Tuesday, August 30, 2016

"UKUTA" WAPATA NYUFA MWANZA, NI BAADA YA KATIBU MKUU WA CHADEMA, JOHN NWALILE KUJITOA KWENYE CHAMA HICHO NA KUJIUNGANA CCM AKIPINGA OPERESHENI HIYO



KATIBU Mkuu wa CHADEMA mkoani Mwanza, John Nwalile (pichani), ametangaza kukihama chama hicho na kujiunga na CCM mapema leo Agosti 30, 2016.
Akitangaza uamuzi huo mbele ya waandishi wa habari, alisema sababu kubwa aliyoitaja iliyomsukuma kukihama CHADEMA, ni pamoja na kutokuwa na sababu ya msingi ya kutomuunga mkono Rais John Pombe Magufuli katika jitihada zake za kujenga misingi mipya ya nchi ikiwa ni pamoja na kupambana na wala rushwa na kuimarisha uwajibikaji miongoni mwa watumishi wa umma.
Pia Nwalile amesema, sababu nyingine ni kupinga mpango wa Operesheni UKUTA iliyotangazwa nchinzima na Kamati Kuu ya CHADEMA ambayo imepangwa kuanza Septemba Mosi mwaka huu 2016.
Ikiwa imebaki siku moja tu kuanza kwa operesheni hiyo, kujitoa kwa kiongozi huyu wa juu kabisa wa CHADEMA kwenye mkoa wenye ushawishi mkubwa kisiasa hapa nchini ni pigo kubwa kwa chama hicho katika mkakati wake mpya wa UKUTA.



NMB YAWAKUMBUKA WATOTO WENYE USONJI, YAWAPA MSAADA WA VIFAA VYA MASOMO

Pamoja na kuwa bora utoaji wa huduma za kibenki lakini pia benki ya NMB imejipanga kuhakikisha inakuwa pia bora katika kusaidia jamii na katika kudhihilisha hilo imetoa msaada wa vifaa vya kutumia darasani na vya michezo kwa watoto walio na usonji (autism) ambao wanasoma katika shule ya msingi Mbuyuni, iliyopo Manispaa ya Kinondoni, Dar es Salaam.

Akielezea kuhusu msaada huo, Meneja wa Kanda ya Dar es Salaam wa NMB, Bi. Vicky Bishubo alisema wameamua kutoa msaada kwa shule hiyo kwa ajili ya kuwasaidia watoto wenye usonji kusoma katika mazingira mazuri hasa kutokana na hali zao jinsi zilivyo.

Meneja wa Kanda ya Dar es Salaam wa NMB, Bi. Vicky Bishubo akizungumza wakati wa kukabidhi vifaa vya shuleni kwa wanafunzi wa usonji katika shule ya Msingi Mbuyuni.

"NMB kila mwaka tunatenga asilimia moja ya faida ambayo tunaipata katika kusaidia jamii, tumeshatoa misaada mingi kama madawati na sasa tuliona tuwasaidie watoto hawa na tunaamini msaada wetu utaweza kuwasaidia kwa kiasi kikubwa," alisema Bi. Bishubo.

Kwa upande wa mgeni rasmi katika makabidhiano ya msaada huo, Kamishna wa Ustawi wa Jamii kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu, Rabikira Mushi aliwashukuru NMB kwa msaada ambao wamewapatia shule ya Mbuyuni na kuwataka kuendelea kuwa na moyo huo kwa kutoa msaada katika shule zingine zilizo na mahitaji.

Mgeni rasmi katika makabidhiano ya msaada huo, Kamishna wa Ustawi wa Jamii kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu, Rabikira Mushi akiwashukuru NMB kwa msaada ambao wamewapatia ambao unakadiriwa kuzidi Milioni 7.

Alisema licha ya serikali kufanya jitihada mbalimbali lakini bado inahitaji wadau wengine wa kusaidiana na kama kunakuwa na wadau kama NMB ambao wanajitoa kusaidia jamii basi wanakuwa wadau wa ukweli ambao wanaunga mkono juhudi za serikali kuleta maendeleo.

