Sasha
Obama, binti wa rais wa Marekani Barack Obama, ameacha kwa muda
kudeka Ikulu na kufanya kazi ya uhudumu kwenye kaunta ya hoteli ya
vyakula vya baharini.
Shasha
mwenye miaka 15 amechukua kibarua cha muda katika majira ya joto kwa
sasa katika eneo la biashara huko Martha's Vineyard, Massachusetts.
Sasha,
anatumia jina lake kamili la Natasha, amekuwa akisindikizwa kwenda
kufanya kazi kwenye hoteli hiyo na walinzi wa rais sita kwa mujibu wa
Boston Herald.
NYOSHI EL SADAT AHAIDI KUWAPAGAWISHA WAKAZI WA JIJI LA ARUSHA
WAKURUGENZI WA MIKOA YA KANDA YA KASKAZINI WATAKIWA KUJENGA MABANDA YA KISASA YA MAONYESHO YA NANE NANE
Wa
kwanza kulia ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa Maiko Lekule Laiser ,akifuatiwa
na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Daud Filex Ntibenda, aliyepo kushoto kwa mkuu
huyo ni mwenyekiti wa Taso kanda ya Kaskazini ndugu Athar Kitonga Shayo
wakiwa katika uzinduzi wa maonyeho hayo ya wakulima na wafugaji katika
viwanja vya Taso Themi nanenane Njiro Jijini Arusha.MKUU WA MKOA WA MWANZA AFUNGUA RASMI MAONESHO YA NANENANE KANDA YA ZIWA
Mkuu
wa mkoa wa Mwanza, John Mongela (wa pili kulia, akikagua banda la
Benki Kuu, kwenye Maonesho ya Nanenane yanayofanyika kwenye uwanja wa
Nyamuhongolo Jijini Mwanza, kwa mikoa ya Kanda ya Ziwa
Mkuu
wa mkoa wa Mwanza, John Mongela, akisaini kitabu cha wageni kwenye
banda la Benki kuu, kwenye maoneshp ya Nanenane Jijini Mwanza.
Mkuu
wa mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack (kushoto) akiteta jambo na Mkuu
wa mkoa wa Mwanza, John Mongella (kulia)
Mcheza
ngoma wa kikundi cha kutoka Bujora akitumbuiza huku akicheza na nyoka
Na, Binagi Online TV
Mkuu
wa mkoa wa Mwanza, John Mongela, ameiagiza Mamlaka ya Usimamizi wa
Biashara Tan-trade kukamilisha ramani ya viwanja vya Nyamuhongolo
vinavyotumika kwa maonesho ya Wakulima na Wafugaji Nanenane ili
kuanza ujenzi wa majengo ya kudumu kwenye viwanja hivyo.
Akifungua
rasmi jana maonesho ya Nanenane yanayohusisha mikoa ya Kanda
ya
ziwa, Mongela, alisema kukamilika kwa ramani hiyo kutaharakisha
kuanza kwa ujenzi wa mabanda ya kudumu kwenye viwanja hivyo ili
kuwezesha kuendelea kwa shughuli mbalimbali hata maonesho
yatakapomalizika.
Alisema
mkoa wa Mwanza kwa kushirikiana na mikoa mingine ya kanda ya ziwa,
umejipanga kuandaa maonesho ya Nanenane kitaifa ndani ya miaka miwili
ijayo, hivyo ujenzi wa mabanda hayo utachangia kuongeza hamasha ya
mikoa hiyo kuwa mwenyeji.
Aidha
mkuu huyo wa mkoa wa Mwanza ameungana na mwenzake wa mkoa wa
Shinyanga, Zainab Telack, kuwahamasisha wakulima wa mikoa hiyo
kufufua kilimo cha
pamba ambacho amesema kitachangia kufufua viwanda mbalimbali na
kuongeza fursa za ajira hasa kwa vijana na hivyo kukuza pato la
familia na taifa kwa jumla.
CHEIKHOU KOUYATE APACHIKA MAWILI WAKATI WEST HAM IKITINGA HATUA YA MTOANO LIGI YA UROPA
Mchezaji
Cheikhou Kouyate amefunga mara mbili wakati West Ham wakati timu hiyo
ikicheza mchezo wake wa kwanza katika dimba lake jipya kwa kuifunga
NK Domzale na kutinga hatua ya mtoano ya Ligi ya Uropa.
