Friday, August 5, 2016

BINTI WA RAIS OBAMA, SASHA AFANYA KIBARUA CHA KUTOA HUDUMA HOTELINI


Sasha Obama, binti wa rais wa Marekani Barack Obama, ameacha kwa muda kudeka Ikulu na kufanya kazi ya uhudumu kwenye kaunta ya hoteli ya vyakula vya baharini.

Shasha mwenye miaka 15 amechukua kibarua cha muda katika majira ya joto kwa sasa katika eneo la biashara huko Martha's Vineyard, Massachusetts.

Sasha, anatumia jina lake kamili la Natasha, amekuwa akisindikizwa kwenda kufanya kazi kwenye hoteli hiyo na walinzi wa rais sita kwa mujibu wa Boston Herald.

NYOSHI EL SADAT AHAIDI KUWAPAGAWISHA WAKAZI WA JIJI LA ARUSHA

WAKURUGENZI WA MIKOA YA KANDA YA KASKAZINI WATAKIWA KUJENGA MABANDA YA KISASA YA MAONYESHO YA NANE NANE

Wa kwanza kulia ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa Maiko Lekule Laiser ,akifuatiwa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Daud Filex Ntibenda, aliyepo kushoto kwa mkuu huyo ni mwenyekiti wa Taso kanda ya Kaskazini ndugu Athar Kitonga Shayo wakiwa katika uzinduzi wa maonyeho hayo ya wakulima na wafugaji katika viwanja vya Taso Themi nanenane Njiro Jijini Arusha.
Vijana wa JKT Oljoro wakiwa wanatoa burudani siku ya uzinduzi wa maonyesho ya wakulima na wafugai ya nayandelea katika vianja vya Taso Themi nanenane njiro Arusha.
Meya wa Jiji la.Arusha wa pili kutoka kulia ndugu Calist Lazaro akiwa wakiteta jambo na diwani wa kata ya Themi Melance .E.Kinabo wa kwanza kulia katika maonyesho yanayoendelea katika maonysho yanayoendelea katika viwanja vya Taso nanenane Njiro Jijini Arusha.

SERENGETI YAFUNGUA UKURASA AFRIKA KUSINI

TAARIFA KWA UMMA KUTOKA SIMBA SPORT CLUB KUHUSU SIMBA DAY

MKUU WA MKOA WA MWANZA AFUNGUA RASMI MAONESHO YA NANENANE KANDA YA ZIWA

Mkuu wa mkoa wa Mwanza, John Mongela (wa pili kulia, akikagua banda la Benki Kuu, kwenye Maonesho ya Nanenane yanayofanyika kwenye uwanja wa Nyamuhongolo Jijini Mwanza, kwa mikoa ya Kanda ya Ziwa
Mkuu wa mkoa wa Mwanza, John Mongela, akisaini kitabu cha wageni kwenye banda la Benki kuu, kwenye maoneshp ya Nanenane Jijini Mwanza.
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack (kushoto) akiteta jambo na Mkuu wa mkoa wa Mwanza, John Mongella (kulia)
        Mcheza ngoma wa kikundi cha kutoka Bujora akitumbuiza huku akicheza na nyoka

Na, Binagi Online TV

Mkuu wa mkoa wa Mwanza, John Mongela, ameiagiza Mamlaka ya Usimamizi wa Biashara Tan-trade kukamilisha ramani ya viwanja vya Nyamuhongolo vinavyotumika kwa maonesho ya Wakulima na Wafugaji Nanenane ili kuanza ujenzi wa majengo ya kudumu kwenye viwanja hivyo.

Akifungua rasmi jana maonesho ya Nanenane yanayohusisha mikoa ya Kanda
ya ziwa, Mongela, alisema kukamilika kwa ramani hiyo kutaharakisha kuanza kwa ujenzi wa mabanda ya kudumu kwenye viwanja hivyo ili kuwezesha kuendelea kwa shughuli mbalimbali hata maonesho yatakapomalizika.