"Kwa nia yenu ya kusaidia jamii basi nyie mnaipatia kabisa serikali sababu inajitahidi kuleta elimu bora na hata kwa watoto hawa ambao bado kuna changamoto ya vifaa kwahiyo sisi tuwashukuru kwa msaada wenu na msisite tena kutusaidia siku tukiwafata kwa kuomba msaada," alisema Mushi.

Na Rabi Hume, MO BLOG


Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Mbuyuni, Dorothy Malecela akitoa neno la shukrani kwani niaba ya uongozi wa shule na wanafunzi. (Picha zote na Rabi Hume - MO BLOG)


Mgeni rasmi katika makabidhiano ya msaada huo, Kamishna wa Ustawi wa Jamii kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu, Rabikira Mushi akimshukuru Meneja wa Kanda ya Dar es Salaam wa NMB, Bi. Vicky Bishubo kwa msaada ambao wamewapatia.

Mgeni rasmi katika makabidhiano ya msaada huo, Kamishna wa Ustawi wa Jamii kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu, Rabikira Mushi na Meneja wa Kanda ya Dar es Salaam wa NMB, Bi. Vicky Bishubo wakicheza na wanafunzi wa Shule ya Msingi Mbuyuni.

Mgeni rasmi katika makabidhiano ya msaada huo, Kamishna wa Ustawi wa Jamii kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu, Rabikira Mushi akipokea vifaa vya michezo kutoka kwa Meneja wa Kanda ya Dar es Salaam wa NMB, Bi. Vicky Bishubo ambavyo vitatumiwa na wanafunzi wa Shule ya Msingi Mbuyuni.

Mwonekano wa baadhi ya vifaa vya michezo ambavyo NMB imetoa msaada kwa Shule ya Msingi Mbuyuni.
 Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, akisalimiana namakamanda wa Jeshi laUlinzila Wananchi wa Tanzania JWTZ, alipokutana nao ofisini kwake jijini Dar es Salaam leo Agosti 30, 2016. JWTZ itaadhimisha miaka 52 kwa kufanya usafi kote nchini. ambapo Makonda alitumia fursa hiyo kuzungumzia operesheni UKUTA na kuwaitawalioandaa operesheni hiyo iinayoratibiwa na CHADEMA, wamefikia mwisho wa kufikiri.
WAZIRI NAPE AZINDUA MICHEZO YA UMOJA WA VYAMA VYA WALIMU WA NCHI ZA KUSINI MWA AFRIK

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akisalimiana na wachezaji wakati wa  ufunguzi  wa mashindano ya  Vyama Vya Walimu wa Nchi za Kusini mwa Afrika (SATO) kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, Agosti 30, 2016.(PICHA NA LORIETHA LAURENCE WHUSM)


Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akifyatua baruti juu kuashiria ufunguzi rasmi wa mashindano ya Vyama vya Walimu wa Nchi za Kusini mwa Afrika(SATO) leo JijiniDar es Salaam.


Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akisalimiana na wachezaji wakati wa  ufunguzi  wa mashindano ya  Vyama Vya Walimu wa Nchi za Kusini mwa Afrika (SATO) kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, Agosti 30, 2016.


Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akitoa salamu kwa wanamichezo ambao ni walimu wanaowakilisha nchi za kusini mwa Afrika wakati wa ufunguzi wa mashindano hayo leo jijini Dar es Salaam. Wa pili kulia ni Rais wa  Umoja wa Vyama vya Walimu wa Nchi za Kusini mwa Afrika (SATO) Bw. Henry Kapenda na kushoto ni Rais wa Chama cha WaalimuTanzania (CWT) Bw. Gratian Mukoba.


