KATIBU
Mkuu wa CHADEMA mkoani Mwanza, John Nwalile (pichani), ametangaza kukihama chama hicho na
kujiunga na CCM mapema leo Agosti 30, 2016.
Akitangaza uamuzi huo mbele ya waandishi wa habari, alisema sababu
kubwa aliyoitaja iliyomsukuma kukihama CHADEMA, ni pamoja na kutokuwa na sababu
ya msingi ya kutomuunga mkono Rais John Pombe Magufuli katika jitihada zake za
kujenga misingi mipya ya nchi ikiwa ni pamoja na kupambana na wala rushwa na
kuimarisha uwajibikaji miongoni mwa watumishi wa umma.
Pia
Nwalile amesema, sababu nyingine ni kupinga mpango wa Operesheni UKUTA
iliyotangazwa nchinzima na Kamati Kuu ya CHADEMA ambayo imepangwa kuanza
Septemba Mosi mwaka huu 2016.
Ikiwa
imebaki siku moja tu kuanza kwa operesheni hiyo, kujitoa kwa kiongozi huyu wa
juu kabisa wa CHADEMA kwenye mkoa wenye ushawishi mkubwa kisiasa hapa nchini ni
pigo kubwa kwa chama hicho katika mkakati wake mpya wa UKUTA.
NMB YAWAKUMBUKA WATOTO WENYE USONJI, YAWAPA MSAADA WA VIFAA VYA MASOMO
Pamoja na kuwa bora utoaji wa huduma za
kibenki lakini pia benki ya NMB imejipanga kuhakikisha inakuwa pia bora
katika kusaidia jamii na katika kudhihilisha hilo imetoa msaada wa vifaa
vya kutumia darasani na vya michezo kwa watoto walio na usonji (autism)
ambao wanasoma katika shule ya msingi Mbuyuni, iliyopo Manispaa ya
Kinondoni, Dar es Salaam.
Akielezea kuhusu msaada huo, Meneja wa
Kanda ya Dar es Salaam wa NMB, Bi. Vicky Bishubo alisema wameamua kutoa
msaada kwa shule hiyo kwa ajili ya kuwasaidia watoto wenye usonji kusoma
katika mazingira mazuri hasa kutokana na hali zao jinsi zilivyo.
Meneja wa Kanda ya Dar es Salaam wa NMB,
Bi. Vicky Bishubo akizungumza wakati wa kukabidhi vifaa vya shuleni kwa
wanafunzi wa usonji katika shule ya Msingi Mbuyuni.
"NMB kila mwaka tunatenga asilimia moja
ya faida ambayo tunaipata katika kusaidia jamii, tumeshatoa misaada
mingi kama madawati na sasa tuliona tuwasaidie watoto hawa na tunaamini
msaada wetu utaweza kuwasaidia kwa kiasi kikubwa," alisema Bi. Bishubo.
Kwa upande wa mgeni rasmi katika
makabidhiano ya msaada huo, Kamishna wa Ustawi wa Jamii kutoka Ofisi ya
Waziri Mkuu, Rabikira Mushi aliwashukuru NMB kwa msaada ambao
wamewapatia shule ya Mbuyuni na kuwataka kuendelea kuwa na moyo huo kwa
kutoa msaada katika shule zingine zilizo na mahitaji.
Mgeni rasmi katika makabidhiano ya
msaada huo, Kamishna wa Ustawi wa Jamii kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu,
Rabikira Mushi akiwashukuru NMB kwa msaada ambao wamewapatia ambao
unakadiriwa kuzidi Milioni 7.
Alisema licha ya serikali kufanya
jitihada mbalimbali lakini bado inahitaji wadau wengine wa kusaidiana na
kama kunakuwa na wadau kama NMB ambao wanajitoa kusaidia jamii basi
wanakuwa wadau wa ukweli ambao wanaunga mkono juhudi za serikali kuleta
maendeleo.