Alisema mkoa wa Mwanza kwa kushirikiana na mikoa mingine ya kanda ya ziwa, umejipanga kuandaa maonesho ya Nanenane kitaifa ndani ya miaka miwili ijayo, hivyo ujenzi wa mabanda hayo utachangia kuongeza hamasha ya mikoa hiyo kuwa mwenyeji.

Aidha mkuu huyo wa mkoa wa Mwanza ameungana na mwenzake wa mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack, kuwahamasisha wakulima wa mikoa hiyo kufufua kilimo cha pamba ambacho amesema kitachangia kufufua viwanda mbalimbali na kuongeza fursa za ajira hasa kwa vijana na hivyo kukuza pato la familia na taifa kwa jumla.

NAIBU WAZIRI WA ELIMU MH. MHANDISI STELLA MANYANYA AWA MGENI RASMI MAHAFALI YA BROOKHOUSE INTERNATIONAL SCHOOL JIJINI DAR

MKUU WA WILAYA YA IKUNGI ATOA ONYO KWA WANASIASA WANAOKOSESHA MAPATO YA HALMASHAURI

CHUO CHA UONGOZI WA FEDHA KUWAPELEKA WANAFUNZI TAASISI ZA KIJAMII KUFANYA MAZOEZI KWA VITENDO

SERENGETI BOYS WAKIWA KATIKA MAZOEZI NCHINI AFRIKA KUSINI

CHEIKHOU KOUYATE APACHIKA MAWILI WAKATI WEST HAM IKITINGA HATUA YA MTOANO LIGI YA UROPA

Mchezaji Cheikhou Kouyate amefunga mara mbili wakati West Ham wakati timu hiyo ikicheza mchezo wake wa kwanza katika dimba lake jipya kwa kuifunga NK Domzale na kutinga hatua ya mtoano ya Ligi ya Uropa.

Ikiwa nyuma kwa magoli 2-1 katika mchezo wa awali, wagonga nyundo hao walisawazisha wingi wa magoli baada ya Kouyate kufunga goli la kwanza katika dimba hilo la zamani la michezo ya Olimpiki ambapo sasa ni uwanja wa London.

Kouyate tena aliunganisha wavuni krosi ya Sam Byram na baadaye Sofiane Feghouli kupachika goli la tatu na kuifanya West Ham kuibuka na ushindi wa magoli 3-0 na kuwatoa NK Domzale kwa matokeo ya jumla ya magoli 3-2.
                           Cheikhou Kouyate akiunganisha krosi na kupachika goli wavuni
              Sofiane Feghouli akiachia shuti lililojaa wavuni na kuandika goli la tatu

WAHAMIAJI KUTOKA AFRIKA WAPIGWA MABOMU YA MACHOZI NA KUKAMATWA UFARANSA

IRANI YAWANYONGA WAPIGANAJI 20 WAISLAMU WA DHEHEBU LA SUNNI

TAJIRI WA LEICESTER CITY AWAAMBIA ARSENAL MAHREZ HAUZWI

WAPIGANAJI WASHAMBULIA MSAFARA WA WATALII AFGHAN NA KUWAJERUHI

SERENGETI BOYS WAWASILI AFRIKA KUSINI, KUSHUKA UWANJANI JUMAMOSI

Nyota wa timu ya Mpira wa Miguu ya Vijana wenye umri wa chini ya miaka 17 – Serengeti Boys wakiwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa O.R. Tambo jijini Johannesburg, Afrika Kusini wakitokea Antananarivo, Madagascar walikoweka kambi kujiandaa na mchezo dhidi ya Afrika Kusini kwenye mchezo wa kuwania nafasi ya kushiriki fainali za Kombe la Mataifa kwa vijana wenye huo hapo mwakani. Serengeti Boys itakipiga na Afrika Kusini Jumamosi kwenye Uwanja wa Dobsonville, Johannesburg, Afrika Kusini. (Picha na Alfred Lucas wa TFF)
Nyota wa timu ya Mpira wa Miguu ya Vijana wenye umri wa chini ya miaka 17 Serengeti Boys na viongozi walipowasili Hoteli ya Garden Court Milapark ambako imepiga kambi kabla ya kuivaa Afrika Kusini kwenye mchezo wa kuwania nafasi ya kushiriki fainali za Kombe la Mataifa kwa vijana wenye huo hapo mwakani. Serengeti Boys itakipiga na Afrika Kusini Jumamosi kwenye Uwanja wa Dobsonville, Johannesburg, Afrika Kusini. (Picha na Alfred Lucas wa TFF)