Rais wa Chama cha  Walimu wa Nchi za Kusini mwa Afrika (SATO) Bw. Henry Kapenda akizungumza wakati wa ufunguzi wa mashindano ya Umoja wa Vyama vya walimu wa Nchi za Kusini mwa Afrika (SATO) leo Jijini Dar es Salaam. Katikati ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye, na kushoto ni Rais wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT)Bw. Gratian Mukoba.


Rais wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT) Bw. Gratian Mukoba akisoma risala wakati wa ufunguzi wa mashindano ya Vyama vya Walimu wa Nchi za Kusini mwa Afrika (SATO), kulia ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye.


Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (katikati) akiimba wimbo wa Taifa wakati wa ufunguzi wa   mashindano ya michezo inayoshirikisha Vyama vya Walimu wa Nchi za Kusini mwa Afrika (SATO), wa pili kushoto ni Rais wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT)Bw. Gratian Mukoba, na kushoto ni Katibu kutoka Ofisi ya Uhamiaji wa Ubalozi wa Malawi Bw. Michael Gama.  Wa pili kulia ni Rais wa Umoja wa Vyama vya Walimu wa Nchi za Kusini mwa Afrika (SATO) Bw. Henry Kapenda na kulia ni Katibu Mkuu wa chama hicho Bw. Richard Gundane.


Wanamichezo ambao ni walimu kutoka Afrika ya Kusini wakiingia uwanjani wakati wa ufunguzi wa mashindano yaliyoshirikisha nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) leo Jijini Dar es Salaam.


Wanamichezo ambao ni walimu kutoka Zambia wakiingia uwanjani wakati wa ufunguzi wa mashindano yaliyoshirikisha nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) leo JijiniDar es Salaam.


Wanamichezo ambao ni walimu kutoka Tanzania wakiingia uwanjani wakati wa ufunguzi wa mashindano yaliyoshirikisha nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) leo Jijini Dar es Salaam.



Kikosi cha Brass Bendi ya Polisi Nchini wakiongoza maandamano ya wanamichezo ambao ni walimu kutoka nchi za Kusini mwa Afrika kuingia uwanjani wakati wa ufunguzi wa mashindano hayo leo Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe akizungumza wakati wa kongamano la kujadili uhifadhi wa misitu pamoja na kuzindua ripoti ya uvunaji wa misitu na mapendekezo ya kuboresha utawala wa misitu nchini Tanzania.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe(katikati) akizindua ripoti ya matokeo ya utafiti pamoja na mapendekezo ya kuboresha utawala wa misitu nchini Tanzania, Wa kwanza kulia ni Mwakilishi wa Bodi ya Jumuiko la Maliasili Tanzania( TNRF), Charles Meshack na kulia ni Msaidizi wa Balozi wa Finland nchini Tanzania, Simo-Pekka Parviainen
Msaidizi wa Balozi wa Finland nchini Tanzania, Simo-Pekka Parviainen akizungumza jambo wakati wakuzindua ripoti ya uvunaji wa misitu pamoja na kujadili ripoti hiyo
  Mwakilishi wa Bodi ya Jumuiko la Maliasili Tanzania( TNRF), Charles Meshack akizungumza jambo wakati wa kongamano lililowahusisha wadau mbalimbali wa misitu ili kujadili ripoti ya uvunaji wa misitu nchini Tanzania.
Mtafiti na Mshauri wa masuala ya Misitu, Kihana Lukumbuzya akiwasilisha ripoti ya uvunaji wa misitu kwa waziri wa Maliasili na Utalii pamoja na wadau mbalimbali wa masuala ya misitu(hawapo pichani) katika ukumbi wa Utalii leo jijini Dar es Salaam
   Waziri wa Maliasili na Utalii Profesa Jumanne Maghembe(wa kwanza kushoto) pamoja na wadau mbalimbali wakifuatilia uwasilishwaji wa ripoti ya uvunaji wa misitu iliyokuwa ikiwasilishwa na Mtafiti na Mshauri wa masuala ya Misitu, Kihana Lukumbuzya.
Baadhi ya wadau wakifuatilia mada
Mkurugenzi wa Jumuiko la Maliasili Tanzania( TNRF), Joseph Olila akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mapendekezo yaliyopatikana katika utafiti pamoja na kuboresha utawala wa misitu nchini Tanzania.
Baadhi ya wadau wa misitu wakifuatilia mada kwenye kongamano hilo lililofanyika leo jijini Dar es Salaam
Picha ya Pamoja