"Kwa nia yenu ya kusaidia jamii basi
nyie mnaipatia kabisa serikali sababu inajitahidi kuleta elimu bora na
hata kwa watoto hawa ambao bado kuna changamoto ya vifaa kwahiyo sisi
tuwashukuru kwa msaada wenu na msisite tena kutusaidia siku tukiwafata
kwa kuomba msaada," alisema Mushi.
Na Rabi Hume, MO BLOG
Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Mbuyuni,
Dorothy Malecela akitoa neno la shukrani kwani niaba ya uongozi wa
shule na wanafunzi. (Picha zote na Rabi Hume - MO BLOG)
Mgeni rasmi katika makabidhiano ya
msaada huo, Kamishna wa Ustawi wa Jamii kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu,
Rabikira Mushi akimshukuru Meneja wa Kanda ya Dar es Salaam wa NMB, Bi.
Vicky Bishubo kwa msaada ambao wamewapatia.
Mgeni rasmi katika makabidhiano ya
msaada huo, Kamishna wa Ustawi wa Jamii kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu,
Rabikira Mushi na Meneja wa Kanda ya Dar es Salaam wa NMB, Bi. Vicky
Bishubo wakicheza na wanafunzi wa Shule ya Msingi Mbuyuni.
Mgeni rasmi katika makabidhiano ya
msaada huo, Kamishna wa Ustawi wa Jamii kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu,
Rabikira Mushi akipokea vifaa vya michezo kutoka kwa Meneja wa Kanda ya
Dar es Salaam wa NMB, Bi. Vicky Bishubo ambavyo vitatumiwa na wanafunzi
wa Shule ya Msingi Mbuyuni.
Mwonekano wa baadhi ya vifaa vya michezo ambavyo NMB imetoa msaada kwa Shule ya Msingi Mbuyuni.
Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul
Makonda, akisalimiana namakamanda wa Jeshi laUlinzila Wananchi wa
Tanzania JWTZ, alipokutana nao ofisini kwake jijini Dar es Salaam leo
Agosti 30, 2016. JWTZ itaadhimisha miaka 52 kwa kufanya usafi kote
nchini. ambapo Makonda alitumia fursa hiyo kuzungumzia operesheni UKUTA
na kuwaitawalioandaa operesheni hiyo iinayoratibiwa na CHADEMA,
wamefikia mwisho wa kufikiri.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses
Nnauye akisalimiana na wachezaji wakati wa ufunguzi wa
mashindano ya Vyama Vya Walimu wa Nchi za Kusini mwa Afrika (SATO) kwenye
uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, Agosti 30, 2016.(PICHA NA LORIETHA LAURENCE WHUSM)
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses
Nnauye akifyatua baruti juu kuashiria ufunguzi rasmi wa mashindano ya Vyama vya
Walimu wa Nchi za Kusini mwa Afrika(SATO) leo JijiniDar es Salaam.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses
Nnauye akisalimiana na wachezaji wakati wa ufunguzi wa
mashindano ya Vyama Vya Walimu wa Nchi za Kusini mwa Afrika (SATO) kwenye
uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, Agosti 30, 2016.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses
Nnauye akitoa salamu kwa wanamichezo ambao ni walimu wanaowakilisha nchi za
kusini mwa Afrika wakati wa ufunguzi wa mashindano hayo leo jijini Dar es
Salaam. Wa pili kulia ni Rais wa Umoja wa Vyama vya Walimu wa Nchi
za Kusini mwa Afrika (SATO) Bw. Henry Kapenda na kushoto ni Rais wa Chama cha
WaalimuTanzania (CWT) Bw. Gratian Mukoba.
Rais wa Chama cha Walimu wa Nchi za Kusini mwa Afrika
(SATO) Bw. Henry Kapenda akizungumza wakati wa ufunguzi wa mashindano ya Umoja
wa Vyama vya walimu wa Nchi za Kusini mwa Afrika (SATO) leo Jijini Dar
es Salaam. Katikati ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape
Moses Nnauye, na kushoto ni Rais wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT)Bw.
