni Mkurugenzi Mtendaji
wa Kampuni ya Lodhia Group Bw. Sailesh Pandit, Mwenyekiti wa kampuni
ya Lodhia Group Bw. Arun Lodhia wakiongozana na Waziri Mkuu wa
Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa ndani ya
kiwanda cha Lodhia Plastic kinachotengeneza Mabomba ya Maji ,kilichopo
Njiro jijini Arusha Leo, 3 Disemba 2016.
Waziri
Mkuu wa
Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa akisaini
kitabu cha wageni mara baada ya kuzindua kiwanda cha Lodhia Plastic
kinachotengeneza Mabomba ya Maji ,kilichopo Njiro jijini Arusha Leo, 3
Disemba 2016.
Mwenyekiti
wa Kampuni ya Lodhia Group Bw. Arun Lodhia akimkaribisha Waziri Mkuu wa
Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa ili kuongea na hadhara iliyopo kwenye kiwanda hicho mara baada ya
kuzindua kiwanda kinachotengeneza Mabomba ya Maji ,kilichopo Njiro jijini Arusha Leo, 3 Disemba 2016.
Waziri Mkuu wa
Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa akiongea machache mara baada ya
kuzindua kiwanda cha Lodhia Plastic kinachotengeneza Mabomba ya Maji ,kilichopo Njiro jijini Arusha Leo, 3 Disemba 2016.
Waziri Mkuu wa
Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa akizindua
jiwe la msingi katika kiwanda cha Lodhia Plastic kinachotengeneza
Mabomba ya Maji ,kilichopo Njiro jijini Arusha Leo, 3 Disemba 2016.
Mkurugenzi Mtendaji
wa Kampuni ya Lodhia Group Bw. Sailesh Pandit akiagana na Waziri Mkuu wa
Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa mara baada ya
kuzindua kiwanda cha Lodhia Plastic kinachotengeneza Mabomba ya Maji ,kilichopo
Njiro jijini Arusha Leo, 3 Disemba 2016.
Mwenyekiti wa kampuni
ya Lodhia Group Bw. Arun Lodhia akiagana na Waziri Mkuu wa
Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa mara baada ya
kuzindua kiwanda cha Lodhia Plastic kinachotengeneza Mabomba ya Maji ,kilichopo
Njiro jijini Arusha Leo, 3 Disemba 2016.
Mkurugenzi Mtendaji
wa Kampuni ya Lodhia Group Bw. Sailesh Pandit akisoma risala mbele ya Mgeni rasmi ambaye niWaziri Mkuu wa
Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa ndani ya
kiwanda cha Lodhia Plastic kinachotengeneza Mabomba ya Maji ,kilichopo
Njiro jijini Arusha Leo, 3 Disemba 2016. Picha zote Gadiola Emanuel
habari na Woinde Shizza , Arusha.
Halmashauri za majiji, manispaa na miji
wametakiwa kutumia mabomba ya maji yanayozalishwa nchini badala ya kuagiza
bidhaa hiyo toka nje ili kuweza kuvinufaisha
viwanda vya ndani.
Hayo
yamebainishwa na waziri mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim
Majaliwa
wakati akizindua kiwanda cha kutengeneza mabomba ya Plastic ya maji
yenye ukubwa wa aina mbalimbali (Lodhia Plastics ) kilichopo njiro
jijini
hapa.
Alisema
kuwa haiana haja ya halmashauri au
majiji kuagiza bidhaa mbalimbali nje ya nchi
wakati nchi yetu inaviwanda vya
kutosha vya kutengeneza bidhaa hizo.
“Sioni
sababu ya wahandisi wa Halmashauri na washauri elekezi halmashauri kushinikiza
wakandarasi wa hapa Arusha kwenda kununua mabomba ya maji nje ya mkoa wakati
hapa kuna kiwanda kama Lodhia ambacho kinatengeneza hizo bidhaa kwakweli hii
labda iwe ni chuki tu”alisema Majaliwa ambaye ameanza
ziara ya siku nane mkoani Arusha.
Alisema
ni muhimu kwa halmashauri kununua mabomba hayo kwa matumizi ya miradi ya maji
na kuunga mkono juhudi zinazofanywa na wawekezaji wa ndani.
