Thursday, November 3, 2016

ZANTEL YAZIDI KUSOGEZA HUDUMA KARIBU KWA WATEJA WAKE

zal1
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Zantel, Benoit Janin (kushoto), akisalimiana  na mkazi wa Bugururuni, Awadh Selemani,  Dar es Salaam jana, katika moja ya kampeni za masoko katika kufikisha huduma na bidhaa zao karibu kwa wateja. Zantel imemaliza hivi karibuni ukarabati mkubwa wa mtandao wake wa 3G na 4G wenye lengo la kuboresha ubora wa huduma za intaneti na sauti hivyo kupatikana kwa  zaidi za asimilia 85 ya Tanzania. 
zal2
Mkuu wa Mauzo wa Zantel, Herbert Louis (kushoto) na baadhi ya wafanyakazi wa timu ya mauzo, wakizungumza na baadhi ya wakazi wa  Bugururu,  Dar es Salaam, katika moja ya kampeni za masoko kufikisha huduma na bidhaa zao karibu kwa wateja. Zantel imemaliza hivi karibuni ukarabati mkubwa wa mtandao wake wa 3G na 4G wenye lengo la kuboresha ubora wa huduma za intaneti na sauti hivyo kupatikana zaidi za asimilia 85 ya Tanzania. 
zal3
Mkuu wa Masoko wa Zantel, Gasper Mbowa (katikati) na Naibu Ofisa Mtendaji Mkuu wa kampuni hiyo, Zadok Prescott (kulia), wakiwafahamisha wafanyabiashara wa soko la Kariakoo, Dar es Salaam, Yassin Hassani (kushoto) na Abdallah Issa, baadhi ya huduma za kampuni hiyo  katika moja ya kampeni za masoko kufikisha huduma  zao karibu na wateja. Zantel imemaliza hivi karibuni ukarabati mkubwa wa mtandao wake wa 3G na 4G wenye lengo la kuboresha ubora wa huduma za intaneti na sauti hivyo kupatikana zaidi za asimilia 85 ya Tanzania. 
zal4
Mkuu wa Mauzo wa Zantel, Herbert Louis (kushoto) akizungumza na baadhi ya wapiti njia katika mtaa wa Kongo,  Dar es Salaam jana, katika moja ya kampeni za masoko kufikisha huduma na bidhaa zao karibu kwa wateja. Zantel imemaliza hivi karibuni ukarabati mkubwa wa mtandao wake wa 3G na 4G wenye lengo la kuboresha ubora wa huduma za intaneti na sauti hivyo kupatikana zaidi za asimilia 85 ya Tanzania. 
zal5
Maofisa wa Zantel wakizungumza na wachuuzi wa matunda karibu ya soko la buguruni, Dar es Salaam, katika moja ya kampeni za masoko kufikisha huduma na bidhaa zao karibu kwa wateja. Zantel imemaliza hivi karibuni ukarabati mkubwa wa mtandao wake wa 3G na 4G wenye lengo la kuboresha ubora wa huduma za intaneti na sauti hivyo kupatikana zaidi za asimilia 85 ya Tanzania.  Kutoka kushoto ni, Mkuu wa Masoko, Gasper Mboya, Ofisa Mtendaji Mkuu, Benoit Janin na Mkuu wa Mauzo, Herbert Louis.
zal6
Maofisa wa ngazi ya juu wa  Zantel wakibadilishana mawazo karibu na soko la Buguruni, Dar es Salaam walipokwenda pamoja na timu ya mauzo kuzungumza na wateja na wakazi wa maeneo hayo kuhusu huduma za Zantel na jjnsi ilivyojipanga upya kuwaletea huduma bora. Kutoka kushoto; Ofisa Mtendaji Mkuu, Benoit Janin, Kaimu CEO, Zadok Prescott,  Mkuu wa Masoko, Gasper Mboya na Mkuu wa Mauzo, Herbert Louis. 

TAARIFA YA JESHI LA POLISI KWA VYOMBO VYA HABARI


adverapolice
Jeshi la Polisi nchini, katika kuhakikisha usalama wa raia na mali zao unaimarika, limeendelea na operesheni za kukamata wahalifu wa makosa mbalimbali yakiwemo makosa ya usalama barabarani katika mikoa yote ili kudhibiti vitendo vya uhalifu  na wahalifu. Katika operesheni hizo, Jeshi la Polisi limefanikiwa kukamata silaha na katika baadhi ya mikoa, wananchi wameweza kusalimisha silaha kwa hiari katika vituo vya Polisi.
Operesheni hizi ni endelevu,  na ili tuweze kufanikiwa zaidi katika kudhibiti uhalifu na wahalifu  hususani katika kipindi hiki tunapoelekea mwisho wa mwaka, wananchi  wanatakiwa kuwa makini na kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu haraka kwa kutumia namba za bure 111 na 112 pindi wanapowatilia shaka watu wasiowajua katika maeneo yao ili hatua za haraka ziweze kuchukuliwa.
Kwa wamiliki wa maduka makubwa, hoteli na maduka ya kufanyia miamala ya fedha kwa njia ya simu waangalie namna ya kuweka vifaa maalumu vyenye uwezo wa kurekodi mienendo ya watu wanaoingia na kutoka  ama kufuata huduma katika maeneo yao ya biashara.
Pia, wananchi katika makazi yao waimarishe ulinzi kwa kutumia mpango wa ulinzi jirani kwa kuhakikisha wanakuwa na utaratibu wa kubadilishana taarifa za hali ya usalama  ili kuhakikisha mitaa yao inakuwa salama wakati wote.
Aidha,  Jeshi la Polisi nchini linawataka madereva wa vyombo vya moto kuheshimu na kutii sheria za usalama barabarani ili kuepusha ajali na kuokoa maisha ya abiria na watumiaji wengine wa barabara. Jeshi la polisi nchini, litaendelea kutekeleza majukumu yake kwa mujibu wa sheria, bila woga ama upendeleo katika kuhakikisha usalama wa raia na mali zao unaimarika.
Imetolewa na:
          Advera John Bulimba – Kamishina Msaidizi wa Polisi (ACP)
Msemaji wa Jeshi la Polisi,
Makao Makuu ya Polisi.

No comments :

Post a Comment