Gratian Mukoba.
Rais wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT) Bw. Gratian
Mukoba akisoma risala wakati wa ufunguzi wa mashindano ya Vyama vya Walimu wa
Nchi za Kusini mwa Afrika (SATO), kulia ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa
na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses
Nnauye (katikati) akiimba wimbo wa Taifa wakati wa ufunguzi wa mashindano
ya michezo inayoshirikisha Vyama vya Walimu wa Nchi za Kusini mwa Afrika
(SATO), wa pili kushoto ni Rais wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT)Bw.
Gratian Mukoba, na kushoto ni Katibu kutoka Ofisi ya Uhamiaji wa Ubalozi wa
Malawi Bw. Michael Gama. Wa pili kulia ni Rais wa Umoja wa Vyama vya
Walimu wa Nchi za Kusini mwa Afrika (SATO) Bw. Henry Kapenda na kulia ni Katibu
Mkuu wa chama hicho Bw. Richard Gundane.
Wanamichezo ambao ni walimu kutoka Afrika ya Kusini wakiingia
uwanjani wakati wa ufunguzi wa mashindano yaliyoshirikisha nchi za Kusini mwa
Afrika (SADC) leo Jijini Dar es Salaam.
Wanamichezo ambao ni walimu kutoka Zambia wakiingia uwanjani
wakati wa ufunguzi wa mashindano yaliyoshirikisha nchi za Kusini mwa Afrika
(SADC) leo JijiniDar es Salaam.
Wanamichezo ambao ni walimu kutoka Tanzania wakiingia uwanjani
wakati wa ufunguzi wa mashindano yaliyoshirikisha nchi za Kusini mwa Afrika
(SADC) leo Jijini Dar es Salaam.
Kikosi cha Brass Bendi ya Polisi Nchini wakiongoza maandamano ya
wanamichezo ambao ni walimu kutoka nchi za Kusini mwa Afrika kuingia uwanjani
wakati wa ufunguzi wa mashindano hayo leo Jijini Dar es Salaam.
MO AKUTANA NA WAZIRI MKUU MAJALIWA JIJINI DAR ES SALAA
Waziri
wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe akizungumza wakati wa
kongamano la kujadili uhifadhi wa misitu pamoja na kuzindua ripoti ya
uvunaji wa misitu na mapendekezo ya kuboresha utawala wa misitu nchini
Tanzania.
Waziri
wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe(katikati) akizindua
ripoti ya matokeo ya utafiti pamoja na mapendekezo ya kuboresha utawala
wa misitu nchini Tanzania, Wa kwanza kulia ni Mwakilishi wa Bodi ya Jumuiko la Maliasili Tanzania( TNRF), Charles Meshack na kulia ni Msaidizi wa Balozi wa Finland nchini Tanzania, Simo-Pekka Parviainen
Msaidizi
wa Balozi wa Finland nchini Tanzania, Simo-Pekka Parviainen akizungumza
jambo wakati wakuzindua ripoti ya uvunaji wa misitu pamoja na kujadili
ripoti hiyo
Mwakilishi
wa Bodi ya Jumuiko la Maliasili Tanzania( TNRF), Charles Meshack
akizungumza jambo wakati wa kongamano lililowahusisha wadau mbalimbali
wa misitu ili kujadili ripoti ya uvunaji wa misitu nchini Tanzania.
Mtafiti
na Mshauri wa masuala ya Misitu, Kihana Lukumbuzya akiwasilisha ripoti
ya uvunaji wa misitu kwa waziri wa Maliasili na Utalii pamoja na wadau
mbalimbali wa masuala ya misitu(hawapo pichani) katika ukumbi wa Utalii
leo jijini Dar es Salaam
Waziri wa Maliasili na Utalii Profesa Jumanne Maghembe(wa kwanza kushoto) pamoja na wadau mbalimbali wakifuatilia uwasilishwaji wa ripoti ya uvunaji wa misitu iliyokuwa ikiwasilishwa na Mtafiti na Mshauri wa masuala ya Misitu, Kihana Lukumbuzya.