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akisalimiana na balozi wa India nchini Mhe.Sandeep Arya aliyekutana naye na kufanya mazungumzo Ikulu jijini Dar es salaam leo Agosti 30, 2016. (PICHA NA IKULU)


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimsindikiza  balozi wa India nchini Mhe.Sandeep Arya aliyekutana naye na kufanya mazungumzo Ikulu jijini Dar es salaam leo Agosti 30, 2016


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akisalimiana na balozi wa Cuba nchini Mhe Jorge Lopez Tormo aliyekutana naye na kufanya mazungumzo Ikulu jijini Dar es salaam leo Agosti 30, 2016



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akifanya  mazungumzo na balozi wa Cuba Mhe Jorge Lopez Tormo nchini Ikulu jijini Dar es salaam leo Agosti 30, 2016
Bw. Simon Kivamwo
Waandishi wa habari wakitoa damu ili kuwezesha matibabu ya Mwandishi wa habari mkongwe hapa nchini Bw. Simon Kivamwo ambaye anapatiwa matibabu kwenye hospitali ya Ocean Raod iluyoko jijini Dar es Salaam leo Agosti 30, 2016. Kwa mujibu wa Mwandishi wa Habari anayeratibu zoezi hilo Bw. Benjamin Thompson, Kivamwo ambaye anaugua kwa muda mrefu sasa, amezidiwa na maradhi leo hii na kukimbizwa kwenye hospitali hiyo ambapo madaktari walihitaji kumuongezea damu. Thomspon ametoa  wito kwa wanahabari na jamii kwa ujumla kujitokeza kumchangia damu mwanidhi mwenzetu ili kuokoa maisha yake. Sehemu ya kutolea damu ni Hospitali ya Mnazi Mmoja, Kariakoo jijini Dar es Salaam
MO AKUTANA NA WAZIRI MKUU MAJALIWA JIJINI DAR ES SALAA


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akizungumza na Mkurugenzi  Mtendaji wa Makampuni ya  Mohammed  Enterprises Tanzania Limited (METEL), Bw. Mohammed Dewji, Ofisini kwake jijini Dar es salaam Agosti 30, 2016. (PICHA NA OFISI YA WAZIRI

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akiwa katika picha ya pamoja na watumishi wa NSSF baada ya kukabidhiwa hundi ya shilingi milioni 50  na Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Profesa Godius Kanyarara (kushoto), Ofisini kwake jijini Dar es salaam Agosti 30. 2016. (PICHA NA OFISI YA WAZIRI MKUU)
NA MWANDISHI MAALUM

WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amepokea msaada wa sh. milioni 50 kutoka Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) ili kusaidia ujenzi wa shule ya sekondari Lindi iliyoungua moto usiku wa kuamkia Julai 10 mwaka huu.
NSSF imetoa msaada huo ikiwa ni utekelezaji wa ahadi yake iliyoitoa  Julai 17, 2016 katika harambee ya kuchangisha fedha za ujenzi wa majengo ya shule ya hiyo iliyoendeshwa na Waziri Mkuu .
Katika ajali hiyo, shule ya sekondari Lindi iliathirika kwa asilimia 34 ambapo vyumba tisa vya madarasa, jengo lenye matundu 26 ya vyoo na jengo la maabara ya kemia na fizikia yaliungua na kusababishia hasara ya sh. milioni 682.78.
Akipokea msaada huo leo (Jumanne, Agosti 30, 2016) Waziri Mkuu ameushukuru uongozi wa shirika hilo na kuwaomba wadau wengine waliotoa ahadi wazitekeleze ili waweze kukamilizsha ujenzi wa majengo hayo.
“Naamini fedha hizi zitakwenda kufanya kazi ambayo NSSF wameikusudia. Na leo hii naikabidhi kwa Meya wa Manispaa ya Lindi pamoja na  Mkurugenzi wake ili waende kuzifanyia kazi,” amesema.
Baada ya kukabidhiwa hundi hiyo na Waziri Mkuu, Meya wa Manispaa ya Lindi, Mohamed Lihumbo amelishukuru shirika hilo kwa kutimiza ahadi waliyoitoa siku ya harambee na kwamba fedha hizo hazitapotea kwa sababu zinaenda kutumika katika malengo yaliyokusudiwa.
Meya huyo amesema baada ya kukamilisha ujenzi wa shule hiyo wataanda hafla na kuwaita wadau wote waliotoa michango yao kwa ajili ya ujenzi huo ili wakaone matumizi ya michango waliyoitoa.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Prof. Godius Kahyarara amesema msaada huo ni sehemu ya mpango wa shirika hilo wa kusaidia jamii katika mambo mbalimbali kwa mujibu wa sera iliyowekwa na shirika hilo.
“NSSF imekuwa kinara kwenye Mifuko ya Hifadhi ya Jamii kwa kutoa misaada mbalimbali ya kijamii ambapo imejiwekea sera ya kusaidia katika sekta za elimu, afya na huduma nyingine muhimu za kijamii,” amesema.
Prof. Kahyarara amesema misaada hiyo haiathiri michango ya wanachama wa mfuko huo na mafao yatolewayo kwani hutokana na faida inayopatikana kwa uwekezaji makini wa mfuko huo.


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akipokea hundi  ya Shilingi milioni 50 kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu  wa NSSF,  Profesa Godius Kahyarara kwa ajili ya ujenzi na ukarabati wa Shule ya Sokondari ya Lindi iliyoungua moto. Makabidhiano hayo yalifanyika  Ofisini kwa Kwaziri Mkuu jijini Dar es salaam Agosti 30, 2016
Wazri Mkuu, Kassim Majaliwa  akizungumza badaa ya kupokea hundi ya shilingi milioni 50 kwa ajili ya ujenzi na ukarabati wa Shule ya Sekondari ya Lindi ambayo iliungua moto.  Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Profesa Godius Kanyarara, Wapili kulia ni Mkurugenzi wa manispaa ya Lindi, Jomaary Satura na wapili kushoto ni Meya wa Manispaa ya Lindi, Mohamed Lihumbo
Meya wa manispaa ya Lindi, Mohamed Lihumbo akizungumza baada ya  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kukabidhiwa hundi ya Shilingi milioni 50 kwa ajili ukarabati na ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Lindi iliyoungua Moto . Makabidhiano ya hundi hiyo yalifanyika Ofisini kwa Waziri Mkuu jijini Dar es salaam Agosti 30, 2016. Wapili kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Profesa Godius Kanyarara na wapili kulia ni Mkurugenzi wa manispaa ya Lindi, Jomaary Satura
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akiagana na watumishi wa NSSF baada ya kukabidhiwa hundi ya  Shilingi milioni 50 kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Profesa  Godius Kanyarara  (kushoto), Ofisini kwake jijini Dar es salaam Agosti 30, 2016
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akiagana na watumishi wa NSSF baada ya kukabidhiwa hundi ya  Shilingi milioni 50 kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Profesa  Godius Kanyarara  (kushoto), Ofisini kwake jijini Dar es salaam Agosti 30, 2016

Waandishi wa habari waliohudhuria katika tukio la NSSF kumkabidhi Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  hundi ya sh. milioni 50 kwa ajili ya ujenzi na ukarabati wa Shule ya Sekondari ya Lindi iliyoungua . Makabidhiano hayo yalifanyika Ofisini kwa Waziri Mkuu jjini Dar es salaam Agosti 30, 2016.

No comments :

Post a Comment