“Washauri
wa miradi mbalimbali acheni chuki …waache wakandarasi wanunue bidhaa bora
zilizothibitishwa na Shirika la Viwango la Taifa (TBS) na Shirika la Viwango la
Kimataifa (ISO),” alisema.
Aidha
alitoa mfano, kwa upande wa Mkoa wa Arusha kuna mpango wa kujenga mradi mkubwa
wa maji utakaogharimu dola za Marekani milioni 200, na katika utekelezaji wake
ni lazima watoe kipaumbele cha kutumia mabomba yanayozalishwa na kiwanda hicho.
Mradi
huo ukikamilika unatarajiwa kumaliza kero ya maji kwa wakazi wa jijini hapa.
Alisisiza
haoni umuhimu wa halmashauri na wakandarasi kununua mabomba kutoka nje ya
Arusha au nje ya nchi wakati kuna mabomba yanayozalishwa na wawekezaji wazawa
na yanakidhi viwango.
“Serikali
yetu itaendelea kuwaenzi na kuwalinda
wawekezaji wote wa ndani ambao wamekuwa msaada mkubwa wa kutoa ajira ambayo ni
janga kwa taifa na dunia kwa ujumla”alisema Majaliwa.
Awali
Mwenyekiti wa Bodi ya Lodhia Group, Arun Lodhia, alisema serikali ichukue
nafasi ya kuzungumza na wenye viwanda mara kwa mara ili kujua matatizo yao na
kuyatafutia ufumbuzi.
Alisema
viwanda chini ya kampuni hiyo, vinazalisha bidhaa nyingi zenye ubora lakini
makampuni yanashindwa kununua na kupenda zaidi kununua bidhaa za nje.
Kwa
upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa kiwanda hicho, Sailesh Pandit, alisema kwamba wanashindwa kuuza mabomba ya maji na
malighafi nyingine katika miradi mikubwa ya maji iliyopo mkoani Arusha.
Alisema
wanashindwa kufanya hivyo licha ya bidhaa zao kuwa na TBS na ISO kutokana na
hujuma wanazofanyiwa na baadhi ya wahandisi na washauri elekezi wa miradi.
“Imeshatokea
mara kadhaa kwa wakandarasi wanaotekeleza miradi kuzuiwa kununua mabomba ya
maji kutoka Lodhia Plastics na badala yake hulazimishwa kununua mabomba kutoka
nje ya mkoa hivyo kuwasababishia gharama za ziada,” alisema.
Kuhusu
ajira, alisema kiwanda hicho kimetoajiri Watanzania kati ya 1, 200 hadi 1, 300 lakini
pia Watanzania zaidi ya 500 wananufaika kutokana na kushiriki katika utoaji wa
huduma mbalimbali kiwandani hapo.
Alisema
mtandao wa viwanda vinne vinavyomilikiwa na kampuni ya Lodhia Group wanalipa kodi
wastani wa Sh. bilioni 20 kwa mwaka.
Kwa
upande wao, baadhi ya makandarasi, Samuel Lugemalila wa Kampuni ya Vest
Tanzania Ltd na Kastuli Mandange kutoka Fraju Group Ltd na Maxmilian Iranghay wa kampuni Wining Spirit Construction Ltd,
walitoa ushuhuda kuhusu namna washauri waelekezi na watumishi wengine
wanavyowakataza kununua bidhaa za Lodhia Plastics na kuwataka wanunue
zinazotengenezwa nje ya mkoa.
Walisema
kitendo hicho kinawashababisha kushindwa kukamilisha miradi yao kwa wakati na
kuwaongezea gharama kubwa.
Aidha
waliiomba serikali kuondoa urasimu kwa wahasibu kulipa malipo kwa wakati licha
ya miradi kukaguliwa na kupata cheti cha uhakiki wa kazi.
Mlimbwende
anayeshikilia Taji la Urembo la Mkoa wa Dodoma (Miss Dodoma 2016/17),
Anna Nitwa (wa pili kulia) akiwa na Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini
ambaye pia ni Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira,
Anthony Mavunde (wa pili kushoto) pamoja na madaktari wakati wakielekea
kwenye Wodi ya Wazazi wanaojifungua Watoto kabla ya wakati (Njiti),
katika Hospitali ya Mkoa wa Dodoma, Desemba 1, 2016.