Baadhi ya wadau wakifuatilia mada
Mkurugenzi
wa Jumuiko la Maliasili Tanzania( TNRF), Joseph Olila akizungumza na
waandishi wa habari kuhusu mapendekezo yaliyopatikana katika utafiti
pamoja na kuboresha utawala wa misitu nchini Tanzania.
Baadhi ya wadau wa misitu wakifuatilia mada kwenye kongamano hilo lililofanyika leo jijini Dar es Salaam
Picha ya Pamoja
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akisalimiana na balozi
wa India nchini Mhe.Sandeep Arya aliyekutana naye na kufanya mazungumzo Ikulu
jijini Dar es salaam leo Agosti 30, 2016. (PICHA NA IKULU)
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimsindikiza
balozi wa India nchini Mhe.Sandeep Arya aliyekutana naye na kufanya
mazungumzo Ikulu jijini Dar es salaam leo Agosti 30, 2016
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akisalimiana na balozi
wa Cuba nchini Mhe Jorge Lopez Tormo aliyekutana naye na kufanya mazungumzo
Ikulu jijini Dar es salaam leo Agosti 30, 2016
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akifanya
mazungumzo na balozi wa Cuba Mhe Jorge Lopez Tormo nchini Ikulu jijini
Dar es salaam leo Agosti 30, 2016
Bw. Simon Kivamwo |
Waandishi
wa habari wakitoa damu ili kuwezesha matibabu ya Mwandishi wa habari
mkongwe hapa nchini Bw. Simon Kivamwo ambaye anapatiwa matibabu kwenye
hospitali ya Ocean Raod iluyoko jijini Dar es Salaam leo Agosti 30,
2016. Kwa mujibu wa Mwandishi wa Habari anayeratibu zoezi hilo
Bw. Benjamin Thompson, Kivamwo ambaye anaugua kwa muda mrefu sasa, amezidiwa na
maradhi leo hii na kukimbizwa kwenye hospitali hiyo ambapo madaktari
walihitaji kumuongezea damu. Thomspon ametoa wito kwa
wanahabari na jamii kwa ujumla kujitokeza kumchangia damu mwanidhi
mwenzetu ili kuokoa maisha yake. Sehemu ya kutolea damu ni Hospitali ya
Mnazi Mmoja, Kariakoo jijini Dar es Salaam
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na
watumishi wa NSSF baada ya kukabidhiwa hundi ya shilingi milioni 50 na
Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Profesa Godius Kanyarara (kushoto), Ofisini kwake
jijini Dar es salaam Agosti 30. 2016. (PICHA
NA OFISI YA WAZIRI MKUU)
NA MWANDISHI MAALUM
WAZIRI MKUU, Kassim
Majaliwa amepokea msaada wa sh. milioni 50 kutoka Shirika la Taifa la Hifadhi
ya Jamii (NSSF) ili kusaidia ujenzi wa shule ya sekondari Lindi iliyoungua moto
usiku wa kuamkia Julai 10 mwaka huu.
NSSF imetoa msaada huo
ikiwa ni utekelezaji wa ahadi yake iliyoitoa Julai 17, 2016 katika
harambee ya kuchangisha fedha za ujenzi wa majengo ya shule ya hiyo
iliyoendeshwa na Waziri Mkuu .
Katika ajali hiyo, shule ya sekondari Lindi iliathirika kwa asilimia
34 ambapo vyumba tisa vya madarasa, jengo lenye matundu 26 ya vyoo na jengo la
maabara ya kemia na fizikia yaliungua na kusababishia hasara ya sh. milioni
682.78.
Akipokea msaada huo leo
(Jumanne, Agosti 30, 2016) Waziri Mkuu ameushukuru uongozi wa shirika hilo na
kuwaomba wadau wengine waliotoa ahadi wazitekeleze ili waweze kukamilizsha
ujenzi wa majengo hayo.