SERIKALI MKOANI SIMIYU YAAMUA ASILIMIA MBILI YA USHURU WA PAMBA IJENGE MADARASA

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. Anthony J. Mtaka (Katikati) akizungumza na Viongozi wa Mkoa huo na Wajumbe wa Kamati za Fedha, Mipango na Uongozi kutoka katika Halmashauri za Mkoa huo katika kikao kilichofanyika Mjini Bariadi, kujadili mikakati ya ujenzi wa vyumba vya madarasa, (kushoto) Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu, Jumanne A. Sagini na (kulia) Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, mhe. Festo S. Kiswaga
Wakuu wa Wilaya wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Simiyu (hayupo pichani) katika kikao cha kujadili mikakati ya ujenzi wa vyumba vya madarasa mkoani humo, mstari wa kwanza kutoka kushoto, Mhe. Benson Kilangi (Itilima), Joseph Chilongani (Meatu), Seif Shekalaghe, Tano Mwera (Busega) na mstari wa pili, kutoka kushoto, Mhe. Stanslaus Nyongo(Mbunge Maswa Mashariki), Mhe. Mashimba Ndaki (Mbunge Maswa Magharibi).
  Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu, Jumanne A. Sagini akizungumza kabla ya kumkaribisha Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony J. Mtaka (kulia) ili azungumze na Viongozi wa Mkoa huo na Wajumbe wa Kamati za Fedha, Mipango na Uongozi kutoka katika Halmashauri za Mkoa huo, katika kikao kilichofanyika Mjini Bariadi, kujadili mikakati ya ujenzi wa vyumba vya madarasa.
Viongozi na baadhi Wajumbe wa Kamati za Fedha, Mipango na Uongozi wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Simiyu (hayupo pichani) katika kikao cha kujadili mikakati ya ujenzi wa vyumba vya madarasa mkoani humo kilichofanyika Mjini Bariadi.

MHANDISI MASAUNI AZINDUA MKAKATI WA BARAZA WA KUKABILIANA NA AJALI ZA BARABARANI NCHINI

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Mhandisi Hamad Masauni akizungumza na Waandishi wa Habari (hawapo pichani) mara baada ya kuzindua Mkakati wa Baraza wa Kukabiliana na Ajali za Barabarani nchini. Mkakati huo wa miezi Sita ambao unalenga kukabiliana na ajali umenza mwezi huu Agosti na unatarajiwa kumalizika mwezi Februari 2017 ambapo tathmini itatolewa. Kulia ni Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini, ambaye pia ni Katibu Mtendaji wa Baraza hilo, Kamanda Mohammed Mpinga. Uzinduzi huo umefanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Wizara, jijini Dar es Salaam. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Mhandisi Hamad Masauni akizungumza na Waandishi wa Habari mara baada ya kuzindua Mkakati wa Baraza wa Kukabiliana na Ajali za Barabarani nchini. Mkakati huo wa miezi Sita ambao unalenga kukabiliana na ajali umenza mwezi huu Agosti na unatarajiwa kumalizika mwezi Februari 2017 ambapo tathmini itatolewa. Kulia meza kuu ni Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini, ambaye pia ni Katibu Mtendaji wa Baraza hilo, Kamanda Mohammed Mpinga. Uzinduzi huo umefanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Wizara, jijini Dar es Salaam. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

No comments :

Post a Comment