Mrembo
huyo ambaye aliguswa na hali aliyoikuta hapo awali wakati alipotembelea
Wodi ya Wazazi wanaojifungua Watoto kabla ya wakati (Njiti) hasa pale
alipoona mazingira ya choo cha kina Mama hao kuwa si ya kuridhisha kwa
afya ya mama na Mtoto na ikizingatiwa kuwa watoto hao wanahitaji
uangalizi wa hali ya juu, alijitolea kukikarabati Choo hicho na Desemba
1, 2016 alikikabidhi kwa uongozi wa Hospitali hiyo ya Mkoa wa Dodoma.
Akizungumza
mbele ya wanahabari pamoja na uongozi wa Hospitali hiyo, Mrembo Anna
Nitwa alisema "Siku ya Novemba 4, 2016 nilitembelea Wodi ya Watoto Njiti
wakati wa kujiandaa na siku ya maadhimisho ya watoto wazaliwao kabla ya
wakati ambayo ilikua Novemba 17, Niliona mazingira ya choo kilichokua
kinatumiwa na Wazazi wa Watoto Njiti pamoja na wauguzi wao, hakikua
katika hali nzuri. Hivyo niliahidi kushirikiana na washikadau mbalimbali
ili kuweza kukarabati.
Aliendelea
kusema kuwa "Wazazi wangu pamoja na watu wachache walioguswa waliweza
kushirikiana nami kuchangia fedha za kukarabati choo hicho, na kazi ya
ukarabati imekamilika na sasa nimekikabidhi.
Kwa
Upande wa Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini ambaye pia ni Naibu Waziri,
Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira, Anthony Mavunde
aliyeambatana na Mrembo huyo Hospitalini hapo, alimpongeza kwa kazi
nzuri aliyoifanya na kumuahidi kuijenga korido ambayo itaunganisha Wodi
hiyo na choo ili kuwasaidia wakina mama hao kuwa katika mazingira ya
ulinzi hasa nyakati za usiku, kwani kwasasa choo hicho kipo kwa nje ya
wodi hiyo, hivyo korido ikijengwa itawasaidia sana.
Kwa
upange wake Mganga Mkuu wa Hospitali ya Dodoma,Dkt. James Charles
alitoa shukrani kwa Mrombo huyo kwa jitihada zake za kufanikisha
ukarabati huo, na hasa kwa moyo wake wa kujitolea, na kuwaomba
Watanzania wengine kujitolea kufanikisha mahitaji mengine Hospitalini
hapo.
Mlimbwende
anayeshikilia Taji la Urembo la Mkoa wa Dodoma (Miss Dodoma
2016/17), Anna Nitwa (kushoto) na Mbunge wa Jimbo la Dodoma
Mjini ambaye pia ni Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na
Ajira, Anthony Mavunde (katikati) wakiwa katika Wodi ya Wazazi
wanaojifungua Watoto kabla ya wakati (Njiti), katika Hospitali ya Mkoa
wa Dodoma, Desemba 1, 2016.
Mbunge wa Jimbo la Dodoma
Mjini ambaye pia ni Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na
Ajira, Anthony Mavunde akiangalia namna Choo hicho kilivyokarabatiwa kwa jitihada za Miss Dodoma
2016/17, Anna Nitwa.
Kinavyoonekana kwa ndani.
Mlimbwende
anayeshikilia Taji la Urembo la Mkoa wa Dodoma (Miss Dodoma
2016/17), Anna Nitwa akiwa amewabeba watoto Mapacha, wakati
alipotembelea Wodi ya Wazazi wanaojifungua Watoto kabla ya wakati
(Njiti), katika Hospitali ya Mkoa wa Dodoma, Desemba 1, 2016.
Mwalimu Tuhobwike Mwinuka Mwakatumbula enzi za uhai wake.
Jeneza lenye mwili wa mwalimu Tuhobwike
Mwinuka Mwakatumbula likiwa ndani ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri
Tanzania (KKKT), Usharika wa Wazo Hili Dar es Salaam leo asubuhi wakati
wa ibada ya kuuaga mwili huo.