“Naamini fedha hizi
zitakwenda kufanya kazi ambayo NSSF wameikusudia. Na leo hii naikabidhi kwa
Meya wa Manispaa ya Lindi pamoja na Mkurugenzi wake ili waende
kuzifanyia kazi,” amesema.
Baada ya kukabidhiwa
hundi hiyo na Waziri Mkuu, Meya wa Manispaa ya Lindi, Mohamed Lihumbo
amelishukuru shirika hilo kwa kutimiza ahadi waliyoitoa siku ya harambee na
kwamba fedha hizo hazitapotea kwa sababu zinaenda kutumika katika malengo
yaliyokusudiwa.
Meya huyo amesema baada
ya kukamilisha ujenzi wa shule hiyo wataanda hafla na kuwaita wadau wote
waliotoa michango yao kwa ajili ya ujenzi huo ili wakaone matumizi ya michango
waliyoitoa.
Kwa upande wake
Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Prof. Godius Kahyarara amesema msaada huo ni sehemu ya
mpango wa shirika hilo wa kusaidia jamii katika mambo mbalimbali kwa mujibu wa
sera iliyowekwa na shirika hilo.
“NSSF imekuwa kinara
kwenye Mifuko ya Hifadhi ya Jamii kwa kutoa misaada mbalimbali ya kijamii
ambapo imejiwekea sera ya kusaidia katika sekta za elimu, afya na huduma
nyingine muhimu za kijamii,” amesema.
Prof. Kahyarara amesema
misaada hiyo haiathiri michango ya wanachama wa mfuko huo na mafao yatolewayo
kwani hutokana na faida inayopatikana kwa uwekezaji makini wa mfuko huo.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea hundi ya Shilingi
milioni 50 kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Profesa Godius
Kahyarara kwa ajili ya ujenzi na ukarabati wa Shule ya Sokondari ya Lindi
iliyoungua moto. Makabidhiano hayo yalifanyika Ofisini kwa Kwaziri Mkuu
jijini Dar es salaam Agosti 30, 2016
Wazri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza badaa ya kupokea hundi ya
shilingi milioni 50 kwa ajili ya ujenzi na ukarabati wa Shule ya Sekondari ya
Lindi ambayo iliungua moto. Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Profesa
Godius Kanyarara, Wapili kulia ni Mkurugenzi wa manispaa ya Lindi, Jomaary
Satura na wapili kushoto ni Meya wa Manispaa ya Lindi, Mohamed Lihumbo
Meya wa manispaa ya Lindi, Mohamed Lihumbo akizungumza baada ya
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kukabidhiwa hundi ya Shilingi milioni 50 kwa
ajili ukarabati na ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Lindi iliyoungua Moto .
Makabidhiano ya hundi hiyo yalifanyika Ofisini kwa Waziri Mkuu jijini Dar es
salaam Agosti 30, 2016. Wapili kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Profesa
Godius Kanyarara na wapili kulia ni Mkurugenzi wa manispaa ya Lindi, Jomaary
Satura
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiagana na watumishi wa NSSF baada
ya kukabidhiwa hundi ya Shilingi milioni 50 kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa
NSSF, Profesa Godius Kanyarara (kushoto), Ofisini kwake jijini Dar
es salaam Agosti 30, 2016
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiagana na watumishi wa NSSF baada
ya kukabidhiwa hundi ya Shilingi milioni 50 kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa
NSSF, Profesa Godius Kanyarara (kushoto), Ofisini kwake jijini Dar
es salaam Agosti 30, 2016
Waandishi wa habari waliohudhuria katika tukio la NSSF
kumkabidhi Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa hundi ya sh. milioni 50 kwa ajili
ya ujenzi na ukarabati wa Shule ya Sekondari ya Lindi iliyoungua . Makabidhiano
hayo yalifanyika Ofisini kwa Waziri Mkuu jjini Dar es salaam Agosti 30, 2016.
No comments:
Post a Comment