Ofisa Mtendaji Mkuu wa Zantel,
Benoit Janin (kushoto), akisalimiana na mkazi wa Bugururuni, Awadh
Selemani, Dar es Salaam jana, katika moja ya kampeni za masoko katika
kufikisha huduma na bidhaa zao karibu kwa wateja. Zantel imemaliza hivi
karibuni ukarabati mkubwa wa mtandao wake wa 3G na 4G wenye lengo la
kuboresha ubora wa huduma za intaneti na sauti hivyo kupatikana kwa
zaidi za asimilia 85 ya Tanzania.
Mkuu wa Mauzo wa Zantel, Herbert
Louis (kushoto) na baadhi ya wafanyakazi wa timu ya mauzo, wakizungumza
na baadhi ya wakazi wa Bugururu, Dar es Salaam, katika moja ya kampeni
za masoko kufikisha huduma na bidhaa zao karibu kwa wateja. Zantel
imemaliza hivi karibuni ukarabati mkubwa wa mtandao wake wa 3G na 4G
wenye lengo la kuboresha ubora wa huduma za intaneti na sauti hivyo
kupatikana zaidi za asimilia 85 ya Tanzania.
Mkuu wa Masoko wa Zantel, Gasper
Mbowa (katikati) na Naibu Ofisa Mtendaji Mkuu wa kampuni hiyo, Zadok
Prescott (kulia), wakiwafahamisha wafanyabiashara wa soko la Kariakoo,
Dar es Salaam, Yassin Hassani (kushoto) na Abdallah Issa, baadhi ya
huduma za kampuni hiyo katika moja ya kampeni za masoko kufikisha
huduma zao karibu na wateja. Zantel imemaliza hivi karibuni ukarabati
mkubwa wa mtandao wake wa 3G na 4G wenye lengo la kuboresha ubora wa
huduma za intaneti na sauti hivyo kupatikana zaidi za asimilia 85 ya
Tanzania.
Mkuu wa Mauzo wa Zantel, Herbert
Louis (kushoto) akizungumza na baadhi ya wapiti njia katika mtaa wa
Kongo, Dar es Salaam jana, katika moja ya kampeni za masoko kufikisha
huduma na bidhaa zao karibu kwa wateja. Zantel imemaliza hivi karibuni
ukarabati mkubwa wa mtandao wake wa 3G na 4G wenye lengo la kuboresha
ubora wa huduma za intaneti na sauti hivyo kupatikana zaidi za asimilia
85 ya Tanzania.
Maofisa wa Zantel wakizungumza na
wachuuzi wa matunda karibu ya soko la buguruni, Dar es Salaam, katika
moja ya kampeni za masoko kufikisha huduma na bidhaa zao karibu kwa
wateja. Zantel imemaliza hivi karibuni ukarabati mkubwa wa mtandao wake
wa 3G na 4G wenye lengo la kuboresha ubora wa huduma za intaneti na
sauti hivyo kupatikana zaidi za asimilia 85 ya Tanzania. Kutoka kushoto
ni, Mkuu wa Masoko, Gasper Mboya, Ofisa Mtendaji Mkuu, Benoit Janin na
Mkuu wa Mauzo, Herbert Louis.
Maofisa wa ngazi ya juu wa
Zantel wakibadilishana mawazo karibu na soko la Buguruni, Dar es Salaam
walipokwenda pamoja na timu ya mauzo kuzungumza na wateja na wakazi wa
maeneo hayo kuhusu huduma za Zantel na jjnsi ilivyojipanga upya
kuwaletea huduma bora. Kutoka kushoto; Ofisa Mtendaji Mkuu, Benoit
Janin, Kaimu CEO, Zadok Prescott, Mkuu wa Masoko, Gasper Mboya na Mkuu
wa Mauzo, Herbert Louis.
TAARIFA YA JESHI LA POLISI KWA VYOMBO VYA HABARI
Jeshi la Polisi nchini, katika
kuhakikisha usalama wa raia na mali zao unaimarika, limeendelea na
operesheni za kukamata wahalifu wa makosa mbalimbali yakiwemo makosa ya
usalama barabarani katika mikoa yote ili kudhibiti vitendo vya uhalifu
na wahalifu. Katika operesheni hizo, Jeshi la Polisi limefanikiwa
kukamata silaha na katika baadhi ya mikoa, wananchi wameweza kusalimisha
silaha kwa hiari katika vituo vya Polisi.
Operesheni hizi ni endelevu, na
ili tuweze kufanikiwa zaidi katika kudhibiti uhalifu na wahalifu
hususani katika kipindi hiki tunapoelekea mwisho wa mwaka, wananchi
wanatakiwa kuwa makini na kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu haraka
kwa kutumia namba za bure 111 na 112 pindi wanapowatilia shaka watu
wasiowajua katika maeneo yao ili hatua za haraka ziweze kuchukuliwa.
Kwa wamiliki wa maduka makubwa,
hoteli na maduka ya kufanyia miamala ya fedha kwa njia ya simu waangalie
namna ya kuweka vifaa maalumu vyenye uwezo wa kurekodi mienendo ya watu
wanaoingia na kutoka ama kufuata huduma katika maeneo yao ya biashara.
Pia, wananchi katika makazi yao
waimarishe ulinzi kwa kutumia mpango wa ulinzi jirani kwa kuhakikisha
wanakuwa na utaratibu wa kubadilishana taarifa za hali ya usalama ili
kuhakikisha mitaa yao inakuwa salama wakati wote.
Aidha, Jeshi la Polisi nchini
linawataka madereva wa vyombo vya moto kuheshimu na kutii sheria za
usalama barabarani ili kuepusha ajali na kuokoa maisha ya abiria na
watumiaji wengine wa barabara. Jeshi la polisi nchini, litaendelea
kutekeleza majukumu yake kwa mujibu wa sheria, bila woga ama upendeleo
katika kuhakikisha usalama wa raia na mali zao unaimarika.
Imetolewa na:
Advera John Bulimba – Kamishina Msaidizi wa Polisi (ACP)
Msemaji wa Jeshi la Polisi,
Makao Makuu ya Polisi.
No comments:
Post a Comment