Mume wa marehemu, Samuel Mwakatumbula
akimbusu mke wake wakati wa ibada hiyo ya kumuaga mpendwa wake. Kushoto
ni mtoto wake Kelvin.
Binamu wa marehemu, Nobert Nselu (kulia)
akimsaidia rafiki wa karibu wa marehemu mama Malugu wakati mwili wa
marehemu ukiwasili nyumbani kwake.
Rafiki wa marehemu mama Malugu (katikati) akisaidiwa.
Waombolezaji wakiwa msibani nyumbani kwa marehemu
Wazo Hill.
Ni huzuni kubwa
Wakina mama wakiwa na maua wakati wakisubiri mwili wa marehemu kuingizwa ndani.
Geneza lenye mwili wa marehemu likiingizwa nyumbani kwake.
Mume wa marehemu Samuel Mwakatumbula akimuaga mke wake
Mtoto mkubwa wa marehemu Nico Mwakatumbula (katikati), akisaidiwa baada ya kutoa heshima za mwisho kwa mama yake.
Waombolezaji wakiingiza jeneza lenye mwili wa marehemu katika Kanisa la KKKT Usharika wa Wazo Hill.
Mwili ukiwa kanisani.
Mume wa marehemu akiwa na watoto wake. Kutoka kulia ni Gloria, Kelvin na Nico.
Wanafamilia wakiwa katika ibada hiyo ya kumuaga mpendwa wao.
Waumini wa kanisa hilo wakiwa kwenye ibada hiyo.N a Dotto Mwaibale
MWALIMU Tuhobwike Mwinuka Mwakatumbula
wa Shule ya Msingi Kumbukumbu katika Manispaa ya Kinondoni amefariki
dunia wakati akiwa katika mkutano wa Chama Cha Walimu Tanzania (CWT) na
viongozi wa Idara ya Elimu wa manispaa hiyo.
Kifo cha mwalimu huyo kimetokea Desemba
1, 2016 Siku ya Ijumaa majira ya jioni wakati viongozi hao walipokuwa
wakimalizia ziara yao ya kutembelea shule mbalimbali katika manispaa
hiyo.
Akizungumza na Jambo Leo mume wa
marehemu Samuel Mwakatumbula alisema mke wake hakuwa na tatitizo lolote
la kiafya na siku ya tukio hilo aliamka salama na kumuaga kuwa anawahi
kwenye mkutano huo.
"Siku chache kabla ya kifo chake mke
wangu aliniambia alikuwa hajisikii vizuri kwani alikuwa na uchovu wa
kawaida" alisema Mwakatumbula.
Mwakatumbula alisema alipigiwa siku na
kuambiwa kuwa mke wake alianguka ghafla wakati mkutano ukiendelea na
kupoteza fahamu ambapo alikimbizwa Hospitali ya Mount Mkombozi iliyopo
maeneo ya Morocco ambapo waliambiwa tayari alikuwa amefariki.
Mwili wa marehemu ulisafirishwa jana
kwenda Kiwira wilayani Rungwe mkoani Mbeya kwa maziko yatakayofanyika
leo marehemu ameacha mume na watoto watatu, Nico, Kelvin na Gloria.
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme
nchini Tanzania, (TANESCO), Mhandisi Felchesmi Mramba, (aliyenyoosha
kidole), akifafanua jambo wakati wahariri na waandishi wa habari kutoka
vyombo mbalimbali vya habari walipotembelea kituo cha kupoza na
kusambaza umeme cha Ilala-Mchikichini jijini Dar es Salaam, wakati wa
ziara ya wahariri kutembelea miradi ya ukarabati wa miundombinu ya
usambazaji umeme jijini Dar es Salaam, Desemba 3, 2016.
Mhandisi Mramba akiwa na wahariri na waandishi kwenye kituo cha kupoza na kusambaza umeme cha City Centre
NA
K-VIS BLOG/KHALFAN SAID
WAHARIRI
wa vyombo vya habari nchini, wametembelea miradi ya ukarabati wa miundombinu ya
usambazaji umeme jijini Dar es Salaam leo Desemba 3, 2016, ili kujionea hatua
zinazochukuliwa na shirika hilo katika kuboresha hali ya upatikanaji umeme
jijini.