Ikiwa
nyuma kwa magoli 2-1 katika mchezo wa awali, wagonga nyundo hao
walisawazisha wingi wa magoli baada ya Kouyate kufunga goli la kwanza
katika dimba hilo la zamani la michezo ya Olimpiki ambapo sasa ni
uwanja wa London.
Kouyate
tena aliunganisha wavuni krosi ya Sam Byram na baadaye Sofiane
Feghouli kupachika goli la tatu na kuifanya West Ham kuibuka na
ushindi wa magoli 3-0 na kuwatoa NK Domzale kwa matokeo ya jumla ya
magoli 3-2.
Cheikhou Kouyate akiunganisha krosi na kupachika goli wavuni
Sofiane Feghouli akiachia shuti lililojaa wavuni na kuandika goli la tatu
SERENGETI BOYS WAWASILI AFRIKA KUSINI, KUSHUKA UWANJANI JUMAMOSI
Nyota
wa timu ya Mpira wa Miguu ya Vijana wenye umri wa chini ya miaka 17 –
Serengeti Boys wakiwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa O.R. Tambo
jijini Johannesburg, Afrika Kusini wakitokea Antananarivo, Madagascar
walikoweka kambi kujiandaa na mchezo dhidi ya Afrika Kusini kwenye
mchezo wa kuwania nafasi ya kushiriki fainali za Kombe la Mataifa kwa
vijana wenye huo hapo mwakani. Serengeti Boys itakipiga na Afrika Kusini
Jumamosi kwenye Uwanja wa Dobsonville, Johannesburg, Afrika Kusini.
(Picha na Alfred Lucas wa TFF)
Nyota
wa timu ya Mpira wa Miguu ya Vijana wenye umri wa chini ya miaka 17
Serengeti Boys na viongozi walipowasili Hoteli ya Garden Court Milapark
ambako imepiga kambi kabla ya kuivaa Afrika Kusini kwenye mchezo wa
kuwania nafasi ya kushiriki fainali za Kombe la Mataifa kwa vijana wenye
huo hapo mwakani. Serengeti Boys itakipiga na Afrika Kusini Jumamosi
kwenye Uwanja wa Dobsonville, Johannesburg, Afrika Kusini. (Picha na
Alfred Lucas wa TFF)
SERIKALI MKOANI SIMIYU YAAMUA ASILIMIA MBILI YA USHURU WA PAMBA IJENGE MADARASA
Mkuu
wa Mkoa wa Simiyu Mhe. Anthony J. Mtaka (Katikati) akizungumza na
Viongozi wa Mkoa huo na Wajumbe wa Kamati za Fedha, Mipango na Uongozi
kutoka katika Halmashauri za Mkoa huo katika kikao kilichofanyika Mjini
Bariadi, kujadili mikakati ya ujenzi wa vyumba vya madarasa, (kushoto)
Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu, Jumanne A. Sagini na (kulia) Mkuu wa
Wilaya ya Bariadi, mhe. Festo S. Kiswaga
Wakuu
wa Wilaya wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Simiyu (hayupo pichani) katika
kikao cha kujadili mikakati ya ujenzi wa vyumba vya madarasa mkoani
humo, mstari wa kwanza kutoka kushoto, Mhe. Benson Kilangi (Itilima),
Joseph Chilongani (Meatu), Seif Shekalaghe, Tano Mwera (Busega) na
mstari wa pili, kutoka kushoto, Mhe. Stanslaus Nyongo(Mbunge Maswa
Mashariki), Mhe. Mashimba Ndaki (Mbunge Maswa Magharibi).
Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu, Jumanne A. Sagini akizungumza kabla ya
kumkaribisha Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony J. Mtaka (kulia) ili
azungumze na Viongozi wa Mkoa huo na Wajumbe wa Kamati za Fedha, Mipango
na Uongozi kutoka katika Halmashauri za Mkoa huo, katika kikao
kilichofanyika Mjini Bariadi, kujadili mikakati ya ujenzi wa vyumba vya
madarasa.![]() |
| Viongozi na baadhi Wajumbe wa Kamati za Fedha, Mipango na Uongozi wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Simiyu (hayupo pichani) katika kikao cha kujadili mikakati ya ujenzi wa vyumba vya madarasa mkoani humo kilichofanyika Mjini Bariadi. |





























No comments:
Post a Comment