Akiongea
wakati wa ziara hiyo ambayo iliwawezesha wahariri hao kutembelea vituo vya
kupoza na kusambaza umeme vya Muhimbili, kituo kipya cha City Centre, kituo cha
Sokoine Drive, kituo cha Ilala Mchikichini na kituo cha kuratibu na kudhibiti
mifumo ya umeme jijini kilichoko Mikocheni.
“Dhana
ya kujenga uchumi wa viwanda ni dhana inayotekelezeka na ushahidi wa wazi ni
kiasi cha uwekezaji uliowekwa na serikali kwenye sekta ya umeme,” alisema
Mhandisi Mramba.
Alisema
hivi miradi hiyo ya kuboresha miundombinu ya umeme jijini Dar es Salaam
inayotekelezwa na Serikali kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo imehusisha
ufungaji wa vifaa vipya kabisa.
“Tumeona
kituo hiki cha Ilala, upanuzi mkubwa unafanyika hapa kwa ushirikiano na
serikali ya Japan, City centre kinatekelezwa kwa ushirikiano na serikali ya Japan
na Finland, kituo cha Sokoine kwa ushirikiano na African Development Bank,
kituo kipya cha Muhimbili kwa ajili ya kutoa huduma kwenye hospitali ya taifa
Muhimbili, Taasisi ya Moi na Taasisi ya Jakaya Kikwete, pamoja na chuo kikuu
cha Muhimbil Kituo cha kudhibiti mifumo ya umeme cha Mikocheni kinachosimamia
mifumo yote ya umeme kwa jumla ukilinganisha
vituo vyote vya distribution, (usambazaji), ukaunganisha na vituo vya
uzalishaji umeme kama vile Kinyerezi I na II, ukaunganisha na vituo vya transmission
(kusafirisha) Backborne, Makambako-Songea na miradi mingine mingi, vitafanya
nchi yetu iweze kupata umeme wa kutosha.” Alifafanua.
Mhandisi
Mramba pia aliwaambia wahariri hao kuwa agizo alilolitoa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Kikwete, wa kupeleka umeme kwenye kiwanda cha
Bakhresa kilichoko Mwandege tayari umeme umeshafika.
Mhandisi
Mramba amesema, kwa sasa TANESCO inatekeleza miradi mbalimbali ya umeme kote
nchini ili kuhakikisha taifa linapata umeme wa uhakika na ulio bora.
Miradi
hii ya Dar es Salaam, itakamilika ifikapo Aprili mwakani, alisema Mhandisi
Mramba.
Akielezea
lengo la ziara hiyo, Kaimu Meneja Uhusiano wa TANESCO, Leila Muhaji alisema, ni
kuwawezesha wahariri kuona na kuwafahamisha wananchi jinsi serikali ilivyofanya
uwekezaji mkubwa wa katika sekta ya umeme. “Mnaweza kuona kwamba umeme
unaopatikana sasahivi ni bora zaidi ukilinganisha na ule uliokuwa ukipatikana
miaka michache ya nyuma,” Alisema.
Aidha
Mhandisi Mramba alisema miradi ya TANESCO inayotekelezwa hivi sasa nchi nzima
ina thamani ya zaidi ya shilingi Trilioni 5 za kitanzania.
Meneja
Mwandamizi wa Usambazaji Umeme wa Shirika la
Umeme Tanzania, (TANESCO), ambaye pia ndiye Meneja wa Mradi wa
kuimarisha
miundombinu ya Umeme, Injinia Theodory Bayona, (kulia), akielezea hatua iliyofikiwa
hadi sasa ya uboreshaji miundombinu ya umeme jijini Dar es Salaam
Meneja
Mwandamizi wa Shirika hilo kanda ya Dar es Salaam na Pwani Mhandisi, Mahende
Mgaya.
Meneja
Mwandamizi wa Miradi ya Usafirishaji na Usambazaji Umeme wa Shirika hilo,
Mhandisi Gregory Chegere
Kituo cha City Centre.
Mhandisi Mramba akiwa na wahariri na waandishi wa habari kwenye gari wakati wa ziara hiyo
Mhandisi Mramba, akifafanua jambo wakati wahariri na waandishi walipotembelea kituo cha City Centre.
No comments:
Post a Comment